Al Shabaab yatishia Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Al Shabaab yatishia Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BabuK, Jan 4, 2012.

 1. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  KUNDI la kigaidi nchini Somalia lenye uhusiano na al Qaeda, la al Shabaab limetishia kufanya mashambulizi Tanga na Kilimanjaro na tayari vyombo vya usalama mkoani Kilimanjaro, vimetoa hadhari katika maeneo ya viwanda vinavyoweza kushambuliwa.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Absalom Mwakyoma, alithibitisha kuwapo kwa tishio hilo lakini alikataa kuzungumzia zaidi kwa madai ni la kiusalama zaidi.

  “Hilo jambo lipo lakini sitalizungumzia, kwani ni mambo ya kiusalama zaidi…wewe nani amekupa taarifa hizo, muulize aliyekwambia akufafanulie,” alisema.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Mtendaji Utawala wa Kiwanda cha Sukari cha TPC, Jaffary Ali, wamepewa taarifa za kuchukua hadhari juu ya kuwapo kwa tishio la shambulio kiwandani hapo.

  Alisema taarifa hizo zimetolewa na Kamanda Mwakyoma baada ya kupata taarifa mbalimbali za kiusalama zilizopatikana juu ya kuwapo kwa tukio hilo.

  “Ni kweli tumepata taarifa za kuwapo kwa shambulio la kikundi cha al Shabaab lakini haijataja moja kwa moja kwamba sisi ndio tunashambuliwa ila tumetakiwa kujihadhari na watu, magari na hata pikipiki, tusizozifahamu,” alisema.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda Mwakyoma, huenda kikundi hicho kikatekeleza mashambulizi yao kwa kutumia pikipiki, jambo ambalo linasababisha kutilia shaka vyombo vyote vya usafiri vinavyopita kiwandani hapo.

  Alisema kutokana na taarifa hizo, tayari kiwanda kimetoa hadhari kwa wafanyakazi wake, viongozi wa vijiji vinavyozunguka kiwanda pamoja na familia za wafanyakazi kuwa makini
  dhidi ya watu wasiowafahamu.

  “Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda, kwa Tanga kimetajwa kiwanda cha saruji, lakini huku kwetu tumehadharishwa katika maeneo haya ya viwanda, kwani ndiyo lengo lao, tumewataka wafanyakazi wasiwe na hofu, lakini pia tunaendelea na kazi,” alisema.

  Alisema menejimenti imeimarisha ulinzi katika eneo la kiwanda, lakini pia imeagiza mbwa maalumu wa kutambua mabomu kutoka Arusha ili kusaidia ukaguzi wa maeneo yote.

  Alisema wafanyakazi wa mashambani wamepewa taarifa kuhusu ubebaji miwa, kwani huenda
  wakabeba bomu na kuliingiza kiwandani, iwapo kikundi hicho kitatega kupitia mashamba.

  "Hawa mbwa tulioagiza watafanya doria maeneo yote ya kiwanda na mashamba kutokana na
  hofu kwamba wakitumia mashamba ni rahisi kuyabaini," alisema.

  Kwa upande wao, baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha TPC, waliojitambulisha kwa jina moja la Mziray na Juma, walisema tishio hilo limeleta hofu, kwani athari za mashambulizi ya kikundi hicho ni makubwa.

  Alisema wameshuhudia mara kadhaa kupitia vyombo vya habari, katika nchi za Kenya na Uganda, jinsi ambavyo vimeshambuliwa na kikundi hicho na kusababisha vifo vya mamia ya wananchi wasio na hatia.

  "Hili tishio limetulazimu kuhamisha baadhi ya wanafamilia wetu, tumewataka waende mjini
  Moshi kuishi na ndugu," alisema.

  Akizungumzia taarifa hizo, mkazi wa kijiji cha Langasani wilayani Moshi vijijini, Abdul Sultan, alisema ni vyema Serikali ikaimarisha usalama katika mipaka ili kudhibiti kikundi hicho.

  Alisema pamoja na suala la mipaka ya nchi, lakini pia zipo sababu za msingi kwa wananchi kupewa elimu ya utambuzi wa watu wenye nia ovu ili iwasaidie kukabiliana na watu hao.

  Kikundi cha al Shabaab kimekuwa kikifanya vitendo vya ugaidi ndani ya Somalia, Uganda na Kenya hata kulazimu majeshi ya Kenya kuingia nchini Somalia kukabiliana nacho.

  Chanzo: HabariLeo
   
 2. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Hao nao wameshindwa nini kwenda magogoni. Matahira tu hao waoga sana hawa. Waje kwangu niwashikishe adabu pumbavu zao
   
 3. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ujinga na ushoga mtupu.
  Hawa polisi wetu inaonekana hawana kazi za kufanya ndio maana wanazusha mambo ya kishoga shoga. Imefika wakati majeshi yetu yapunguzwe ili badala pesa kuliwa bure zitumike zinakohitajika.

  Hakuna tena maadui enzi hizi. Vikosi vya kupambana na majambazi vinatosha. Adui kwa sasa angekuwa ni mmoja tu kwa nchi zote;Marekani na Israel kwani ndio wanaotishia amani ya dunia.Kwa vile tumewafanya marafiki na watoa sera za ulinzi wa nchi zetu hivyo majeshi yetu yanakuwa upuuzi mtupu kuendelea nayo.

  Hatimae huwa wanakunywa pombe nyingi huko makambini kwao halafu kuzusha fitna.
  Turudi kuchambua hao watu wanaoitwa Alshabaab.S ababu zaweza kuwa ni zipi za wao kutaka kupiga kiwanda cha miwa na kiwanda cha saruji?.Ikitajwa Alshabaab tunaambiwa wana sura za kisomali.Jana tu wasomali 10 wamekufa kama kwamba wamekufa paka ndani ya lori na kutupwa porini.

  Wasomali hao habari zao wala hazijawa muhimu kwa vyombo vingi vya habari tofauti na kama angekufa mbwa Ulaya kwa kutumbukia kwenye pipa la taka.

  Maiti zilizookotwa hazikuwa na majeraha yoyote na inakisiwa walikufa kwa kukosa hewa wakiwa wamefichwa kwenye lori kupelekwa Afrika kusini. Hivi kweli watu wa aina hii wanaokimbia shida wakiwa hawawezi kubeba hata nguo za kutosha wataweza kuingia Tanzania na vifaa vya kuripua viwanda ambavyo havijawakosa chochote.

  Tishio hilo mpaka limeleta usumbufu kwa watu wenye majina ya kiislamu tu kuhamisha familia zao mijini kwa hofu ya mashambulio....Hizi ni habari za kishoga aina ya ushoga wa kipolisi.

  Aibu tupu! Mungu (Allah) tupitishie hukumu kwa fitna hizi ili ubaya wake kwa waliozitenda wauonje hapa hapa duniani.
   
 4. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Naona unataka kupingana na polisi wa nchi yako kwa kutetea wasomali ambao hata kukufahamu hawakufahamu
  pole sana,USA NA ISRAEL zitaendelea kuwa juu kila siku na alshabaab wanapotezwa kwenye ramani ya dunia na wanajeshi wa kenya na ethiopia,utabaki unalia mwenyewe
   
 5. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mimi sipingani na polisi bali napinga uzushi.Kuhusu Israel na USA kuwa juu kila siku ni tamaa zako tu.Hata hivyo Mungu hafuati ratiba za kibinadamu kumpoteza adui yake.Umewahi kusoma habari na vitimbi vya Firauni?.
   
 6. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mungu yupi unayemsema wewe?
   
 7. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Tusidanganyaje Tanzania haipo katika tishio la Al shabaab. Hizi ni siasa za kutisha watu wasiandamane. Gaidi mkuu hapa ni wale wanaotisha watanzania wasiishi vile watakavyo kwa sababu zao za kisiasa. Al shabaab wavamie Tanzania tumewafanya nini?, hatujavamia nchi yao hatuja fanya lolote. Wakuu wa usalama Tanzania acheni kutisha wananchi fanyeni kazi zenu kuhakikisha wanaishi bila kuwa na threat ya kushambuliwa na yeyote yule.

  Kwa nini wakati wa kusheherekea miaka hamsini ya uhuru hatukusikia vitisho hivi na kuwaweka watanzania on alert?. Mimi bado ninaamini kuwa kama kutakuwa na shambulio lololte basi litakuwa limefanywa na wanausalama wa Tanzania ili ku-further political agenda ya kuzuia wapinzani kufanya siasa period, na ikitokea hivyo basi huo ni mwisho wa CCM na mbinu chafu za kukandamiza upinzani
   
 8. m

  mams JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  They are (Police) joking, nguvu zilezile wanazotumia kudhibiti waandamanaji zinatosha kuwadhibiti hao Elshabab.

  We are (The wananchi) serious, kama waandamanaji wanahatarisha usalama wa raia basi hao elshabab ni zaidi . No jokes, tunataka ulinzi.
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Nina hofu kwenye lile kundi la Al-shabaab kuna Watanzania ambao wamechafukwa na mioyo kwa kiwanda cha saruji na sukari kuuza vifaa vya kwa bei ghali utafikiri hatuna Rais!
  Tena ingetakiwa wawe wameshatoa mfano!
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  kwani hawa al shabaab tumewafanya nini?
   
 11. K

  Kanyigo JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 959
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  alshabaab hawawezi kupiga waoga kama sisi,naomba waelekeze mabomu yao magogoni kwenye lile jumba la mkulu.
   
 12. Tz-guy

  Tz-guy JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapa sijakuelewa vizuri, unatetea Uislam au Al Shabaab.
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  naomba bomu walipige limpate malaria sugu
   
 14. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Tumewaudhi kwa ujinga wetu uliopitiliza
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona Tz mna hamu ya milipuko ya ili kundi maana kila mara mnalitaja taja.
  Naona wakikunguta shambulizi moja la kiume mtaacha kuleta masihara na hawa jamaa.
  Maana watu wakitaka andamana mnasingizia ilo kundi
   
 16. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Wewe unadhani wasomali ndio wakufanyiwa kila aina ya majaribio na kusingiziwa!.Huna ubinadamu wa kuwatetea hata pale wanapodhulumiwa.
   
 17. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  hii itakuwa kama ile hadithi ya mtoto na mbwa mwitu; kila siku tunasingizia mashambulio ya al shabab ambayo ni ya kufikirika - kuna siku watatushambulia kweli na watakuta hatujachukua tahadhali yoyote kwa sababu tumeshachukulia ni porojo za kisiasa tu
   
 18. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Al shabab!!!?? From where!!!? Hopeless kabisa
   
 19. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Siasa za maji taka. Eti Alshababu, habari za kutengeza ili kutishia watu wasifanye harakati zao za ukombozi. Hamna lolote wala si chochote.
   
 20. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Huu ni mwendelezo wa zile taarifa za ki'intelijensia au?
   
Loading...