Muwindaji
JF-Expert Member
- Feb 28, 2015
- 245
- 206
Kilio changu kili[...], kina[...] na kitaendelea kuhusu madhara ya sera za kibeberu za Marekani na washirika wake wa Magharibi ndio chanzo cha umwagaji damu wote unaotokea hapa Duniani, na tutaendelea kuteseka kwenye hili mpaka Kila upande, nchi au watu watakapokua tayari kuupinga kwa lengo la kuufuta kabisa ubeberu wa kimagharibi.
Jana tarehe 3/04/2015 mwandishi Roberty Baesocchini aliandika makala kupitia mtandao wa WWW.COUNTERCURRENTS.ORG makala isemayo kua kundi la Al Shabaab lililofanya shambulio la kigaidi juzi na kuua wanafunzi wa cho kikuu cha Garrisa WASIO NA HATIA wasiopungua 150 ni moja kati ya makundi yaliyoyonufaika kwa kupata silaha baada ya kumalizika kwa vita ya wamagharibi ya kumng'oa kiongozi shupavu, aliyekua analitakia mema bara la Afrika. Tukumbuke moja kati ya vitu vilivyomponza Gaddafi ni kutaka kuanzisha Benki ya Afrika ambayo ingetoa pesa za maendeleo bila riba wala mashariti yoyote na hivyo kuondokana na uwepo wa vyanzo vya pesa vya kishetani kama IMF na WORLD BANK.
Marekani, Uingereza na Ufaransa ndio walikua mstari wa mbele kuhakikisha Gaddafi anatoka madarakani. Mbaya zaidi waligawa silaha kwa kupitia majeshi ya NATO na kwa vibaraka wake SAUDI ARABIA na UTURUKI ili wazipenyeze kwa makundi ya Itikadi kali kama Al Qaeda, Tuareg na wengineo.
Haraka mno, watoto wa kiarabu ambao ni zao la tatizo la kutokua na ajira linalotokana sera za kibepari wakazigombania na kugawana, wakajumlisha na zile walizozipata kutoka kwenye kambi za Gaddafi wakawa "full equipped" (kwa lugha ya kimombo).
Bila kupumua, mapinduzi ya Mali yakatokea, na waasi wa kaskazini mwa Mali ambapo silaha zilizagaa baada ya vita vya Libya wakajitangazia Uhuru wao. Wakawa hawashikiki, mpaka Ufaransa akaingilia kati kuzima msala huo(Japo inasemekana ilikua ni kwaajili ya kuinusuru maktaba ya Timbuktu ambayo wavumbuzi walipo NASA wanaitegemea kwa nyaraka zake, ambayo tayari ilikua kwenye mikono ya waasi).
Boko Haramu pia ni moja kati ya makundi yaliyonufaika moja kwa moja na ugawaji wa silaha hizo. Na ndio chanzo cha uimara wake ambao tunauona sasa hivi.
Enzi za vita baridi, Marekani na washirika wake waliwapa mafunzo na silaha makundi ya vijana wa Itikadi kali waliojulikana kama "MUJAHEDEEN" kwa lengo la kuzikomboa nchi ambazo zilikua na mkono wa Urusi ndani yake kama Afghanstan, Uzbek na zinginezo ili kuudhoofisha utawala wa Kisovieti. Na lengo hilo lilifanikiwa. Lakini ndio kikawa chanzo cha makundi hatari kama Taleban. Kwahiyo Ubepari wa Marekani na washirika wake ndio chanzo cha Ugaidi. Kuna sababu nyingine ya Ugaidi ambayo ni kuanzishwa kwa taifa la Israel.
Moto unawaka kila pande, tukianzia Syria ambapo Marekani amekua akidhamini makundi ya waasi wa itikadi kali ili wamtoe raisi Assad, mgogoro ambao umezaa kundi la ISIS ambalo kiongozi wake Abubakar Al Baghdad alitolewa Guantanamo kwa makusudi na kupokea mafunzo ya mwaka mmoja nchini Jordan chini ya CIA na MOSSAD ili kuanzisha kundi hilo ambalo litang'oa tawala za kishia zilizo Iraq na Syria ili kumdhoofisha Iran. Afghan na Pakistan nako alama ya Taleban kundi ambalo chimbuko lake ni MUJAHEDEEN wakati wa vita baridi kama tulivyoona hapo juu. Yemen ambapo mshirika wake Saudi Arabia anaendelea kuua raia wasio na hatia. Libya, nchi ambayo imegawanyika ina serikali tatu sasa hivi, kila kundi limeteka bandari yake na linauza mafuta, Somalia na Nigeria ndo kama tunavyoziona.
Mpaka sasa dunia imekua haikaliki, maeneo hapo juu ndiyo yanayoathirika zaidi. Na hali ya kibinadamu imekua na mashaka makubwa. Waathirika wakubwa wa vurugu hizi ni wakina mama na watoto na kumekua na ongezeko kubwa la wakimbizi kuelekea Ulaya, hasa nchi za Scandinavia na Ujerumani. Huku Marekani akinufaika na kunyonya mafuta tu.
Binafsi naliona hili ni tatizo. Tatizo ambalo linasababisha madhara makubwa kwa watu ambao hawana hatia na hawajui nini kinaendelea. Marekani amekua tishio juu ya amani ya dunia, na yupo nyuma ya kila kitu kibaya kinachohatarisha maisha ya binadamu.
Tatizo ambalo ni kama zimwi lenye madhara lililofunguliwa na wamagharibi wakati wakiwa kwenye harakati zao za unyonyaji, wame- "unleash the dragon"....