Habari zilizoifikia blogu hii ya watu, hivi punde zinasema mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni ya executive solutions ya jijini dar es sallaam, bw. Alan robert turner amefariki dunia nchini afrika kusini mchana wa leo alipokwenda kuchekiwa afya yake kama iliyo ada yake kila mwaka.aliondoka akiwa mzima wiki iliyopita, na vipimo vya kidaktari vilionesha yu bheri wa afya.lakini siku mbili baadaye akazimia na kudondoka, kisha akarejeshwa tena hospitali, ambako hali yake ikazidi kudorola mpaka mauti yalipomfika jumanne mchana.
Bw.turner pichani juu, ni raia wa uingereza, aliyeishi nchini afrika kusini kwa muda mrefu alijiunga na kampuni ya executive solutions miezi michache baada ya kuanzishwa kwake na aggrey marealle mwaka 2004.alikuwa akiishi mbezi beach dar es salaam jirani na hoteli ya jangwani sea breez na white sand.
Mkurugenzi huyo ambaye alikuwa ndiye wa pili kimadaraka baada katika kampuni hiyo ya mkurugenzi mtendaji aggrey marealle atakubmbukwa sana na wafanyakazi wote wa kampuni hiyo hasa media relations managers benjamin thompson na ibrahim kyaruzi ambao ndio wamefanya naye kazi tangu mwaka 2004. Pole sana bw marealle kwa kuondokewa na nguzo yako hiyo. Bwana alitoa na sasa ametwaa.
Mipango ya mazishi itafahamika kesho baada ya kupata taarifa ya familia yake huko afrika kusini.
Blogu ya watu inatoa pole kwa wafiwa wote hasa executive solution..