Akhaa babu ukubwa kitu gani?...

Akhaa babu ukubwa kitu gani?...

Mahondaw

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
71,993
Reaction score
177,229
Habari wana JF.

Juzi kati kuna kazi nilipata katika shirika Fulani hivi sasa songombingo ikawa siku ya kuhamia hapo kwenye chumba nilichotaftiwa na shirika.

Tulifika hapo kama mida ya saa 12.00 jioni nikapokelewa vizuri wenyeji wakapika tukala kwa pamoja.

Tulipomaliza kula mkaka mmoja akaaga kuwa anaenda kuangalia mpira akaondoka zake.

Tukabaki mimi na mkaka mwingine wa hapohapo kwenye hiyo nyumba.

Tukapiga stori za hapa na pale wee mpaka nilipohisi usingizi, basi nikamuaga huyo kaka kuwa mimi naenda zangu kulala, lol!!! kumwambia hivo tu akanyanyuka na kwenda kufunga milango yoote ya nyumba akarudi na kuniambia "usilale humo kwako" Nikamuuliza "ati unasemajee??!!" akajibu "hakuna kulala humo ndani kwako" nikamuuliza nikalale wapi?" kulee" huku akioneshea chumbani kwake.

Mimi nikachukulia utani tu nikatoka sebuleni kuelekea room kuandaa vizuri ili nilale. khaaa!!! nikashangaa mtu kazima taa zote za nyumba kuanzia sebuleni nje na kwingineko akaja nilipokuwa naandaa chumba changu ili nilale.

Nikamuuliza kulikoni mbona umezima taa? akajibu siriazi huwezi lala humu wewe ni mgeni hiki chumba ni kichafu sana.

Nikamwambia huoni kama ndio nakiandaa mimi nalala zangu humu nilipooneshwa (huku naendelea kufagia).

Akasema tunalala kwangu mimi nalala hukuu wewe kulee (ila kitanda kimoja)usijari wala hakutatokea chochote kwani hujaishi maisha ya chuo banah unajifanya kama mtoto aargh(akiniambia).

Mhh nikaanza kuogopa kwani tulibaki wawili tu na mimi ni mgeni sijui a wala z nikamwambia siwezi lala chumba kimoja nawewe from nowhere eti kisa ni mgeni na mimi sina mahusiano na wewe.

Uwiii akazima na taa ya chumbani kwangu mimi nikawasha akaizima tena nikaiwasha akaizima nikawasha nikapanic na kuanza kuongea kwa sauti ya juu na hasira naomba utoke chumbani kwangu akang'ang'ania akiniambia usiwashe taa banah kule nje wataniona si unaona hapo dirishani hakuna pazia na ni usiku halafu usiongee kwa sauti kubwa watasikia.

Mhh binti nikazidi kuogopa kwani milango yote amefunga na taa za sebuleni na nje amezima.

Alivoona simsikilizi niko bize kufanya usafi, akasema inamaana hujaelewa nilichokwambia ama? nikamjibu hapana nashukuru kwa msaada wako ila siwezi lala kwako.

Nikaendelea na ubize khaa!!! kutahamaki mkaka huyu hapa kanishika mkono ananivutia chumbani kwake, hapohapo miguu pamoja na joints zake vikaishiwa nguvu vimelegea nikakaa chini.

Thanks God wakati nimeishiwa nguvu na nikihema kwa supersonic speed, mdogo wangu akanipigia simu sasa yule kaka alikuwa ameweka mziki sauti kubwaa nikamwambia naomba nifungulie mlango nikaongelee nje humu sitasikia, akafungua mlango nikajikongoja mpaka nje nikamwambia dogo akate kwanza simu nitampigia, akakata.

Palepale nikampigia mratibu kwanza ile amepokea simu tu na mimi kusema hallo.. Mratibu akaitikia mbona sauti yako kama unalia nini kimetokea? Nikamweleza kila kitu.

Kwakuwa mratibu anaishi mbali akampigia Project Facilitator( sijui kiswahil wanamwitaje) na huyo PF akampitia mkaka alieenda kucheki mechi walichoongea mi sijui nikaona watu wanakuja na pikipiki usiku huo mimi nilikua nmekaa zangu nje japo mimi ni muoga ila niliogopa kurudi ndani.

PF akasovu tatizo nikahamishwa kwingine ili nikalale japo muda ulikua umeenda ila sikulala usiku mzima mpaka asubuh kulivokucha.

Sasa huyo mkaka ananilaumu sana eti hakuona kosa na hajaona sababu ya kumripoti kwa mratibu sababu alikua ananisaidia so nimemuweka hatarini na eti kama sikupenda ningemwambia tu angenielewa.

Namimi nikamuuliza ulitaka nikweleze au nikatae kwa lugha gani labda ambayo ungeielewa? Akhaa babuuu mi mkubwa ndio ila mmhhh hapana kwakweli.... JE MWANA JF UNGEKUA WEWE UNGEFANYEJE?

Toa maoni yako kupitia........
 
Pole mkuu...una bahati maana ungegegedwa ucku kucha...ndio mitihani lkn inatufunza kila cku.
 
mmmmmhhhh! siku ya kwanza kukutana tena bila "theme" ya "i love u, i lov u 2" then analazimisha kugemua?
 
Dah jamaa alifikiri we maharage ya Mbeya, pole hope atakuwa kajifunza kitu.
 
Huyo jama ni mbakaji amezoea vya kunyongewa
Sasa kipindi anakusukumizia kwake statu ya "zeep" yake ilikuaje?ilikua imetuna/vimba(mlima)?
 
Huyo jama ni mbakaji amezoea vya kunyongewa
Sasa kipindi anakusukumizia kwake statu ya "zeep" yake ilikuaje?ilikua imetuna/vimba(mlima)?

kwani nilitamani hata kuiangalia!!!!!
usser
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom