Ajinyonga kwa kukatazwa kuoa mke wa pili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajinyonga kwa kukatazwa kuoa mke wa pili

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by VIKWAZO, Jun 17, 2011.

 1. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  MKAZI wa kijiji cha Ubinga kata ya Mhugi, Tabora, Bundala Mwandu (26) amejinyonga baada ya walezi wake kumkataza kuoa mke wa pili.
  Akithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Nzega, Issa Muguha, alisema Mwandu alikutwa amejinyonga Juni 13 saa nne asubuhi katika kijiji hicho.
  Muguha alisema, kabla ya kujinyonga, Mwandu alikuwa na mke mmoja na alitaka kuoa wa pili, lakini alipopeleka taarifa hiyo kwa walezi wake, hawakukubaliana na uamuzi huo.

  Baada ya taarifa hiyo kukataliwa, Mwandu alifikia uamuzi wa kujinyonga kwa kutumia kamba ya gome la mti.

  Akizungumza na gazeti hili, babu wa Mwandu, Bulabo Kinimba, alisema alipopata taarifa ya mjukuu wake kutaka kuoa mke wa pili, alimshauri asubiri mpaka baadaye.

  Kinimba alisema alimshauri kwamba kwa sasa umri wake hauruhusu kubeba majukumu makubwa ya familia mbili.
  "Nilimwambia asubiri baadaye ndipo angeze mke wa pili, kwani bado ana umri mdogo, nashangaa kijana wangu amefikia uamuzi huu," alisema babu huyo.

  source gazeti habari leo

  mapenzi au ngono ndio ilikuwa inamsumbua kaaaaaaaaa
  jamani tumfika huku
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Yaani kama kweli kajinyonga kwa hilo then he was mentally disturbed!!!
  Hata kama umependa mwanamke, kumpenda gani huku unaachia watu wengine??
   
 3. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  kama wamegoma na wewe umependa kiasi hicho si bora kujiiba kuliko kujiuwa
  au kuoa kwa nguvu kama yeye kweli kidume
   
Loading...