Akikutongoza kwa njia ya kuchat WhatsApp utafanyaje?

Mke wangu mtarajiwa ni single mother,ana mtoto mmoja,kwetu ni mkoani Tabora ila wote tunaishi Sumbawanga pamoja na huyo baba wa mtoto wa mtarajiwa wangu,wiki tatu zilizopita mchumba wangu alikuwa na safari ya kwenda nyumbani Tabora,alimuagamzazi mwenzake akaja akaniaga na Mimi pia,nilichokifanya kabla hajaondoka nikafuta namba ya mzazi mwenzake nikasave namba nyingine kwa jina lilelile la Baba Mariam ,akiwa njiani kulelekea huko aendako nikaanza kuchat naye whatsApp kwa namba ileile ya baba Mariam feki ,nikajieleza mengi kwake nikimtaka turudiane,akaniuliza Kama nataka kuzaa burudani tu au kumuoa?nikamjibu nataka tuzae mtoto wa pili na wa tatu,mambo mengine yatafuata,huku na kule mke mtarajiwa akawa anaona aibu kukubali haraka haraka akawa anapiga chenga fupifupi za matumaini,Mimi nakakaza Uzi kwelikweli mtarajiwa akalainika ila akawa mzito sana kutamka kuwa amekubali,Mara anitumie picha za jamaa mara za mtoto wao mara za mtoto wa mzazi mwenzake(ana mke)hapo bado hajakubali,hatimaye akanipigia video call Mimi sikupokea,nikamtumia ujumbe samahani siwezi kupokea mazingira hayaruhusu,naye akajibu usiku mwema,nikamwambia usiage kabla hatujafikia muafaka ,natoka nje ili nikupigie audio call maana hata nikipiga video call hutaniona nje ni giza, akasema poa,nikatoka nje nikampigia audio akaitambua sauti yangu,nikamwambia nashukuru najua angekuwa yeye mzazi mwenzako tayari ulishakubali kurudiana naye ndio maana ulipiga video call ulitaka upate uhakika kwanza Kama ni yeye au la ndipo ukubali,akaanza hooo Mimi nilipiga video call kwa bahati mbaya wala sikutaka kukuona,nikamuuliza je nilipokwambia natoka nje nikupigie kwanini hukuniambia nisitoke umepiga bahati mbaya?je ungekuwa wewe mwanaJF ungeendelea kuwa na imani tena na mtu Kama huyu? Je utetezi wake unatosha?
Hapo alishakula kiapo kuwa kamwe hawezi kurudiana naye hata iweje,na akienda tofauti na kiapo chake Mungu ampe adhabu yoyote hata kifo ikiwezekana,Sasa nikawa nimesikiasikia fununu kwamba jamaa hamtaki kabisa mwanamke ila mwanamke bado anamtaka mwanaume,ndipo nikaona nitumie mbinu mbadala ili kuujua ukweli.
pumba sizani kama kuna easy ulishawahi ata kupata 5/20
 
Umemuonea
 
Kuolewa au kuoa mtu mwenye mtoto ni sawasawa na kununua shamba lenye mgogoro.
 
huelewi nini kuhusu single mother labda nikueleweshe?
 
Ha ha ha.
Kwa nini uoe mke wa mtu?
Kila mtu aoe au kuolewa na aliyezaa naye!!
Ukizaa nao kumi oa wote.!!
Mambo ya kuzalisha na kuacha mnasababisha wanaume wengine wanateseka.!!
Sio mke wake alizaa naye tu,na si unajua kupenda ni upofu
 
Mara nyingi uandishi katika chati huwa tofauti baina ya mtu na mtu,huyo mpenzi wako alishindwa kweli kubaini uandishi wa ex wake uko tofauti na alivyouzoea?
Kwakuwa nina namba ya mzazi mwenzake nilichukua hata picha aliyoweka profile nikaiweka kwangu kwenye namba feki,na nilijitahidi sana kubadilisha uandishi na hata baadhi ya maneno,ila baadae alipohisi tofauti ndipo akapiga video call
 
Wewe umeamuaje?
Just jua huyo mwanamke anampenda baby daddy wake bado yupo na wewe kaa kuwa unampenda au la alishakugundua akataka akukomeshe
Ni kweli,ila naamini hakujua ndio maana alitaka anipigie video call ili ajiridhishe,na karopoka mengi ambayo mimi sikuyajua ambayo naamini angejua Ni Mimi asingefanya hivyo
 
Wanawake wamejaa hivi ukang'ang'ane na mke wa mtu? Single mother ni mke wa baba wa mtoyo wake by default, wewe hata ufanyeje jamaa ataendelea kumla wakati wowote akijisikia. Baba mtoto kumla mama mtoto ni sawa na 22/7.

Ushauri wa bure, oa single mother ikiwa tu una uhakika baba wa mtoto amekufa. Ila hata kama ameugua ukichaa bado akitaka kumla mama mtoto wake ni sawa na kunywa joice, ni fasta tu
Nimekupata mkuu nashukuru kwa ushauri
 
Brother naomba nikukumbushe kwamba siku zote kwa watu waliozaa pamoja,mwanaume ndio mwenye maamuzi ya either mahusiano yaendelee ama yakome. Maana yake ni kwamba mzazi mwenzake akiamua kumkazia hata ufanye nini atamla tu
 
Wanawake bana. Aisee wanawake dah ila mkuu huwezi juwa .usukute alishagundua kabra kama alikuwa anachati na wewe maana chati za watu zile styles huwa hazifanani. Kwahiyo alikuwa anakuchora tu na mawivu yako.
Hapana mkuu hakugundua ndio maana alijiachia Sana,akaja kushtuka mwishoni akaamua kupiga video call
 
Huko kupima kwenu km mtu anakupenda ndo kunawacost
 
Siku ikitokea baba wa mtoto wake akahitaji kweli kurudiana nae,wewe unaachwa mara moja

Kama ningekuwa ni mimi ningeachana nae,huyo mwanamke bado ana uhitaji mkubwa wa kurudiana na mume/baba wa mtoto wake....shukuru sana umegundua haya mapema

Tuliza akili,utapata atakayekufaa zaidi

Pole sana mkuu
Nashukuru sana kwa ushauri
 
Back
Top Bottom