Ajikata Koromeo Ili Asirudishwe Kwao Toka Uingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajikata Koromeo Ili Asirudishwe Kwao Toka Uingereza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 22, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]Mwanaume mmoja toka Jamaica aliyekuwa akiishi kinyume cha sheria nchini Uingereza amejaribu kujichinja kwa kutumia kiwembe baada ya kupandishwa ndege ili arudishwe kwao Jamaica.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Tukio hilo liitokea muda mfupi kabla ya ndege ya shirika la ndege la Virgin Atlantic kuanza safari toka uwanja wa ndege wa Gatwick jijini London kuelekea Kingston, Jamaica.

  Abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo walipatwa na mshtuko walipomuona Mjamaica huyo akijikata koromeo lake kwa kutumia kiwembe ambacho haijajulikana aliwezaje kuingia nacho kwenye ndege.

  Mjamaica huyo alikuwa akirudishwa kwao Jamaica baada ya kukamatwa akiishi kinyume cha sheria nchini Uingereza.

  Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 449 ililazimika kuahirisha safari yake huku watu wa huduma ya kwanza wakijaribu kunusuru maisha yake kwa kuibandika kwa kutumia gundi sehemu ya koromeo lake.

  Mjamaica huyo aliwahishwa hospitali ambapo baadae alirudishwa rumande akisubiri kurudishwa Jamaica siku nyingine.

  "Aliwahishwa hospitali akiwa na majeraha makubwa sana kwenye koromeo lake", alisema msemaji wa mamlaka ya uhamiaji Uingereza.

  "Alipelekwa mahabusu baada ya kutolewa hospitali, uchunguzi wa tukio hili unaendelea", alimalizia kusema afisa huyo wa Uhamiaji.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Duh! Yaelekea mshikaji kule kwao Jamaica ana soo ya balaa! Mpaka m2 anakataa kwako hakika ana jambo zito alifanyaga na aki2a tu bila shaka kiama kitamhusu.
   
Loading...