Ajizi ya Kibuge... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajizi ya Kibuge...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Apr 15, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,432
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Jamani mtalii wetu mtukuka yuko wapi? mbona kaachia ngazi kwenye daladala?

  Imepita muda sijamsikia akishika mchuma au kuzamia mtemba kutembeza ungo kukusanya unga, kauzu na mchunga!

  Je yanayowakabili Baniani ni machungu mno mpaka Kibuge ameacha kukaa nje ya Jamatini akisubiri kiporo cha Cheuro, Pera maziwa na Kuku wa Tanduri na Tika?

  Mara ya mwisho nilisikia alikuwa aongoze msafara wa Wagogo (FMES kumradhi usinishikie marimba!) kwenda Jamatini kudai unga wa dengu, choroko na pilipili, kisa kule nyumbani kwa kina Baniani, wameanza kulishana dengu na maziwa lala!

  Miezi thenasahara mara tatu ukiongeza nne, imemalizika, Kibuge bado kang'ang'ania usukuani wa mabua, akidai anajua njia ya kufika mtoni, lakini kila tukimuuliza tutafika lini anasema tumuache aendelee kuendesha mkweche tusimuingilie kazi.

  Mkweche uko hoi bin taabani, viraka kila kona, mafuta ya breki yanavuja watu washayapigia hesabu eti yanatibu Utangotango, abiria wanapiga kelele Mkweche waenda chopi, utingo anasema tunapiga domo, tuende na wakati tushangilie mwendo kasi, tusihofu kuvuja kwa mafuta na kuungua kwa gasketi!

  Huko juu ya Mkweche ni gombania goli, utingo wako wengi, kila mtu akivutia abiria wake na kujinadi kuwa anajua kubwabwaja hovyo, tairi lina viraka, fundi gari wanadai moto chini!

  Kibuge kakaa kimya, anakenua meno ka mahindi ya Krismasi, kafutuka na ile gogozi yake, anakwangua gia ambalo linasaga chuma kwa kukosa girisi, watu wanalia tema mate, kusanya banjo ulainishe vyuma, anapayuka "babako analo?"

  Sasa mimi nilifikiri Mkweche ni wetu sote, kumbe una watu wake maalum, wenye kujidai kuwa wao ndio wenye mali! Lakini hawachelewi kuchangisha nauli za ziada eti kusaidia Mkweche uende kwenye msitu mzuri watu wakajisaidie.

  Mimi sijali hayo, nalia na ule ungo, Kibuge anatudanganya kila siku akienda kukusanya ufuta na giligilani! Tunamwambia hatuhitaji Sambusa na Kababu, tuna mbaazi na samaki nchanga wenye protini, yeye anadai, lazima tupate pera maziwa, la sivyo tutakufa njaa!

  Akienda Jamatini, hakosi kujikomba komba na kutoa misifa kibao, kazi kuomba kula pozi na MaBaniani wa mitaani na si wale wenye maana ambao watamsukuma akapande mbaazi na kuziuza kwao.

  Nasikia kuna Banyamulenge mmoja, kaamua kuwa yeye na ungo, basi hakuna urafiki na wala hataki tena kupewa viporo na chupi mtumba! Banyamulenge anasema lazima aanze kuwalisha Wagogo, Wanyaturu, Wazaramo na Warangi chakula na kuwavalisha nguo!

  Najiuliza tena Kibuge vipi anapigwa teki na Banyamulenge? Vipi tena mwenzetu hataki Pera maziwa au kuomba Mshiko kwa Baniani eti hana ukoma anaweza jitegemea huku ni mtoto mdogo tuu?

  Lakini nasikia, Kibuge yeye damu damu na Gabacholi! Hata yule Gabacholi anayejitapa kuwa mikuku na miembe yote ni yake ni mshikaji wake ingawa Baniani washamshitukia Gabacholi kuwa ni alosto!

  Sisikitiki Kibuge kupunguza safari kukatisha mitaa na masafa, nasikitika atakachowaambia watoto wake na abiria mwaka huu, maana Baniani dengu zimekauka na wamekuwa wakali!

  Mpeni Kibuge pole zangu, mwaambieni tumeshakubali kachoka, usukani wa Mkweche aachie wenye uwezo wauchukue!
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Apr 15, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 10,424
  Likes Received: 2,668
  Trophy Points: 280
  Siku hizi anatumia internet, na ile e-mail ya ikulu yenye (yahoo)! so usihofu, mabaniani wakisema aende basi anaenda tu kukinga!
   
 3. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kimya cha Kibuge, ni vyema kiwe cha fikira! kwani ungo umeanza kupigwa jua! Na sasa anatanabai uhalisia wa mkweche na utingo wake. Alidhani anautingo mmoja kumbe ni utitiri kila mmoja anatoa taarifa zake. Hamaki, tukombali na ukingoni, lakini malighafi zimetuishia. Mwache ainamishe shingo, tukijaliwa upande na yaliyomema! Ila mema yatajiri pale tu mdogo hautafunga! Waache wagadhabike labda nuru inaweza rejea
   
 4. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,432
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ahhh nasikia Kibuge kapata Baniani mpya!

  KUna Baniani anayeishi Jangwani kuliko kukavu kama Sahara kaja anasema atatupa Bofulo, Chapati na Tende tukimpa uwanja wetu azalishe ngano na tende!
   
 5. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sharti la kwanza la Baniani mpya kwa Kibuge ni kupewa uwanja kwanza (bure) kabla hajaanza kupanga namna ya kutoa bofulo (msisitizo kwenye kupanga). Kama uzoefu uliopita utasimama na historia ikajirudia, Kibuge atatoa uwanja huo, na kugharimia walinzi wa kulinda uwanja huo kwa Baniani bila mjadala.
   
 6. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hizi hadithi za kumpa hekta kwa hekta ni za kweli?
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,432
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kibuge anawaomba kura, anajitapa kawaletea maendeleo mengi, mwasubiri nini kupiga kura? Si mpeni tuu dhamana aendeleze libeneke...?
   
Loading...