Jabakeke
JF-Expert Member
- Apr 18, 2019
- 386
- 362
Mke wangu mtarajiwa ni single mother,ana mtoto mmoja,kwetu ni mkoani Tabora ila wote tunaishi Sumbawanga pamoja na huyo baba wa mtoto wa mtarajiwa wangu,wiki tatu zilizopita mchumba wangu alikuwa na safari ya kwenda nyumbani Tabora,alimuagamzazi mwenzake akaja akaniaga na Mimi pia,nilichokifanya kabla hajaondoka nikafuta namba ya mzazi mwenzake nikasave namba nyingine kwa jina lilelile la Baba Mariam ,akiwa njiani kulelekea huko aendako nikaanza kuchat naye whatsApp kwa namba ileile ya baba Mariam feki ,nikajieleza mengi kwake nikimtaka turudiane,akaniuliza Kama nataka kuzaa burudani tu au kumuoa?nikamjibu nataka tuzae mtoto wa pili na wa tatu,mambo mengine yatafuata,huku na kule mke mtarajiwa akawa anaona aibu kukubali haraka haraka akawa anapiga chenga fupifupi za matumaini,Mimi nakakaza Uzi kwelikweli mtarajiwa akalainika ila akawa mzito sana kutamka kuwa amekubali,Mara anitumie picha za jamaa mara za mtoto wao mara za mtoto wa mzazi mwenzake(ana mke)hapo bado hajakubali,hatimaye akanipigia video call Mimi sikupokea,nikamtumia ujumbe samahani siwezi kupokea mazingira hayaruhusu,naye akajibu usiku mwema,nikamwambia usiage kabla hatujafikia muafaka ,natoka nje ili nikupigie audio call maana hata nikipiga video call hutaniona nje ni giza, akasema poa,nikatoka nje nikampigia audio akaitambua sauti yangu,nikamwambia nashukuru najua angekuwa yeye mzazi mwenzako tayari ulishakubali kurudiana naye ndio maana ulipiga video call ulitaka upate uhakika kwanza Kama ni yeye au la ndipo ukubali,akaanza hooo Mimi nilipiga video call kwa bahati mbaya wala sikutaka kukuona,nikamuuliza je nilipokwambia natoka nje nikupigie kwanini hukuniambia nisitoke umepiga bahati mbaya?je ungekuwa wewe mwanaJF ungeendelea kuwa na imani tena na mtu Kama huyu? Je utetezi wake unatosha?
Hapo alishakula kiapo kuwa kamwe hawezi kurudiana naye hata iweje,na akienda tofauti na kiapo chake Mungu ampe adhabu yoyote hata kifo ikiwezekana,Sasa nikawa nimesikiasikia fununu kwamba jamaa hamtaki kabisa mwanamke ila mwanamke bado anamtaka mwanaume,ndipo nikaona nitumie mbinu mbadala ili kuujua ukweli.
Hapo alishakula kiapo kuwa kamwe hawezi kurudiana naye hata iweje,na akienda tofauti na kiapo chake Mungu ampe adhabu yoyote hata kifo ikiwezekana,Sasa nikawa nimesikiasikia fununu kwamba jamaa hamtaki kabisa mwanamke ila mwanamke bado anamtaka mwanaume,ndipo nikaona nitumie mbinu mbadala ili kuujua ukweli.