Ajira mpya: Serikali itukumbuke sisi wenye shahada za namna hii...

matemabi

Senior Member
May 2, 2017
113
145
Salamu kwako wewe uliechaguliwa kupitia mfumo wa TCU lakini huna uhakika kama kile ambacho umekisoma unaweza pata ajira serikalini ama katika taasisi ambazo si za kiserikali.

Tangu nilipoanza chuo pale Kampala international university kwa kozi ya conflict resolution and peace bulding mbayo nilipata kuchaguliwa kwa kupitia mfumo ule TCU sijawahi kuona hata siku moja serikali ama taasisi binafsi zinatangaza kuwa zinahitaji kuajili watu waliosomea shahada hii. Nilikuwa nikisaka sana nakukuta ni Umoja wa Mataifa na taasisi nyingi ambazo ni za nchi nyingine haswa baani Ulaya.

Nimeanzisha uzi huu kukukaribisha wewe uliyesoma kozi yoyote ile ambayo hukuwahi kusikia wakiitangaza kuwa wanataka kuwaajiri mtu kama wewe. Nadhani hili kwa namna moja ama nyingine itaweza kukumbusha serikali/taasisi nyingine kuwa kuna watu kama sisi.

Pia itawakumbusha TCU kama waliweza kuruhusu wanafunzi kuchagua kozi walizoziorodhesha ina maana kuwa hata serikali ama taasisi nyingine zitatoa ajira hizo.

Basi sasa weka kozi yako hapo chini kuikumbusha serikali kuwa kuna watu kama sisi ambao waliorodhesha kozi.
 
hahahahahaha!!! tukumbukwe kwakweli wengine shahada tumechukua kutunza kumbukumbu ajira huwa naona wanataka wenye cheti na diploma tu pia tukumbukwe
 
Sijui wale wa BA archeology nao watasemaje?
Tatizo mlikuwa mnasoma kozi za kwenye "magazeti"...Mkiwa grp discussion mnapeana ma-hope kuwa kazi zenu ni UN na mashirika makubwa makubwa.

Sisi wazee wa Plumbering ngoja tuendeleee na kuunganisha tu mabomba
 
Salamu kwako wewe uliechaguliwa kupitia mfumo wa TCU lakini huna uhakika kama kile ambacho umekisoma unaweza pata ajira serikalini ama katika taasisi ambazo si za kiserikali.

Tangu nilipoanza chuo pale Kampala international university kwa kozi ya conflict resolution and peace bulding mbayo nilipata kuchaguliwa kwa kupitia mfumo ule TCU sijawahi kuona hata siku moja serikali ama taasisi binafsi zinatangaza kuwa zinahitaji kuajili watu waliosomea shahada hii. Nilikuwa nikisaka sana nakukuta ni Umoja wa Mataifa na taasisi nyingi ambazo ni za nchi nyingine haswa baani Ulaya.

Nimeanzisha uzi huu kukukaribisha wewe uliyesoma kozi yoyote ile ambayo hukuwahi kusikia wakiitangaza kuwa wanataka kuwaajiri mtu kama wewe. Nadhani hili kwa namna moja ama nyingine itaweza kukumbusha serikali/taasisi nyingine kuwa kuna watu kama sisi.

Pia itawakumbusha TCU kama waliweza kuruhusu wanafunzi kuchagua kozi walizoziorodhesha ina maana kuwa hata serikali ama taasisi nyingine zitatoa ajira hizo.

Basi sasa weka kozi yako hapo chini kuikumbusha serikali kuwa kuna watu kama sisi ambao waliorodhesha kozi.
Nakushauri uuganishe chuo cha diplomasia kurasini. Matunda utayaona japo yanachelewa.
 
Back
Top Bottom