Ajuza wa miaka 80 abakwa bagamoyo-loh!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajuza wa miaka 80 abakwa bagamoyo-loh!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Feb 10, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,018
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  AJUZA wa miaka 80, mkazi wa kitongoji cha Kiwangwa wilayani Bagamoyo amebakwa na kijana mwenye umri wa miaka 35 na kusababishiwa majeraha makali katika sehemu zake za siri.

  Tukio hilo lilitokea saa 8:00 usiku wa kuamkia jana na kwamba kijana aliyehusika na tukio hilo (jina linahifadhiwa), lakini ni mkulima wa Kiwangwa wilayani humu.

  Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Absalom Mwakyoma alidhibitisha tukio hilo na kusema kuwa bibi kizee huyo alibakwa wakati akiwa amelala nyumbani kwake ambapo mtuhumiwa alitumia mbinu ya kuvunja mlango usiku huo na kuingia katika chumba cha ajuza huyo kisha kumbaka kwa nguvu.

  Mwakyoma alisema tukio hilo linasikitisha na kutia aibu vijana kutokana na ukweli kwamba bibi huyo anaishi kwa shida na taabu nyingi.

  "Inavyoonekana huyo jamaa, alikuwa anamvizia ajuza kwa muda mrefu na nadhani alikuwa akimfuatilia kwa karibu ili kujua mwenendo mzima,alipobaini analala mwenyewe ndipo alipotumia mbinu ya kumvizia muda huo na kuvunja mlango na hatimaye kumbaka hata imani za kishirikina zinaweza kuwa ni chanzo,"alisema Mwakyoma.

  Alisema mlalamikaji anaishi mwenyewe kwenye nyumba hiyo na kwamba tayari mtuhumiwa alikamatwa na anaratajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara uchunguzi utakapokamilika, mlalamikaji anaendelea vizuri.

  Katika tukio jingine Kamanda huyo wa Polisi Pwani alisema mkazi wa Kongowe wilayani Kibaha,(Jina linahifadhiwa) alikamatwa kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo vipande vinne vyenye uzito wa kilogramu 15.1 vya thamani ya Sh 1.1milioni. Tukio hilo lilitokea saa 8.00 mchana juzi katika eneo la shule ya msingi Kongowe na waliomkamata mtuhumiwa huyo ni maafisa wa maliasili wa kituo cha Kongowe kwa ushirikiano na askari polisi na kwamba mzee huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote.

  [​IMG]
   
 2. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 655
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kesi kama hii iliwahi kutokea huko Lindi kipindi cha nyuma na mwenendo wake ulikuwa kama ifuatavyo:

  Muendesha Mashitaka: "Enhe bibi ebu tueleze ilivyokuwa"
  Shahidi 1: "Mheshimiwa, huyu kijana alinivizia wakati nimefunga mlango akavunja na kuniingilia"
  Muendesha Mashitaka: "Endelea kutoa maelezo"
  Shahidi 1: "Sasa alidhani mi ni wa kizamani!"
  Muendesha Mashitaka: "Endelea kutoa maelezo"
  Shahidi 1:"Ikawa akienda kushoto, mi nipo nae, kulia mi nipo mpaka akachemsha"
  Hakimu:"Unamaana gani?"
  Shahidi 1:"Ninamaana niliweza kummiliki vilivyo"
  Hakimu:"Sasa unataka tumpe adhabu gani?"
  Shahidi 1: "Mimi nataka anitengenezee mlango wangu na akija tena abishe hodi nitamfungulia!"
  lol
   
 3. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 655
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Duhh!
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,018
  Likes Received: 37,331
  Trophy Points: 280
  Jamani,
  hivi kijana wa miaka thelathini na tano kwenda kumbaka bibi wa miaka 85 kama sio laana ni nini?
  Jamani msiende kwa waganga, waganga watakulia hela zako kisha watakuambia ufanye jambo ambalo litakupeleka jela uli usimsumbueumbue.
   
 5. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Laanakum!!!!! V
   
 6. M

  Mchili JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nadhani alikosea njia na kwa vile alikua amesha-charge hakuweza kujua kama yule alikua ajuza.
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,935
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  Duh laana kubwa sana, na tukio lenyewe ni bwagamoyo hahha lazima ushauri wa MGANGA wa kienyeji, jamaa anatafuta mapene huyoo kimazingara.
   
 8. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ..............mambo ya mkuyati [​IMG]sioooooooo Ndg. Mchili
   
 9. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hahahahahaha!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...