Akaunti za benki za Kanisa la Askofu Gwajima zadaiwa kufungwa

Akaunti za benki za Kanisa la Askofu Gwajima zadaiwa kufungwa

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
20,725
Reaction score
31,305
Hakika kuna jambo Gwajima alikuwa analipanga. Alikuwa anajikosha kujifanya nini sijui, kipindi cha uchaguzi dola inakuwa makini kwa asilimia 1000,000, kama unataka kufadhili magenge ya uhalifu utajulikana tu
==================

"Usiku huo huo majira ya saa tano, kanisa lilivamiwa na magari ya polisi (defenders) likazingirwa, waumini waliokuwa mkesha wa maombi walipigwa, kutolewa nje ya kanisa kwa nguvu bila maelezo na kuwakamata waumini 96, wakiwemo wanawake, wazee na vijana wasio na hatia yoyote zaidi ya kumuomba Mungu wao" - Askofu Mwanamapinduzi

"Makanisa yote 2,112 ya GCTC (Ufufuo na Uzima) yamefungwa nchi nzima. Waumini zaidi ya milioni 6 wamenyimwa haki ya kuabudu. Maaskofu, wachungaji, na wafanyakazi wa kanisa wamepoteza ajira, huduma na wito wa kazi ya Mungu. Akaunti zote za kifedha za kanisa zimefungiwa (frozen) bila kufuta utaratibu wa kisheria" - Askofu Mwanamapinduzi

"Uongozi wa kanisa ulichukua hatua za kisheria kwa kuwasilisha barua ya rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, lakini Waziri alikana barua ile kwa kusema haijasainiwa wala haijatoka kwa Msajili wa Vyama vya Kiraia. Hata hivyo, vyombo vya dola viliendelea kutekeleza amri hiyo ya kufunga makanisa yote ya Ufufuo na Uzima nchini na kuweka ulinzi mkali huku wakizuia mtu yeyote asiingie kwenye makanisa hayo isipokuwa Askari Polisi pake yake" - Askofu Mwanamapinduzi

 
Kama Gwajima alidiriki kuacha fedha kwenye accounts kabla hajafichua watekaji basi hakutumia ujasusi wake vizuri ,hao watu ukiwachokoza lazima wapige block accounts.
Nilisha andika katika hili ,Jasus la mbinguni lazima alishakua mbele ya mda , mtu ana makanisa mpaka nje kwamba ajue analianzisha alafu aache fedha kizembe, mpaka anafika kuliamsha lazima alisha kaa na maaskofu wake na kua na plan B ,so zitakua na pesa kidogo
 
Hata zifunge zitafunguliwa tena kwa fidia juu. 😆😆😆
Nani alipe fidia? Kamuulize Vallambia aliyekuwa mzabuni wa mahitaji ya kivita wakati wa vita ya Kagera, ana hukumu za Mahakama zote, ila hana malipo yoyote. Hukumu ya Mahakama inatakiwa iandikiwe barua kwa Msajili wa Hazina ili aone kama kuna hela Hazina kazi ndio alipe, lini hela zilikosa kazi?
 
Nani alipe fidia? Kamuulize Vallambia aliyekuwa mzabuni wa mahitaji ya kivita wakati wa vita ya Kagera, ana hukumu za Mahakama zote, ila hana malipo yoyote. Hukumu ya Mahakama inatakiwa iandikiwe barua kwa Msajili wa Hazina ili aone kama kuna hela Hazina kazi ndio alipe, lini hela zilikosa kazi?
Utaelewa baadae unaongea mambo mawili tofauti. Mfano wako ni wa hovyo ila.utaelewa baadae sio sasa hivi.
Hasara kwa jamhuri ya Tanzania hasa Tanganyika
 
Back
Top Bottom