Naam safari ilikuwa ndefu sana toka alfajiri mpaka mida ya jioni jioni hivi.....
Tukafika pahala tukaamua kuegesha gari ,,,zamani hizo nyumba za wageni zilikuwa chache sana.
Mwana mama akatoa mkeka,akautandika.
Mie nika ambaa ambaa kando kando ya barabara kutafuta kuni.
Nikaweka mafiga na kuchochea moto.
Akiwa anapika mie nipo uvunguni mwa gari juu ya mkeka ninasikiliza Radio...kumi na mbili unusu kwa saa za Afrika Mashariki...Idhaa ya kiswahili toka BBC Bush House LOndon.
Alipomaliza mapishi akaninawisha mikono(wa mama wa zamani walitunawisha kabla na baada).
Baada ya kunawa na kumuona ameridhika nikainua mkono na kuanza kulifinyanga tonge na kulisomeka kinywani.....akatoa mguno...ulioongeza mshawasha.
Pilipili huwa haikosekani....ofkoz na sharubati.
Baada ya kushiba...tukaendelea kupumzika..... tunasubiri kupambazuke ili tuendelee na swafari.
Naam mawio yamejiri...akanijuza kwamba ana ombi....kwamba leo yeye anataka kuwa dereva.
Nikamkubalia sababu najua yeye ni fundi mzuri....akalipasha gari moto ili kujaza upepo.
GHafla akapiga yowe huku amekamata kichwa cha gia nakuanza kuingiza hiyo gia.
Akaingiza gia huku anapiga ka ukelele fulani ili kufanya swafari inogage.
Lakini kwa khali niliyosikia humo ndani... nikapatwa na mashaka huyu mwanamke hii gia ameingiza namba ngapi???