Ajira sio kipaumbele awamu hii

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,628
6,669
Kwa hali ilivyo sasa, suala la ajira limefumbiwa macho na wanaohusika kutoa vibali vya ajira wala hata hawana dalili zozote kwamba hili suala litapatiwa ufumbuzi hivi karibuni zaidi ya kusema tu eti hili ni tatizo la nchi zote zinazoendelea. Ni kweli, lakini mbona Kikwete aliajiri kwa kuzingatia kada muhimu kama elimu, afya na kilimo

Kwa visingizio anavyovitoa mheshimia ni dhahiri ili suala kwake si kipaumbele na hakutakuwa na ajira kama wengi wanavyotarajia!

Ajira awamu hii si kwa kada ya elimu wala afya, ingawa nchi bado ibauhitaji mkubwa sana. Vijana mnaosubiri ajira kama mimi, inatakiwa mjiajiri hata kwa kuanza kilimo cha matikiti!
 
Serikali mbona inaajiri tu mkuu....sema ww ndo uajiriwi mkuu na sio serikali haiajiri........rais alisharuhusu vibali zamani sana ...
 
Serikali mbona inaajiri tu mkuu....sema ww ndo uajiriwi mkuu na sio serikali haiajiri........rais alisharuhusu vibali zamani sana ...
Ni uzushi tu, ndo mwezi mmoja na nusu haitazidi miwili (muda ulioahidiwa) ! Au kwake mwezi mmoja una siku 200? Ameharibu mambo mengi sana. Waajiriwa wangeajiriwa kwa muda muafaka wangekuwa na akiba ya kutosha kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, wangekuwa wanakaribia kupanda madaraja, wangekuwa tayari wamepokea barua za kuthibitishwa kazini, watu wameharibiwa malengo yao kwani wameshindwa kuanzisha mambo yao ya msingi kwa matumaini Fake kuwa ajira zitattangazwa hivi punde. Nimeichukia sana serikali hii, hata inifanyie jambo gani zuri siwezi kuielewa! Maana mtu akijaribu kukuua halafu Mungu akakunusuru, itatokea huyo mtu umpende tena maishani mwako?
 
Back
Top Bottom