Al Shabaab yatishia Tanzania

Al Shabaab yatishia Tanzania

Soma habari hiyo hapo chini.
Inasikitisha kweli kwamba kauli hizi za kizushi zinaendelea kutoka vinywani mwa makamanda wetu wa Jeshi.

................................................................
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema kuwa uharamia wa kuteka meli unaofanywa na raia wa Kisomali, sasa umeingia katika nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini, Tanzania ikiwamo, na kwamba hali hiyo imeathiri uchumi wa nchi.

Jeshi hilo lilitoa tamko hilo juzi kupitia kwa Mkuu wa Kamandi wa Jeshi la Wanamaji (Navy), Meja Jenerali Said Shaaban Omar, ambaye alisema kuwa athari ya uchumi, ambayo inagusa nchi na mtu mmoja mmoja, inachangiwa na mambo mbalimbali, ikiwamo meli nyingi za kigeni zilizokuwa zikiingia katika bandari ya Dar es Saalam kupungua kutokana na hofu ya kutekwa na maharamia.

Alisema kuwa Kenya, Tanzania, Ushelisheli, mpaka kufikia Mauritius, Madagascar, Comoro na Msumbiji ni eneo, ambalo limekumbwa na uharamia. Alisema kupungua kuingia kwa meli hizo, kunasababisha bidhaa kupanda bei, pia shughuli za uvuvi kupungua kwa vile maharamia hukamata pia meli za uvuvi.

Uharamia pia umeathiri utalii, ambapo meli zilizokuwa zikiingiza idadi kubwa ya watalii nchini zimepungua.

Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2006, meli za aina hiyo zilizoingia nchini zilikuwa 20; lakini mwaka 2010 zilikuwa mbili, wakati mwaka jana haikuja nchini hata meli moja.

JWTZ limesema hivi sasa Tanzania iko katika mchakato mkubwa wa kutafuta mafuta na gesi baharini, lakini mchakato huo unakumbwa na mgogoro mkubwa kwa vile hadi sasa meli za kutafuta mafuta zimekwisha kushambuliwa na maharamia; moja ikiwa imeshambuliwa mwaka juzi na nyingine mwaka jana.

Jambo lingine linalosababishwa na maharamia ni kuzorota kwa hali ya usalama kwa kuwa watu wengi wanapata hofu na hali hiyo inaongeza gharama kwa vile unahitajika ulinzi zaidi.

Hata hivyo, alisema uharamia ni vita kubwa na ni ya dunia nzima, hivyo ina changamoto nyingi, ikiwamo ukubwa wa eneo la bahari, ambalo husababisha kilio cha vitendea kazi, ufinyu wa bajeti na mbinu za maharamia kubadilikabadilika.

Taarifa iliyotolewa na JWTZ inaonyesha jinsi vitendo vya uharamia ni tishio kwa uchumi na usalama wan chi za ukanda huo pamoja na nchi yetu. Pale shughuli za uvuvi, utafiti baharini na usafirishaji wa watalii na mizigo unapokwama maana yake nchi yetu inapata hasara kubwa ya kiuchumi kutokana na kukosa mapato.

Kadhalika, maharamia wanapoingia katika ukanda wetu ni hatari kwa usalama wa nchi yetu kwani ni rahisi kwao kuteka meli pamoja na kufanya vitendo vingine vya uhalifu.

Tunalipongeza jeshi letu kwa kitihada ambazo limezichukua katika kukabiliana na vitendo vya uharamia katika Bahari ya Hindi kwani katika matukio kadhaa limeweza kuokoa baadhi ya meli zilizokuwa katika hatari ya kutekwa na maharamia. Vile vile, limeweza kuwakamata maadhi ya maharamia baada ya kuwashambulia.

Hata hivyo, zipo changamoto ambazo zinakwaza jitihada za kukabiliana na vitendo vya uharamia. Baadhi ya changamoto hizo ni Watanzania kuwa wakarimu kwa wageni, kiasi kwamba kuna baadhi ya wananchi ambao wanatoa hifadhi kwa wageni wakiwemo maharamia bila kujua kwamba watu wa aina hiyo ni hatari kwa usalama wao na wa nchi.

Wageni hao wasiofahamika wanapopewa hifadhi ni rahisi sana kujichanganya na raia na kufanya vitendo vya uharamia. Hivyo basi, njia pekee ya kudhibiti hali hiyo ni kwa wananchi kukataa ukarimu wa aina hiyo.

Changamoto nyingine ni bajeti inayotolewa na serikali kwa JWTZ kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika eneo letu la Bahari. Bajeti hiyo inaelezwa kuwa haitoshi. Jukumu hilo linahitaji fedha za kutosha kwa ajili ya vifaa vya kisasa na shughuli za kufanya doria katika eneo la nchi yetu.

Tunajua kinsi gani serikali imekuwa ikiliwezesha JWTZ katika kukabiliana na tishio la uharamia, ikiwepo kuyaomba baadhi ya mataifa makubwa kusaidia, lakini bado tunasisitiza kuwa jeshi letu lisaidiwe kwa kuongezewa bajeti ili kukabiliana na changamoto za uharamia, ambao sasa umekuwa ni tishio la dunia.
CHANZO: NIPASHE
 
Tuna hamu na mashambulizi? Tunawataja al shabab kuliko hata wakenya!!
 
Back
Top Bottom