Alama za Barabarani

uniq

JF-Expert Member
Nov 22, 2011
5,089
31,085
Kumekuwa na video inayo sambaa juu ya kibao cha alama za barabarani huko Rusumo - Ngara.
Kwa uelewa wangu ile video ina potosha sana ukweli huyu mtu anaeongea hata hajuii nini maana ya kile kibao.
Kuna vibao vya aina nyingi barabarani ambavyo Dereva anatakiwa kuwa makini navyo. Kuna vibao vya pembe Tatu na Duara, kuna vilivyo andikwa kwa wino mwekundu na mweusi. Vyote hivi vina maana yake na dereva anatakiwa kujua kama alikwenda shule ya udereva lazima uwe umefundishwa.
Kwenye video hii unaona kibao cha duara chenye maandishi meusi na mistari mitatu iliyokatisha.

Nini tafsiri ya alama hii, kwa wale wote wanaopita njia hiyo lazima wawe makini sana.

Kabla ya kibao hicho lazoma nyuma yake kutakuwa na kibao cha kukuonyesha kutembea 50km/h na unapo kutana na hicho kibao chenye rangi nyeusi na mistari mweusi iliyokata ujue kuwa inatakiwa kutembea kwa speed iliyoonyesha kwenye kibao na ile mistari ina simama kuonyesha umbali unaotakiwa kutembea kwa speed hiyo (distance). Kila mstari mmoja unaonyesha mita moja. Kwahiyo mistari mitatu ni mita mia tatu mbele.

Kwa hiyo kibao kipo sehemu sahihi kabisa na kinataka kila dereva kuendesha gari kwa speed ya 50km/h kwa umbali wa wa mita miatatu mbele baada ya hicho kibao.

Huyu ndugu alie irekodi hii vidieo anatakiwa kuelewa hilo. Pia nijambo la kushukuru sana kwa yeye kuleta hii hoja maana nina uhakika itasaidia sana uelewa wa hizi alama za barabarani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom