Ajira za Walimu kutangazwa Januari 2013 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajira za Walimu kutangazwa Januari 2013

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Brightman Jr, Nov 19, 2012.

 1. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Walimu wapya 28,638 sasa kupelekwa vijijini. [​IMG]

  Na Godfrey Mushi
  19th November 2012
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufunzi, Philipo Mulugo
  Serikali imetangaza mpango mpya wa ajira za walimu 28,638 wa Shule wa Msingi na Sekondari katika mikoa minane.
  Mikoa hiyo ni ile ambayo inakabiliwa na changamoto ya uduni wa miundo mbinu, mazingira bora ya kufanyia kazi na kukosa motisha kwa wafanyakazi kama vile nyumba za kuishi.
  Utaratibu huo wa ajira mpya hautahusisha majiji na manispaa ambako walimu wengi hukimbilia baada ya kupata ajira na serikali imepanga kuwachukulia hatua watumishi wake zaidi 800 waliotoroka kazini na kujiungana vyuo vya elimu ya juu bila idhini ya mwajiri.
  Hatua hiyo ilitangazwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufunzi, Philipo Mulugo, aliyoitoa wakati akizungumza na wahitimu zaidiya 700 wa Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa (MUCE) kilichopomkoani Iringa.
  Mulugo alisema licha ya kuamua kuajiri walimu 28,638 idadi ya walimu wote waliohitimu kwenye vyuo vinavyotoa mafunzo hayo havikamilishi idadi hiyo.
  “Wote hapa, tutawaajiri, lakini safari hii, hakuna ajira mijini na wote mtakaoajiriwa, tunawapeleka katika wilaya zenye changamoto, kwa hiyo mtakwenda mikoa ya Katavi, Kigoma, Rukwa, Mbeya, Shinyanga, Manyara, Mtwara na Lindi. Tamko la serikali ndio hilo na mfahamu kabisa kwamba ajira hizi hazitahusu majiji na manispaa,” alisema Mulugo.
  Alisema ajira hizo zitangazwa rasmi Januari mwaka 2013 huku akionya kuwa wahitimu hao wa shahada ya kwanza ya ualimu katika fani mbalimbali wasithubutu kuwashawishi maofisa waandamizi wa wizara kuombakuteuliwa kuwa maofisa elimu wa wilaya na mikoa.
  Kuhusu walimu waliotoroka kazini na kujiunga na vyuo vya elimu ya juu pasipo ridhaa ya mwajiri, Mulugo alisema serikali imegundua kuwa tatizo hilo limeiathiri zaidi mikoa iliyopo Kanda ya Ziwa na na mikoa ya Kaskaziniambayo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu.
  “Nawatangazia kiama wale ambao walitoroka kazini na kuja kujiunga na vyuo vya elimu ya juu pasipo ridhaa ya mwajiri wake…Wizara imewaagiza maofisa elimu wa Wilaya na Mikoa kuleta haraka majina hayo wizarani ili tuchukue hatua kali,” alisema Mulugo.
  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mkwawa, Prof. Amandina Lihamba, akizungumzia changamoto zinazoikabili MUCE, alisema baadhi ya miradi ya ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu chuoni hapo kwa sasa imekwama na hivyo kuathiri shughuli za taaluma.
  “Tumepokea kutoka Hazina kiasi cha Silingi bilioni 1.3 zilizoidhinishwa na serikali, lakini baadhi ya miradi tunayoiendesha imekwama na kuathiri shughuli za taaluma kwa ujumla,” alisema.
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandala, alisema kuwa MUCE kimekumbana na changamoto za uongozi na utawala na kwamba bodi ya chuo hicho imelazimika kufanya mabadiliko katika ngazi mbalimbali za utendaji.
  CHANZO: NIPASHE

  Wadau habari ndo hiyo!
   
 2. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 9,939
  Likes Received: 658
  Trophy Points: 280
  Neema kwa walimu.
   
 3. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,644
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Kusomea Ualimu ni na kukubali kuajiriwa na Serikali ni tiketi ya kuishi kijijini kwenye changamoto nyingi.
  Ila wake wa vigogo na watoto wa wakubwa hawatokwenda kijijini.
  "Walimu tuna hali ngumu japo tuna umuhimu".
   
 4. oldd vampire

  oldd vampire JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 253
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dah huyu mulugo cjui,mbona kama anaongea kama anahasira na sisi waalimu?yaani mimi ananibore sana ndo maana alikosea speech south,mtupeleke huko msitupe mishahara,dah hii nchi bana
   
 5. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,410
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Hongera zao maana siku hizi ajira imekua ngumu.
   
 6. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ila wajiandae kukabiliana na maisha magumu vijijini.
   
 7. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,410
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180

  Bora ya hayo kuliko kukosa ajira kabisa. Kuna watu wamemealiza chuo miaka karibu mitano iliyopita lakini hawajapata ajira.
   
 8. k

  king rockie ATL JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Safi kabisa hii ni kuhakikisha kuwa shule zetu za kata nazo zinapata waalimu wa kutosha sio kulundikana mijini tu
   
 9. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,730
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  waweke na maslahi mazuri ili wafanye kazi kwa kujituma
   
 10. A

  Anuary Da Handsome'b Member

  #10
  Dec 23, 2012
  Joined: Dec 16, 2012
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  serikali imeshaona darasa la 7 na form 2 walivyofeli hivyo wajipange xana.
   
 11. N

  NYANGESON Member

  #11
  Dec 25, 2012
  Joined: Dec 24, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuwa wazi kama ni jan mwanzon, katikati, mwishon
   
 12. T

  Temba Innocent Jvr Member

  #12
  Jan 18, 2013
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ajira zitatoka january hii,na watu wataenda kaz february mwanzon.Kama ilivyofanyka miaka mingine iliyopita.WALIMU JIPENI MOYO
   
Loading...