Huyo jamaa yako alijitakia mwenyewe ... kwanza inaonyesha mke mdogo alikaa Bongo kwa muda mrefu akiwa peke yake. Pili inawezekana huyo jamaa alijisahau (kimawasiliano) kwa kuwa alikuwa na mke mkubwa, so hana upweke na wala hawezi kum-miss sana mke mdogo.
Dunia ya leo unaoa mitala halafu mke mdogo damu bado inachemka anataka shughuli muda wote, unamuacha akae peke yake miezi 6 au zaidi, na anajua wazi kwamba huko uliko wewe unapata huduma kama kawaida, kwanini ajitese kukusubiri? Wakija vijana wasiotaka makubwa anajirusha na matokeo yake ndiyo hayo. Hakuna mwanamke wa siku hizi ambaye yuko tayari kusubiri huduma ya ndoa ya mgao, likizo mpaka likizo, na likizo yenyewe mara moja kwa mwaka. Why starve? While your husband is having some with bi mkubwa?
Jamani hayo maisha waliishi wazee wetu na zama hizo ngono haikuwa starehe ilikuwa inatumika kwa ajili ya uzazi. Siku hizi ngono ni starehe na ndio maana manjonjo kibao ili kukoleza shughuli yenyewe.
Mwanamke gani wa leo ambaye atakaa kusubiri mume aje kumuona once in a yr na aachwe na mimba?
Ukishaoa mitala na kama kuna distance kubwa kutoka kwa mke mmoja kwenda kwa mwingine, basi uwe tayari kuibiwa. Unadhani kwanini wazee wa zamani walikuwa wanasema kwamba, "Kitanda hakizai haramu"? Kwa kuwa walikuwa wanajua kuna kuibiwa, na hasa kama mke kaachwa miezi 6 au mwaka mzima peke yake, ukikuta mkeo ni mjamzito wala hutakiwi kuuliza mimba ni ya nani? Bali ni kuwajibika kuitunza mpaka na mtoto.
Jamaa yako alitakiwa aoe na kuondoka na mke wake mara baada ya ndoa au asichukue zaidi ya miezi 6 ku-process maswala ya uhamiaji. Sasa jamaa kaacha mke mdogo peke yake, alitegemea nani amliwaze? Halafu mke mdogo aki-cheat wala haimuumi sana kwa kuwa anajua na mume wake anapata huduma kila siku.
Huyo jamaa kukaa kwake UK hakujamkomboa, maana naona anaishi maisha ya kijima, hata kama dini inakuruhusu, unatakiwa kutumia akili na kujiuliza kwa mazingira ya dunia ya leo unaweza kuacha mke mdogo miezi 6 au mwaka? Kama ni mke pekee inawezekana, ila siku akigundua kwamba una-cheat huko uliko na yeye ataanza kujirusha. Kwa mke wa mitala, hasubiri kugundua maana ana uhakika kwamba unapata huduma kwa mke mkubwa, so na yeye ataenda kusaka huduma kwa "mume mdogo".