Ajira za muda mfupi wakala wa madini (tmaa-mem)

Ajira za muda mfupi wakala wa madini (tmaa-mem)

bhageshi

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2010
Posts
264
Reaction score
101
​

[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 508"]
[TR]
[TD="width: 678, bgcolor: transparent"]
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINIWAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA​
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 454"]
[TR]
[TD="width: 255, bgcolor: transparent"]
[/TD]
[TD="width: 142, bgcolor: transparent"]
​
[/TD]
[TD="width: 209, bgcolor: transparent"]
​
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 255, bgcolor: transparent"]Simu: +255-22-2601819
[/TD]
[TD="width: 209, bgcolor: transparent"]
Kitalu Na. 1129​
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 255, bgcolor: transparent"]Nukushi: +255-22-2601326
[/TD]
[TD="width: 209, bgcolor: transparent"]
Barabara ya Chole, Masaki​
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 255, bgcolor: transparent"]Barua Pepe: info@tmaa.go.tz
[/TD]
[TD="width: 209, bgcolor: transparent"]
S.L.P. 23400​
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 255, bgcolor: transparent"]Tovuti: www.tmaa.go.tz
[/TD]
[TD="width: 209, bgcolor: transparent"]
DAR ES SALAAM​
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 255, bgcolor: transparent"]
[/TD]
[TD="width: 209, bgcolor: transparent"]
​
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 255, bgcolor: transparent"]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 678"]
TANGAZO LA KAZI YA MUDA MFUPI​
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 678"]Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), kwa kushirikiana na Ofisi za Madini za Kanda umekuwa ukifanya ukaguzi wa uzalishaji na mauzo ya madini ya wachimbaji wa kati na wadogo. Lengo la ukaguzi huu ni kutathmini mapato halisi ya wachimbaji na kuhakikisha kuwa wanalipa mrabaha stahiki Serikalini. Kazi ya ukaguzi kwa sasa inafanyika kwa wachimbaji wa madini ya ujenzi na viwandani, wachenjuaji wa marudio ya dhahabu kwa kutumia kemikali ya cyanide na kwa wachimbaji wadogo waliopo katika maeneo ya mifumko ya madini ya dhahabu nchini. Wakala umeweka wakaguzi katika vituo vya ukaguzi vya madini ya ujenzi na viwandani katika Kanda ya Mashariki (Vikindu, Chamazi, Chanika, Mbezi Afrikana, Bunju, Kibaha, Chalinze na Lugoba), Kanda ya Magharibi (Mwandiga, Uvinza, Kakonko, Makere, Kazima na Sumbawanga), Kanda ya Kusini (Nangurukuru) na Kanda ya Kaskazini (Msitu wa Tembo). Pia kuna Wakaguzi wa wachenjuaji wa marudio ya dhahabu na katika maeneo yenye mifumko ya madini ya dhahabu (Mwanza, Geita na Nanyumbu) Hivi sasa, Wakala unaimarisha kazi za ukaguzi katika maeneo yote na unapenda kutangaza nafasi za ajira za muda mfupi kwa vijana wa Kitanzania (26) kwa ajili ya kazi za ukaguzi katika maeneo yaliyotajwa hapo juu kuanzia tarehe 1 Machi 2013. Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:1. Wakaguzi wa madini ya ujenzi na viwandani (Nafasi 21)2. Wakaguzi wa wachenjuaji wa marudio na katika maeneo ya mifumko ya dhahabu nchini (Nafasi 4)3. Msimamizi wa wakaguzi wa madini ya ujenzi Kanda ya Mashariki (Nafasi 1)
Mwombaji anapaswa kuwa kijana raia mwema Mtanzania wenye akili timamu, mwenye ari na nguvu, mwadilifu na mwaminifu na aliye tayari kufanya kazi kwa kujituma bila usimamizi wa karibu.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 678, bgcolor: transparent"]A. WAKAGUZI WA MADINI YA UJENZI NA VIWANDANI (NAFASI 21) SIFA ZA MWOMBAJIMwombaji wa nafasi hizi anatakiwa awe na sifa zifuatazo:1. Umri usiozidi miaka 45:2. Asiwe amewahi kutuhumiwa/kushtakiwa kwa makosa ya jinai kama tuhuma za wizi, udanganyifu au ubadhirifu wa mali ya umma au mtu binafsi;3. Awe amemaliza shule ya msingi au kidato cha nne (4) na kufaulu somo la Hisabati; na 4. Wale waliopitia mafunzo ya Jeshi na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta hasa program ya Ms Excel watafikiriwa zaidi. MAJUKUMU YA KAZI1. Kukagua magari yanayobeba madini ya ujenzi na ya viwandani na kukusanya Hati za Mauzo kutoka kwa wasafirishaji wa madini haya;2. Kuweka kumbukumbu za ukaguzi wa magari yanayopita kituoni ikiwemo aina, uzito na thamani ya madini kwenye kitabu (register)3. Kutoa taarifa zinazohusu ukaguzi wa madini ya ujenzi na ya viwandani kwa msimamizi kila siku; na;4. Kufanya kazi nyingine za udhibiti wa madini zitakazojitokeza kama itakavyoelekezwa na msimamizi.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 678, bgcolor: transparent"]B. WAKAGUZI WA WACHENJUAJI WA MARUDIO NA KATIKA MAENEO YA MIFUMKO YA DHAHABU NCHINI (NAFASI 4) SIFA ZA MWOMBAJIMwombaji wa nafasi hizi anatakiwa awe na sifa zifuatazo:1. Umri usiozidi miaka 45:2. Asiwe amewahi kutuhumiwa/kushtakiwa kwa makosa ya jinai kama tuhuma za wizi, udanganyifu au ubadhirifu wa mali ya umma au mtu binafsi;3. Awe amemaliza Chuo cha Madini na kufaulu kwa ngazi ya Diploma katika fani ya Minerals Processing au Mining Engineering; 4. Wenye uzoefu wa shughuli za uchimbaji na uchenjuaji mbale na ujuzi wa kutumia kompyuta hasusan program ya Ms Excel watafikiriwa zaidi. MAJUKUMU YA KAZI1. Kukagua na kuweka kumbukumbu za uzalishaji wa dhahabu ya wachimbaji na wachenjuaji wa madini ya dhahabu katika eneo husika;2. Kushuhudia na kuweka kumbukumbu za mauzo ya dhahabu kutoka kwa madalali wa dhahabu katika eneo la mfumko wa madini ya dhahabu;3. Kutoa taarifa za uzalishaji na mauzo ya madini ya dhahabu za kila siku; na 4. Kufanya kazi nyingine yoyote ya udhibiti wa uzalishaji wa madini kama itakavyoelekezwa na msimamizi wako wa kazi.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 678, bgcolor: transparent"]C. MSIMAMIZI WA WAKAGUZI WA MADINI YA UJENZI KANDA YA MASHARIKI (NAFASI 1) SIFA ZA MWOMBAJIMwombaji wa nafasi hizi anatakiwa awe na sifa zifuatazo:5. Umri usiozidi miaka 45:6. Asiwe amewahi kutuhumiwa/kushtakiwa kwa makosa ya jinai kama tuhuma za wizi, udanganyifu au ubadhirifu wa mali ya umma au mtu binafsi;7. Awe amemaliza shule ya msingi au kidato cha nne (4) na kufaulu somo la Hisabati;8. Wale waliopitia mafunzo ya Jeshi, uongozi na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta hasa program ya Ms Excel watafikiriwa zaidi. MAJUKUMU YA KAZI1. Kusimamia Wakaguzi wanaokagua magari yanayobeba madini ya ujenzi kwa wasafirishaji wa madini ya ujenzi vituoni;2. Kuhakikisha kazi za ukaguzi vituoni zinafanyika kwa ufanisi mkubwa;3. Kutatua matatizo mbalimbali yanayojitokeza vituoni kwa kushirikiana na msimamizi mkuu wa kazi; 4. Kukusanya Hati za Mauzo vituoni na kuziwasilisha Ofisi ya Wakala;5. Kufanya kazi nyingine za udhibiti wa madini zitakazojitokeza kama itakavyoelekezwa na msimamizi mkuu wa kazi. [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 678, bgcolor: transparent"]MASHARTI YA JUMLA
Inasisitizwa kwamba barua za maombi ya kazi iambatane na utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa/Kijiji au Afisa Mtendaji wa Kata anayoishi mwombaji kuthibitisha uraia na uadilifu wake pamoja na vivuli vya vyeti vya kuhitimu masomo.

ANGALIZO

  1. Waombaji wazingatie sifa zilizotajwa na kuwasilisha taarifa sahihi,
  2. Waombaji waainishe nafasi ya ajira na kituo cha kazi anachoomba kupangiwa,
  3. Barua za maombi ziandikwe kwa mkono na sio kompyuta na ziwe na namba za simu kurahisisha mawasiliano.
  4. Waombaji watakaokidhi masharti ya ajira ya tangazo hili watajulishwa kupitia namba zao za simu ili waweze kuitwa kwenye usaili

Barua zote za maombi zipelekwe kwa mkono kwenye Ofisi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania, Kitalu Namba 1129, Barabara ya Chole, Masaki, Kinondoni Dar es Salaam au zitumwe kwa haraka kwa njia ya Posta kwa anuani ifuatayo:


MTENDAJI MKUU,
WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA,
S.L.P. 23400,
DAR ES SALAAM

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 26 Februari, 2013 saa 9 Alasiri.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Source: Tanzania Daima news paper


 
Back
Top Bottom