Al Jazeera yaanika 'Nyaraka za Palestina' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Al Jazeera yaanika 'Nyaraka za Palestina'

Discussion in 'International Forum' started by Mohammed Shossi, Jan 25, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Al Jazeera yaanika 'Nyaraka za Palestina'  [​IMG]Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas

  Al Jazeera imetangaza na kuchapisha inachokiita 'Nyaraka za Palestina', zinazofichua mlolongo wa mambo muhimu na magumu ambayo wajumbe wa upatanishi wa Kipalestina wamekuwa wakiyaridhia katika mazungumzo yao na Israel.

  Baada ya WikiLeaks, sasa ni hiki kinaweza kuitwa 'JazeeraLeaks.' Jana usiku (23 Januari 2011) kituo cha televisheni cha Al Jazeera, likitangaza rasmi uwekwaji hadharani wa karibuni nyaraka 17,000 ambazo kituo hicho kinasema kwamba, zimetoka katika vyanzo vya uhakika.
  Nyaraka hizi zinatoa siri ya kile kilichokuwa kikizungumzwa ndani ya kuta nne, baina ya wajumbe wa upatanishi wa Kipalestina, wa Kiisraeli na wa Kimarekani; kubwa zaidi ikiwa ni wajumbe wa Kipalestina, wakiongozwa na Saeeb Erakat, kukubali kuyatoa au kuyahalalisha maeneo nyeti sana ya ardhi ya Palestina kwa Israel, kama vile eneo zima la Jerusalem ya Mashariki, ukiacha sehemu ndogo tu iitwayo Jabal Abu Ghneim.
  Mtangazaji wa Al Jazeera, Adrian Finnegan, anasema haijawahi kutokea kwenye historia ya mgogoro wa Mashariki ya Kati, kiwango kikubwa cha siri za ndani kama hiki kuwekwa hadharani.
  "Nyaraka za Palsetina zina taarifa nyingi zaidi kuweza kupenya katika historia ya mgogoro wa Israel na Palestina." Anasema Finnegan.
  [​IMG]Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Kijana wa Kipalestina akifanya shughuli za ujenzi katika makaazi ya walowezi ya Kiyahudi kwenye Ukingo wa MagharibiUtangazaji na uchapishwaji wa nyaraka hizi, ambazo tayari zimeanza kuwekwa kwenye mtadao wa Al-Jazeera tangu jana usiku, una athari kubwa sana kwa heshima ya viongozi wa chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO).
  Viongozi wa kundi la Fatah, kama Rais Mahmoud Abbas, ambalo ni sehemu ya PLO na ndilo linaloongoza Mamlaka ya Ndani ya Palestina, wamekuwa kila siku wakijidhihirisha kama watetezi wakubwa na wa pekee wa ardhi ya Palestina, kwa gharama ya kuyatenga makundi mengine kama vile Hamas.
  Tayari maafisa wa mamlaka hiyo wameuhoji uhalali wa nyaraka hizi wakisema kwamba ni za uongo na au zinasema nusu ukweli. Katika mahojiano na gazeti la kila siku la al-Ayyaam la nchini Misri hii leo, Saeeb Erakat alisema kwamba utolewaji wa taarifa kama hizi na katika wakati kama huu ni njama ya makusudi ya kuwaharibia viongozi wa Kipalestina taswira yao kwa jamii.
  Miongoni mwa yale yaliyomo kwenye nyaraka hizi, ni dondoo za video za kikao cha tarehe 15 Juni 2008 kati ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani , Condoleezza Rice, waziri wa Mambo ya Nje na mjumbe wa Israel katika mazungumzo hayo, Tzipi Livni, waziri mkuu wa zamani wa Palestina, Ahmed Qureia na mkuu wa wajumbe wa upatanishi wa Palestina, Saeeb Erakat, ambapo Qureia anaonekana akipendekea utanuliwaji wa makazi ya walowezi wa Kiyahudi katika eneo lote la Jerusalem ya Mashariki.
  Lakini kwa mujibu wa nyaraka hizo, ni Erakat ndiye aliyekwenda umbali wa kutaja orodha ya maeneo ambayo Mamlaka ya Palestina ilikuwa tayari kuyatoa sadaka, yakiwemo ya Ramat Alon, Ramat Shlomo, Gilo na Talpiot.
  Mwandishi wa gazeti la The Guardian la Uingereza, ambalo nalo limeanza kuzichapisha nyaraka hizo, Seumas Milne, anasema kwamba nyaraka hizi zinaonesha sura halisi ya wajumbe wa Kipalestina wanapokuwa kwenye meza za majadiliano, ikiwa na tafauti sana na kile wanachokionesha wakiwa kwenye majukwaa ya kisiasa:
  "Nyaraka hizi zinaonesha pia picha ya udhaifu na fadhaa kwa upande wa Palestina katika mazungumzo ya upatanishi, kwamba hawajapiga hatua yoyote ile." Anasema Milne.
  Mwandishi: Mohammed Khelef/DPAE
  Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
   
 2. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Al Jazeera yaikasirisha Palestina  [​IMG]Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Spika wa Bunge la Palestina, Abdel-Aziz Dweik

  Nyaraka za siri kwenye mazungumzo ya kutafuta amani kati ya viongozi wa Palestina, Israel na Marekani, zilizoanza kuchapishwa jana na kituo cha Al-Jazeera, zimeanza kuwagawa Wapalestina na kuzusha hasira miongoni mwao.

  Inawezekana, ikawa hii si mara ya kwanza kwa taarifa za siri za utawala wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuwekwa hadharani, lakini ni mara ya kwanza kwa kiwango kikubwa kama hiki cha taarifa kutangazwa kwa pamoja na kwa wakati mmoja.
  Tayari viongozi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina wanakishutumu kituo cha Al Jazeera kwamba kina ajenda ya siri ya kuichafua taswira yao, kwa kile wanachokiita 'kutangaza uongo na nusu ukweli'. Rais wa Mamlaka hayo, Mahmoud Abbas ameziita nyaraka hizi ni upuuzi mtupu, ambao unakusudia kuwachangaya watu.
  "Sisi hatuna siri yoyote ambayo jamii za Kiarabu hauijui." Amesema Abbas.
  [​IMG]Bildunterschrift: Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina akikagua sehemu za ulinzi za mamlaka yakeMapema, kiongozi wa ujumbe wa wapatanishi wa Palestina katika mazungumzo yake na Israel, Saeeb Erakat, alikana kabisa kutoa tamko lolote ambalo linamaanisha kuyatoa sadaka kwa Waisraeli, maeneo ambayo Palestina imezingatia kwamba ni yake kwa muda mrefu, likiwemo la Jerusalem ya Mashariki.
  "Nataka kuuambia ulimwengu kwamba mimi sina kitu cha kuficha. Mara kadhaa nimesema kuwa Mamlaka ya Palestina kamwe haitotoa eneo lolote lile ambalo ni haki yetu. Ikiwa tuliwapa Waisraeli hiyo wanayoiita Al Jazeera kama Jerusalem kubwa kabisa, kwa nini basi Israel haikusaini mkataba wa makubaliano?" Amesema Erakat.
  Lakini si kila mtu anaamini kwamba Erakat na wenzake katika Mamlaka ya Ndani ya Palestina hawakutoa mapendekezo ya kuihalalishia au kuipa Israel maeneo mengi zaidi ya ardhi yao. Abed Dandis, muuza duka wa Kipalestina katika sehemu ya mji mkongwe ya Jerusalem, aliliambia Shirika la Habari la AFP, kwamba viongozi wao wamekuwa kila siku wanalaza shingo zaidi wanapokuwa mbele ya Israel.
  "Kilichowekwa hadharani na Al-Jazeera si kipya. Tumekuwa tukijuwa muda mrefu. Unaweza kufahamu kwamba katika makubaliano, lazima ukubali kutoa baadhi ya mambo ili kupata kitu fulani, lakini sisi Wapalestina tunatoa tu bila ya kupokea chochote." Amesema Dandis.
  Kwa mujibu wa waziri wa zamani ya mambo ya nje wa Israel, Shlomo Ben-Ami, anasema kwamba kile kinachosemwa kuwa ni sadaka ambayo Erakat na wenzake walikubali kuipa Israel, ilikubalika hivyo tangu wakati wa kiongozi wa Palestina, Marehemu Yasser Arafat.
  "Mapendekezo haya ni kama yale ambayo Wapalestina walikubaliana nayo katika Camp David, kupitia upatanishi wa Bill Clinton na ugawaji wa mji wa Jerusalem kwa kutegemea misingi ya kidini, yaani sio kuwa na Jerusalem ya Mashariki na ya Magharibi, bali kusema kuwa kila cha Kiyahudi ni cha Israel na kila cha Kiarabu ni cha Palestina." Ben-Ami amekiambia kituo cha habari cha Al-Jazeera.
  Wakati huo huo, taarifa zinasema kwamba wakaazi wa mji wa Ramallah katika eneo la Gaza wameanza kufanya maandamano ya kuupiga utawala wa ndani ya Palestina kutokana na taarifa zilizoibuliwa na Al-Jazeera.
  Mwandishi: Mohammed Khelef/AFP/Reuters
  Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
   
 3. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wasipoangalia tutakuja sikia Palestine yote imechukuliwa na Israel
   
 4. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Na ndio utakuwa mwisho wa dunia...........
   
 5. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mohammed Shossi

  Mwisho wa Dunia ni pale wewe Utakavyokufa, ww utakufa utaacha Dunia kama ilivyo na wengine wakiifaidi na wapo wanaozaliwa .........Mzunguko unaendelea hivyo2
   
 6. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Alaaaaaaa
   
 7. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Navyoona, endapo makundi yanayozozania madaraka ndani ya Palestina wakitaka kuiondoa serikali ya PLO ya Abu Masen, yaani mzee anayeongoza Palestina, Mahmood Abbas, ghasia za wenyewe kwa wenyewe ni dhahiri kwani jamaa hawa wa Hamas wameshapata kisingizio cha kuiondoa serikali ya sasa.

  ngoma itakavyodunda, wenyewe kwa wenyewe, lazima Israel itie mkono kulinda na hiyo ndo Intifada nyingine itaanza.

  kwa hapo moto mwingine utaowaka, lazima Wapalestina wakimbilie walikokuwa awali, yaani 'ukimbizini' ktk mierezi ya Lebanon!
   
 8. l

  limited JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hivi kuna siku israel na palestina watakaa kwa amani?
   
 9. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nadhani watawala wanaweza kukubaliana kuigawa palestina lakini watawaliwa wasikubali wakafanya sabotage na amani isismame.
   
Loading...