Alama hii inamaninisha nini?

Juakali jr

Member
Joined
Aug 8, 2019
Messages
28
Points
75

Juakali jr

Member
Joined Aug 8, 2019
28 75
Nini maana ya ABS mkuu?
ABS ni mfumo wa braking (Anti Lock Braking).
Ambao kazi yake ni kusaidia gari kuweza kusimama kwa haraka zaidi na kupunguza utelezi wakati wa usimamaji.
Kuilezea ABS ni changamoto kidogo kwa sababu imekaa kifizikia zaidi, ila kwa haraka haraka elewa
1. kukanyaga brake wakati ukiwa kwenye speed, matairi yanalazimishwa yasitembee ila haimaanishi gari nalo litasimama wakati huo. Mara nyingi litateleza na kuacha alama za matairi kwenye barabara.
2. Ili gari likunje kona linahitaji matairi yawe yanatembea, kwa hiyo kama umekanyaga brakes unazuia matairi yasitembee, ki nadharia hutoweza kukunja kona hata kama umeyakunja matairi yaende uelekeo wa kona hiyo.
Ilikuondoa hizo changamoto mfumo wa ABS unakataza matairi yasitembee kwa wakati fulani na kuyaruhusu tena yatembee kidogo kwa muda kidogo hata kama ukiwa bado umekanyaga brakes.
Hiyo taa kuwaka maana yake, gari lako linahitillafu kwenye huo mfumo, brake zinaweza zikawepo na zikawa zinafanya kazi lakini mfumo wa ABS ndo utakua unakosekana
 

Forum statistics

Threads 1,364,616
Members 520,767
Posts 33,322,931
Top