Kkimondoa
JF-Expert Member
- May 31, 2014
- 4,452
- 4,938
Jamani tunashukuru serikali kwa kutangaza ajira kwa mara nyingine maana tuliambiwa walimu walio pangiwa budget ni 36000.
Lakini kutokana na walimu hao kuto riport wote vituoni tukaambiwa idadi ya walimu ya ambao hawajariport vituoni ni 2219. Na kupewa taarifa na waziri mwenyewe luwa idadi hiyo ita jazwa lwa kutangaza ajira upya hizo 2219.
Lakini kinyume na hapo jana wametoa majina ya waajiriwa wapya 1728 tu! Na kuwaacha walimu 491 wakiendelea kusota mtaani wakisubiri serikali iliyo wahakikishia ajira wakati wa kwenda mafunzoni.
Sasa kama ilipita budgeti ya walimu 36000 na sasa mmewaacha au mmetuacha walimu 491 maana na mimi ni muhanga wa hili la kuachwa kwa mara nyingine. Sasa inamana tuendelee kusubiri hiyo idadiniliyo baki yaani 491 au ndio basi imekula kwetu?
Na kama imekula kwetu kwa nini mlituhamasisha kusoma ualimu mkituahidi mtatuajiri kwa vigezo kwamba hatutakiwi kupata supp hata moja katika masomo yetu yote na tukatimiza hilo?
Halafu pili katika tangazo lenu mmesema mmezingatia vigezi kama umri ,sawa sina neno lakini hamja eleza ni umri gani huo mlio utaka na hiki ni kitu kipya maana walio ajiriwa mara ya kwanza kuna walio tuzidi umri sisi mlio tuacha mara mbili.
Tunashindwa kuelewa hatma yetu sisi ambao hadi sasa tutakuwa tumesha poteza miaka zaidi ya miwili na bado tumeendelea kuachwa, hasa sisi tulio soma diploma katika vyuo vya serikali.
Na je kama mmesema mmezingatia umri kwanini hamkutuambia wakati mnatangaza nafasi za masomo kwamba katika utoa ajira mtazingatia pia umri? Na hatujajua pia huo umri ni umri gani mdogo sana au mkubwa sana, maana wengine saizi ndio tuna 25yrs, na tumeachwa, au huu ni umri mkubwa?
Tunaomba ufafanuzi kutoka kwa wahusika ili tuelewe maana hadi sasa tumepigwa butwaa hatujui makosa yetu ni nini hadi tumeachwa kwama nyingine, maana barua niliandika,bado nikajaza na fomu mlizo gawa pale TAMISEMI dar lakini pia bado tulituma na majina yetu vyuo tulivyo soma lakini bado tumeachwa.
Tunaomba ufafanuzi tu ,tusuniri hizo 491 zilizo baki ili kutimiza idadi iliyo tajwa na waziri bungeni ambayo ni 2219?
NAWASILiSHA!!
Mods chonde naomba msiipeleke hii jukwaa la elimu maana wahusika wa hili hawapiti sana kule plz.!