Ajira za jeshi katika vyombo vya habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajira za jeshi katika vyombo vya habari

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Hatudanganyiki, Sep 4, 2010.

 1. H

  Hatudanganyiki Member

  #1
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wiki iliyopita chombo kikuu cha dola kilitoa matangazo yasiyo ya kawaida katika vyombo vya habari kuwa inatarajia kuajiri madereva wasio na idadi wenye elimu kuanizia darasa la Saba. Na wanaotaka ajira hizo waripoti moja kwa moja katika Kambi ya Mgulani.

  Hii ni kinyume kabisa na utaratibu wa kawaida wa chombo hicho wa kutoa ajira kwa vijana kwa kupitisha matangazo yake kwa Halmashauri za Miji na Wilaya yakitaja idadai ya nafasi zilizopo, na hatimaye matangazo hayo hufikishwa katika mbao za matangazo na vijiji jna mitaa yetu nchi nzima.

  Maswali ya kujiuliza:-

  1) Kufikia hivi sasa chombo hicho cha ulinzi kilikwisha achana na kuajiri vijana waliomaliza darasa la Saba, na badala yake vijana hao kwanza hupitia chombo kingine kidogo kwa mafunzo ya kujitoklea kwa katia ya miaka 2 hadi 3; na nafasi katika chombo cha juu zikitoka ndipo huweza kuomba kufikiriwa kupata ajira za kuduma katika chombo cha ulinzi cha juu kabisa.

  Lakini kimsingi chombo hicho cha juu hupendelea kuajiri vijana wenye elimu ya kuanzia Kidato cha nne hata kwa upande wa askari wa kawaida kabisa, Iweje mwaka huu wa uchaguzi wabadilike na kuhitaji vijana wenye sifa chini ya hapo na pasipo kutaja idadi ya nafasi zilizopo?

  2) Kwani chombo hicho kimepata kazi gani kubwa ya kiusalama na magari mapaya kiasi cha kuhitaji madereva wengi kais hicho?


  Taarifa zilizolifikia "DAWATI LA HATUDANGANYIKI" huu ni moja ya mipango ya kuhakikisha vijana wengi hususan madereva wa daladala na pikipiki waliopatiwa leseni za udereva kwa wingi hivi karibuni hawawi katika vituo vyao vya kupiga kura itakapofika tar 31 Oktoba 2010. Pili kuwarubuni vajana hawa ili kuwatumia kupiga kura katika sehemu ambazo CCM inataka kama vile Zanzibar, Pemba na hata katika majimbo ya hapa Dar es Salaam kama ambavyo huwa inafanyika mara kwa mara katika chaguzi mbali mbali.

  Madhumuni ya pili ya mpango huo ni kuhararisha usafirishaji wa makundi makubwa ya vijana kutoka sehemu moja hadi nyingine katika kipindi hiki cha kampeni na uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010 kwa kisingizio cha ajira katika chombo hicho.
   
 2. m

  muafaka Senior Member

  #2
  Sep 4, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  unaonaje ukitupa angalau gazeti moja au chombo cha habari kilichotangaza matangazo hayo, ndani ya JF members wengi ni watu wenye upeo mzuri wa kupambanua mambo based on facts.
   
 3. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,718
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  kama Zenji vile....
   
Loading...