Mfichua siri
Senior Member
- Jun 19, 2012
- 135
- 62
Wadau wa hili jukwaa mimi ni kijana niliye maliza kidato cha sita hivi karibuni na matokeo yangu yametoka hayana hata wiki moja, ndoto zangu ni kuwa Polisi hasa (trafic), katika kufuatilia ni namna gani nianze mchakato wa kuingia katika kulitumikia Taifa langu katika eneo hili nimepata hili Tangazo hapa chini, kwenye Red pananichanganya sana wanaonyesha ....Wataajiri vijana waliomaliza kidato cha nne mwaka2012 na kidato cha sita 2013 ambao ndo sisi, lakini inaonyesha tayari wanao orodha ya ya watu wa kuwaita kwenye Usaili ilihali wahusika ndo kwanza matokeo yetu yametoka na hawaonyeshi kama wanatutaka tuombe kazi.
Sasa swali langu ni je hizi kazi zilishatangazwa? na hawa form six wa mwaka 2013 wamewapata wapi? maana huwezi ukasema umemaliza kidato fulani wakati matokeo hayajatoka bado, naombeni msaada nataka kujua kama deadline ya kuomba bado na kama bado ni namna gani naweza kuomba hizi kazi na kuwaonyesha kwamba mimi nimemaliza kidato cha sita mwaka2013 maana hata transcripts bado hazijatoka, nimejaribu kwenda Polisi makao makuu juhudi za kuonana na wahusika zimegonga mwamba naombeni msaada plz.

Jeshi la Polisi Tanzania katika mwaka wa fedha 2013/2014 litaajiri vijana kutoka katika makundi yafuatayo: waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012, kidato cha sita mwaka 2013, JKT/JKU mwaka 2013 na vyuo vya elimu ya juu mwaka 2013.Taratibu zinakamilishwa ili waliomaliza kidato cha nne na sita na waliojaza fomu za maombi kabla ya kumaliza mitihani yao ya mwisho waitwe kwenye usaili. Usaili wa vijana wa JKT umekamilika mapema mwezi Aprili, 2013.