Akishitaki atakuwa kamkosea mumewe?

Akishitaki atakuwa kamkosea mumewe?

Mkunde Original

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2013
Posts
807
Reaction score
647
Habari zenu wandugu,

Mawazo na michango yenu inahitajika kunusuru hii familia.
Ni familia ya mume mke na watoto 5, watoto 3 wako sekondari shule za bweni na wawili ndo wako shule ya msingi wanakaa nyumbani na wazazi wao.

Hii familia kwa miaka 3 mfululizo wamekuwa kwenye changamoto mbalimbali kiasi kwamba wote baba na mama kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitamani kuachana ila kigezo cha watoto ndo huwa kinakuwa zuio.
Changamoto imeongezeka baada ya utawala mpya kuingia madarakani mume au baba mwenye nyumba alitumbuliwa na mheshimiwa na hadi sasa yuko benchi tuu. Tangu huyo baba atumbuliwe amekuwa kero kwenye familia yake. Mwezi mmoja wa kwanza baada ya kutumbuliwa alikuwa anashinda nyumbani asubuhi hadi asubuhi nyingine, yaani alikuwa baba wa nyumbani na akajikuta anakuwa karibu na housegirl matokeo yake kuanza mahusiano na wadada wa kazi. Aibu hii mkewe aliigundua maana wadada walionesha mabafiliko kuna walioonesha jeuri na kiburi na kuna walioaga kuacha kazi gafla maana si waschana wote wanakubali kuwa na mahusiano na baba mwenye nyumba. Hivyo hilo limefanya mke kuwa na kero ya kubadili waschana wa kazi kila leo kama mjuavyo si rahisi kupata waschana wa kazi waweza kaa miezi 3 hadi 4 ukiwa unatafuta bila kupata.

Mke akiongea hii kero na mumewe mume akaona abadili muelekeo na kuanzia hapo akaanza asubuhi mke akijiandaa kwenda kazini na watoto shule yule baba mwenye nyumba anajiandaa nae anatoka. Anakoenda haijulikani basi ya miezi kadhaa mke akagundua kumbe huwa anaenda baa muda wa asubuhi atakula na kunywa maji hadi mchana akihama baa moja kwenda ingine na pale pombe zinaporuhusiwa kuanza kuuzwa basi huzifakamia utasema kuambiwa zinaongeza nguvu za kiume. Anarudi nyumbani akiwa njwii hajitambui anarudishwa na bodaboda hana hata kumi....

Amekuwa akitumia akiba yake kufanya huo ulevi na sasa amekuwa mlevi wa kupindukia. Mke ameshamshauri mara kadhaa aache kufanya hivyo maana hakubadilishi au kumpunguzia msongo wa mawazo alionao badala yake amekuwa mkali kwa mke na watoto. Mke anaona uvumilivu unamshinda maana kila siku afadhali ya jana. Mbali ya hapo bwana mume amekuwa akishusha kipondo kila arudipo amelewa na hapo kuna siku anarudi ananukia marashi ya kike siku ingine shati zina alama za rangi ya mdomo na foundation.... mke anafua tuu.... Kweli jamani na hii avumilie. .... magonjwa je?

Nyie mwaonaje maana hii familia naifahamu na huyu mama huwa tunaongea sana. Sijamshauri cha kufanya nimekuwa nikimpa pole tuu ila ninakoelekea nahisi ntamwambia aachanena mumewe maana huko si kuvumiliana kwa shida na raha khaa.

Kusema ukweli hata mie ndoa yangu ina misukosuko ila si kama ya huyu mama. Na yangu ingekuwa kama ya huyu wallah ningeachika tangu juzi.

Nyie mnashaurije?
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Mmhhh!!ndoa zina changamoto sana!

Watoto watano ni wengi sana!

Muambie avumulie tu maana muda alioishi nae kwenye raha ni mwingi kuliko shida za anazopata sasa hivi!

Tatizo wafanyakazi wengi wa serikali wanabweteka sana biashara hatuwezi ndo maan tukipatwa na matatizo kazini tunakosa muelekeo
 
Amshauri mumewe watafute plan b ili apate cha kumuweka busy na kujipatia kipato pia.
 
Matokeo yoyote ya kuachana sa hv itaonekana kwa sababu mzee katumbuliwa
Atafute njia mbalimbali za usuluhish kwa maana ya wazaz na watu wanaowaheshimu kama. Kutakua hakuna mabadiliko yoyote kutokana na Hayo anaweza kwenda mbele zaid..
Kwa maana kama Ulivyosema changamoto zlianza kabla ya hajatumbuliwa na alivumilia bas asje akaonekana amekimbia kwa. Sababu mzee yuko benchi
 
Siwezi hata kushauri kitu ila binadamu tumejua kuumizana sana.... Mbaya zaidi kuna machaguo tuliyoyafanya kwenye maisha yetu huko nyuma sasa hivi yanatuumiza sana na kutugharimu furaha zetu na maisha yetu.

Mpe pole, sina cha kushauri.
 
Na hili ndo amekuwa akiniambia mara kwa mara, anajua watu wengi watasema anaachana kwasababu mumewe hana kazi ila akifikiria mateso anayopata hana hamu na ndoa.

Asante kwa wazo lako ntamshauri
 
Siwezi hata kushauri kitu ila binadamu tumejua kuumizana sana.... Mbaya zaidi kuna machaguo tuliyoyafanya kwenye maisha yetu huko nyuma sasa hivi yanatuumiza sana na kutugharimu furaha zetu na maisha yetu.

Mpe pole, sina cha kushauri.

Haya ntampa pole zako
 
Amshauri mumewe watafute plan b ili apate cha kumuweka busy na kujipatia kipato pia.

Yeah hili nalo ni wazo zuri, japo mumewe alikuwa ni wale wanaume wenye kutumia muda wao mwingi kazini hakuwa hata na kiduka au genge la kumuingizia shilingi.
Ntaufikisha huu ushauri
 
Mmhhh!!ndoa zina changamoto sana!

Watoto watano ni wengi sana!

Muambie avumulie tu maana muda alioishi nae kwenye raha ni mwingi kuliko shida za anazopata sasa hivi!

Tatizo wafanyakazi wengi wa serikali wanabweteka sana biashara hatuwezi ndo maan tukipatwa na matatizo kazini tunakosa muelekeo

Nani amekudanganya Ndoa ni kuvumiliana?

Mwambie mke apige chini huyo bwana

akili ikiwa sawa watarudiana tu
 
Ndo hicho saa hizi na msongo wa mawazo mumewe ataweza fanya hiyo biashara kweli...?
 
Nani amekudanganya Ndoa ni kuvumiliana?

Mwambie mke apige chini huyo bwana

akili ikiwa sawa watarudiana tu

Not easier as u think it is...!!
Muda walioshi vizuri ni mwingi kuliko kipindi hiki!
Huyo mume anahtaji faraja haswa baada ya kuachishwa kazi!
Mwanamke anatakiw awe nae karibu mno mmewe...

Kumuacha sio solution zaidi atakua amekosea sana tu!
 
Yeah hili nalo ni wazo zuri, japo mumewe alikuwa ni wale wanaume wenye kutumia muda wao mwingi kazini hakuwa hata na kiduka au genge la kumuingizia shilingi.
Ntaufikisha huu ushauri
Itabidi tu alazimike angalau kujifunza kile atakachoona anaweza kukifanya kwa urahisi vinginevyo hiyo ndoa inaning'inia kwenye kuti kavu!!
 
Not easier as u think it is...!!
Muda walioshi vizuri kuliko kipindi hiki!
Huyo mume anahtaji faraja haswa baada ya kuachishwa kazi!
Mwanamke anatakiw awe nae karibu mno mmewe...

Kumuacha sio solution zaidi atakua amekosea sana tu!

Shemeji unaakili sana wewe
 
Back
Top Bottom