Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Twitter imesema kuwa akaunti hiyo kwa jina @realdonaldtrump iliondolewa na mfanyakazi mmoja na baadaye kueleza kuwa ilikuwa siku yake ya mwisho ya kazi.
Akaunti hiyo iliondolewa kwa muda wa dakika 11 na sasa kampuni ya Twitter inachunguza.
Bwana Trump ambaye ni mtumizi wa mtandao wa Twitter wa mara kwa mara akiwa na wafuasi milioni 41. 7 hajatoa tamko lolote kuhusu suala hilo.
Siku ya Alhamisi jioni wale waliotembelea akaunti ya Rais Trump waliona ujumbe uliosoma "pole ukurasa huu hauko kwa sasa"
Baada ya akaunti kurejeshwa ujumbe wa kwanza wa Bwana Trump ulikuwa kuhusu ule mpango wa Republican wa kupunguza kodi.
Hata hivyo POTUS ambayo ndio akaunti rasmi ya Rais Trump haukuathiriwa.
Twitter wamesema kuwa inachunguza tatizo hilo na kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa kisa kama hicho hakitokei tena.
Kampuni hiyo ilisema katika ujumbe wake kwamba wamebaini katika uchunguzi wao kwamba kisa hicho kilifanywa na mfanyakazi anayewahudumia wateja ambaye alifanya hivyo katika siku yake ya mwisho ya kazi.