Al-Shabab waingia nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Al-Shabab waingia nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 17, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]WEDNESDAY, 16 NOVEMBER 2011 19:35 NEWSROOM  WATANZANIA 10 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali nchini Somalia, wakituhumiwa kushirikiana na kikundi cha kigaidi cha wanamgambo wa Al-Shabab. Aidha, serikali imetahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea kwa mashambulio ya kigaidi nchini, hivyo wananchi kutakiwa kuwa macho na kutoa ushirikiano kwa serikali.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, alitoa tahadhari hiyo jana, alipozungumza na waandishi wa habari juu ya uwezekano wa kutokea mashambulio ya kigaidi kama yaliyotokea nchi jirani za Kenya na Uganda.


  Alisema Watanzania hao walikamatwa na wanajeshi wa Kenya walioingia nchini humo wakiwa katika harakati za kuwasaka wanamgambo wa Al-Shabab.


  Hata hivyo, alisema baada ya kufanya mawasiliano na Kenya na kukabidhiwa Watanzania hao, walihojiwa na kuchukuliwa taarifa muhimu, ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa alama za vidole kisha kuachiwa.


  Kwa mujibu wa Nahodha, watuhumiwa hao waliachiwa kwa kuwa taarifa muhimu ziko mikononi mwa vyombo vya usalama, wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.


  Nahodha alisema kutokana na kushambuliwa kwa nchi za Kenya na Uganda, Tanzania haiko salama kwa kuwa wakati wowote linaweza kutokea lolote.


  "Tumejiandaa vya kutosha kukabiliana na hali yoyote itakayotokea, lakini ni muhimu wananchi wakatusaidia kwa kutoa taarifa kuhusu mienendo ya watu wanaowatilia shaka," alisema Waziri Nahodha.


  Akifafanua jinsi wananchi wanavyoweza kutia shaka mienendo ya watu wasiowajua, alisema ni pamoja na kuhoji mambo na kutaka kupata taarifa ofisi za kibalozi na maeneo mbalimbali ya ofisi nchini.


  Mbali na hilo, alisema endapo watajitokeza raia wa kigeni wanaowarubuni vijana kwa kuwadanganya watawapeleka nje ya nchi na kuwapatia kazi watoe taarifa haraka, kwani ni moja ya viashiria vya magaidi hao.


  "Kukamatwa kwa vijana hao na kuongezeka kwa idadi ya wahamiaji haramu kutoka nchini Somalia, yote hayo yanaashiria uwezekano wa kuingia Al-Shabab na kufanya vitendo vya kigaidi," alisema.


  Alisema serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za tahadhari, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za mienendo ya hali ya usalama, kulinda mipaka na kushirikiana na nchi jirani kukabiliana na ugaidi.


  Wakati huo huo, Waziri Nahodha, alisema amepata majina manane ya maofisa wa juu wa Idara ya Uhamiaji nchini wanaotajwa zaidi kujihusisha na vitendo vya rushwa.


  Kutokana na hilo, alisema amewaeleza maofisa hao kuhusu tuhuma hizo ili wakae wakijijua pamoja na kuwapa muda wa mwezi mmoja kujirekebisha kabla ya hatua dhidi yao hazijachukuliwa.


  Hata hivyo, hakutaja majina ya maofisa hao kwa maelezo kwamba muda wa kufanya hivyo bado haujafika.


  Aidha, aliwataka wananchi kushirikiana na serikali kuwafichua wahamiaji haramu wanaoingia nchi.


  Kwa upande wa serikali alisema imechukua hatua kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuwatimua nchini raia wawili wa Pakistan waliokuwa vinara wa uingizaji wageni kinyume cha taratibu.


  Kikundi cha Al-Shabab kimekuwa tishio kwa ulinzi na usalama wa nchi za Afrika Mashariki, kutokana na mashambulizi kadhaa yaliyofanyika katika nchi za Kenya na Uganda.


  Hivi sasa Kenya inaendelea na mapambano na kuwatafuta wafuasi wa Al-Shabab katika maeneo mbalimbali, ikiwemo nchini Somalia.


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Usalama Nchini... na hivi tulivyo na big income gap? tutakoma!!
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nenda ukasome makala za Mohamed Said.
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Who is Mohamed Said????
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  wanatafutasababu za kuzuia maandamani ya cdm na wana harakati..tumewashitukia hao
   
 6. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bora al-shabab kuliko serikali kandamizi na kifisadi ya ccm.
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa! Nimeipenda hii!
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Huu nao ni usanii wa serikali ya M.kwere! Tutaandamana bila kibali waache kutumia mgongo wa Al-shabaab!
   
 9. N

  N series Senior Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli,bora al shabaab kuliko m-kwere na system yake
   
 10. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Waje tujiunge nao tu....tumechoka kuishi kama wakimbizi kwenye nchi yetu.Mwisho wa CCM U KARIBU..
   
 11. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,582
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Mbona wapo siku nyingi tu, mkurugenzi mkazi wao ni kiongozi mwandamizi wa CCM na mwingine ni mbunge yule anayependa kuringishia kibastola chake kila anapokwenda.
   
 12. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,268
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
  Katika harakati za kuogopa maandamano ya kuupinga huu mswada feki lazima watangaze hayo kuwatia hofu watanzania.

  This time wameongeza akili kidogo wameanzia mbali.
   
 13. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  'Scholar' mmoja wa Gerezani!
   
 14. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Hii ni kazi ya intelejensia yetu, watu uwakamate kwenye vita wakishutumiwa kushirikiana na wahalifu wa kivita, kisha unasema umewaacha kwa kua umechukua taarifa zao muhimu, mbona wezi wa kuku wengi wako rumande na magerezani? kwanini msichukue taarifa zao muhimu kisha muwaachie? Serikali inatafuta namna ya kutanga hali ya hatari ili iweze kubana upinzani na kufanikisha ushenzi wao.
   
Loading...