Ajira za TISS hutangazwa wapi?

Hm. Kwa anaeielewa kiuhalisia,hivyo vigezo ni zero kabisa.
Labda TISS wa mchongo.
Kwanza ukielewa maana ya TISS yenyewe,kuna kitu utaelewa. Baada ya hapo,utagundua nani amekidhi vigezo vya kujiunga.
Hapa nikupe mfano mmoja,jeshini mpaka mtu awe MP(Military Police),inakuwaje? Maana hawaokotwi mtaani na kupewa hicho cheo. Hawatolewi mtaani na kupelekwa course ya uMP. Lakini wapo.
Halafu,ikitokea ukabahatika kujua utendaji kazi wao,ndo utagundua ni watu gani,wana ujuzi gani,missions zao zikoje.
Kila nchi lazima iwe nao,lakini hawafai hata kusikika. Na ukikutana na mtu aliewahi kujikwaa akakutana nao,kwanza ukimuuliza ni kina nani,wanafanya nini,kama mmekaa,atainuka bila jibu. Kwa nini?
Hapo hutotamani hata kufahamiana nao.
Popote ulipo,ujue wapo. Na ndo maana ukipenda,mambo yako yafanye kwa utaratibu.
Mijama kama ina mission,hata zege itakologa na kubeba. Makande itakula kama haina akili. Kibarua cha kuchimba choo,itachimba,hata kwa nusu ya bei.
Sasa waokote mtaani wa msaada gani?
Nijuavyo mimi,hawa hata ikitokea wakagundulika,mpaka anakata upepo utamtesa lakini hakwambii ukweli.
Nimetumwa na furani,yuko sehemu furani,ahhhh wapi. Huyo jambazi tu.
Mtaani mtu haongei,eti yule ni usalama wa taifa. Wengine eti nikivaa miwani yangu,watu wananikimbia wanajua mi usalama wa taifa. Teh teh teh
Ila wale utakaosikia wanasemwa au watu wanawahisi,jua tu hao ni wambea. Wapo watu ambao kazi yao ni kukusanya taarifa na kupeleka kituo cha polisi,hata mia hawapewi,sifa tu kuingia ofisi ya mkuu wa kituo,basi. Na yeye anaambiwa nenda kafatilie hiki na kile.
Hicho ni kitengo kipo,lakini hakinaga ukweli,wahusika,hawajulikanagi,wao wenyewe hawafahamiani,wenyewe kama wanawindana,na siku ukiwajua,basi ujue hicho kitengo kimeshaingiliwa na kuvujisha siri zake. Hapo kinakuwa tayari kimeshakua MOSSAD
 
muvi zisikudanyanye mkuu,wanajulikana vizuri tuu labda wewe ndio hauelewi wala haufatilii,watu wanajua hatua zao za usahili na rushwa zipo kama kawaida wanao enda kwa mchongo wapo.na kuhusu kuripoti tiss hawaripoti vituo vya polisi wao wanaripoti kwa raisi moja kwa moja ndugu.
 
Muulize kwanza maana halisi ya TISS. Akishaijua,atajua na wanaounda kikosi hicho,na wanapatikanaje
kuhusu kuingia wengi tuu wanaingia kwa michongo ila wakiingia kule wanafuliwa ,kuna wanaojulikana kama PU na ambao hawajulikani
 
ahahha hakikisha jina lako la tatu liko kwenye DB muda mrefu
 
Hatua zao za usahili! zipoje?

Na vipi kuhusu DCEA?
 
kuhusu kuingia wengi tuu wanaingia kwa michongo ila wakiingia kule wanafuliwa ,kuna wanaojulikana kama PU na ambao hawajulikani
Huyo anayejulikana sasa wa kazi gani? Na hayo ndo madhala ya kuteua watu wasiostahili. Mpaka ukisikia badhi ya siri za nshi zinavuja,ujue chanzo ni kama hao. Wengine utaishi nae jirani,au kazini nanhuwezi kustuka. Sasa mtu kalewa,kaanza kukutolea bastola na kutamba ni TISS, nidhamu hiyo? Huyo zero. Wanaujitambua ni ngumu kuwajua,hata umchokoze,hutosikia anakujibu. Anakuchora tu. Si anaangalia uwezo wako kiakili ni hamna.
 
Ndo nimekwambiaje,hao wa mchongo sikatai,lakini hawana vigezo vya kitengo hicho mkuu. Nisiingilie sana maana kazi zao wanazijua wenyewe. Ila, uje uangalie hao wa kileo, na wa miaka kama 25 iliyopita,wana tofauti gani? Ikiwa lengo ni mtu wangu nae ale kwenye pesa ya serikali,siku zote itakuwa hivi. Sasa mtu kazi yake ni mission,na inajulikana yuko wapi,na nani,kafanyeje,si afisa tena huyo.
Ukisema ya movie,ntakwambia utakuwa unakosea kwa sababu,hakuna jambo muafrika analolifanya pasipo kumuiga mzungu. Halipo. Kwa hiyo,ukiwa na wa TISS kama wanaosemekana walienda kumdhulu kiongozi furani wa chama furani,basi wewe huoni uwezo huo wa kazi yao hawana?
 
Umetoa maelezo mengi ila haujaeleza ni vipi ajira za tiss zinapatikana.
 
Nataka kuwapa ronja juu ya Tanzania Intelligence security service moyo unaniambia koma wewe ulishaapa kuilinda ya nchi yangu mpaka kufa.... Any way ngoja nisubili siku nyingine
 

Umeelezea vizuri ila nitakurebesha maeneo mawali. MP ni madaraka sio cheo, na si kweli kuwa spies hawajuani. maybe kwa intake fulani ila most of the time wanajuana. Tofauti ni kwamba wana namna ya kutambuana wanapokuwa maeneo ya kazi, namna ambayo mwananchi wa kawaid ni ngumu kujua
 
Vyema,na asante kunilekebisha. Ila,kwa niaba ya wanaojua,nitoe mfano. Ukiandika vitu kwenye simu yako,una imani ni siri yako hawezi mtu kugundua. Kwa anaeelewa,na mwenye dili zake,kamwe hawezi kutumia simu kubwa kwa hayo mambo.
Sawa na hawa wanaoamini kwamba kila mtu anaweza akapata hiyo kazi kirahisi hivi. Kama ni kweli watu wanachaguliwa, basi nafikili watu waelewe kwamba kuna Informers na TISS yenyewe.
Kama ilivyo,mfano wa karibu. Si kila mwanajeshi ana uwezo wa kuwa commando, au kikosi cha kurinda wakuu wa nchi. Basi ifahamike kwamba na TISS ni tofauti.
Nachoweza kuongezea,kwa sifa za kutekeleza majukumu yao,ndani au nje ya nchi,maana hata tunayoyaona kwenye muvi,ni maigizo ya uharisia. Watu wengi wanaona fahali kuitwa usalama wa taifa. Hivyo kumujua mtu,wao kwa wao watatambuana,kwa sababu furani. Ila wanaweza tambua kama unajiita mmoja wao huku si kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…