Alama za nyakati baada ya 25 oct. 2015

Alama za nyakati baada ya 25 oct. 2015

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Posts
8,596
Reaction score
5,584
Nilipata kuandika hapa nini kitatokea chadema na vyama vingine vya upinzani mwaka 2010. Naandika tena hii leo hii sio ramli wala unajimu ni kuzisoma alama za nyakati zinasemaje?

Ziko njia mbili pekee nizionazo, yako mambo matatu yaweza kutokea:

Njia:
1. Mabadiliko ya kweli ikiwa ukawa itaingia madarakani, japo kutakuwepo changamoto za awali (kipindi cha mpito) hakitazidi miezi sita kwani mh. Lowassa anawafahamu watendaji wazuri waliopo katika serikali ya sasa ambao akiunganisha nguvu atajenga serikali imara yenye uwezo wa kutekeleza ilani ya ukawa.


Wananchi wengi watakuwa na matumaini na hamasa kubwa ya kurudisha uzalendo na ari ya kutumikia nchi. Idadi ya watanzania wenye mitaji na ujuzi watavutiwa kurudi nyumbani kuwekeza wakiwa na amani kuliko urasimu waliokutana nao awali walipojaribu kufanya hivyo. Sitozungumzia uwekezaji uliopo kwa sasa. Na mambo yakienda kombo wataweza kujieleza mapema na wananchi wataelewa, punde mambo yatakaa sawa na nchi itapata maendeleo ya haraka kuliko wakati wowote ndani ya miaka minne hadi mitano ya kwanza.

2. Ni serikali ya Magufuli!!! Kama inavyolazimishwa kuitwa, hii ni serikali ya CCM ambayo wananchi wameshakata nayo tamaa. Inawezekana mh. Magufuli akaanza kwa kasi kama alivyoanza mzee ruksa au zaidi, kasi yake itazuiwa kwa nguvu na mashinikizo makubwa toka kwa wanasiasa wakongwe kiasi kwamba atakata tamaa na kukosa uvumilivu, hapa mvurugano mkubwa wa wenye chama na wanachama wa CCM utajitokeza wazi na kukipasua rasmi lakini pia bila kuiacha salama serikali yao.

Upande wa pili wananchi walioweka matumaini kwa serikali ya magufuli watakata tamaa na kuanza kupinga waziwazi huku wakibeba mabango ya kudai ahadi alizotoa. Mambo haya yatamchanganya na sitoshangaa akitumia mkono wa chuma kutuliza hali ya mambo kama si kutawala. Vilio na kulaani vitaenea toka mashariki mpaka magharibi, kaskazini na kusini. Hali ya mambo itazorota na wafanyabiashara watakata tamaa.

Kati ya hizo njia mbili watanzania wana hiyari ya kuchagua moja inayowafaa.

Matokeo matatu.
1. Ikiwa uchaguzi utafanyika kwa haki, mshindi wa ngazi yoyoye iwayo akapata haki yake na matokeo yakawa halali amani itakuwa maradufu ya awali na dalili za maendeleo na ukuaji demokrasia itakuwa dhahiri.

2. Ikiwa wizi au ujanja wowote uwao kwa mgombea yeyote awaye ili kushinda uchaguzi basi mengi yatajitokeza ikiwamo kutokuwajibika na hujuma zinginezo hali itakayopelekea mshindi husika kudharaulika na kutoaminika tena.

3. Iwapo mshindi yeyote au chama chochote watakapojitambua kuwa hii nchi ni ya watanzania na kila mtanzania ana haki ya kushiriki uongozi ama utawala na wakashirikiana basi pia litakuwa jambo la kheri na tanzania itang'ara na kupaa kutoka tulipo kwenda kwenye mafanikio,kinyume na hapo... Ni giza giza tupu.

Kwa ufupi ni hayo ndugu zangu. Tunaitazama tanzania, wapi tulikuwa, wapi tupo, wapi tunapelekwa. Wako watu wamejenga chuki kwa mtindo wa kutengeneza tatizo ili watafute ufumbuzi baada ya uchaguzi je wanao uhakika gani na hayo masuluhisho hao kufaulu?

Ninasubiri kuona, kazi yangu ni kukumbusha na kuonya basi.

Mungu ibariki Tanzania.
 
[h=3]KATA HUYU MTU MAPEMA 25 OKTOBA, 2015 ILI ARUDI KWAO MONDULI[/h]

905557_123322234692824_1422191204904747446_o.jpg
 
Umesahau namba 1 huyo akiingia tu chakwanza kuchukua vitaru vya ges na kumpa rafiki yake …
 
Umesahau namba 1 huyo akiingia tu chakwanza kuchukua vitaru vya ges na kumpa rafiki yake …

Avichukue kutoka kwa JK na wachina wake si ndio? Make kwa sasa vinamilikiwa na nanihii
 
Hiyo namba 2 nakubaliana nayo kwa 100% watu hawatakuja kuamini
 




Maisha yana asili ya ukatili. Falsafa husema "usimhurumie kiumbe usiyemuumba!"

Watu watavuna hawataiona tija! Wako wanaotaraji neema hawataiona itakuwa kama mazigazi jangwani. Wajinga na malofa watapanda huku wenye elimu na ukwasi wakishuka!

Mola atuepushe na madhila, Oktoba yaja.
 
Tatizo ni kuwa nchi hii wananchi bado wanalala usingizi fo for fo fo!

Yaani usingizi zaidi ya ule wa pono!
Walipotaka kuamka kupitia Bunge Live huko nako wakafungiwa. Technically wakarudishwa usingini kwa sababu za kijinga kweli kweli!

Imefika hatua ni bora matukio ya Ikulu, rais au ccm yawe live kuliko Bunge na mengineyo.

Hivyo itatuchukua muda mrefu kiasi kupata mabadiliko! Kumbuka mabadiliko yana hatua na dalili zake. Mabadiliko uongozwa na muda!

Tunahitaji muda kuliko tunavyohitaji majina ya watu na vyama!
 
Maisha yana asili ya ukatili. Falsafa husema "usimhurumie kiumbe usiyemuumba!"

Watu watavuna hawataiona tija! Wako wanaotaraji neema hawataiona itakuwa kama mazigazi jangwani.

Wajinga na malofa watapanda huku wenye elimu na ukwasi wakishuka!!
Mola atuepushe na madhila.

Oktoba yaja. Mwanamageuko,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshana Jr,
Muumbaji alimuumba mwanadamu akampa uwezo wa kufikiri na kutambua mazingira yake ili aweze kuyamudu na kuyatawala... mwanadamu ana asili ya kutofuata matakwa yake bali ushawishi usio na manufaa kwake ambao humletea laana!!! Rejea "Adam na Hawa.... Samson na Delilah..."
Tusubiri tu yajayo...
Tumuombe sana Mola atuvushe salama kwani giza nene limetanda...
 
Jp Omuga,
Hakika hakika Mkuu... nasi kwa kutojipenda ati tunapenda sana majina ya watu na vyama kuliko muda wetu...
Tuna visingizio vyepesi tu...
 
Back
Top Bottom