Ajifungia ****** baada ya kumuona mume wake baa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajifungia ****** baada ya kumuona mume wake baa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  MWANAMKE mmoja amejikuta akiwa katika mazingira magumu baada ya mume wake kumkuta akiwa baaa na mwanaume mwingine aliyokua nae katika mahusiano ya kimapenzi. MWanamke huyo jina lake halikuweza kupatikana mara moja alijikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kukutwa baa huko maeneo ya Tabata akiwa na mwanaume mwingine.

  Wakati akiendelea kunywa kinywaji na mwanaume huyo ghafla alishutukia mume wake wa ndoa amefika katika baa hiyohiyo kwa ajili ya kupumnzika na kupata kinywaji.

  Mtandao huu ulikuwa eneo la tukio, majira ya saa 12:46 za jioni, huko maeneo ya Tabata na kushuhudia mwanamke huyo akikimbilia ****** kuhofia mume wake huyo asimuone.

  Wakati anainuka na kukimbilia ****** kwa bahati mbaya alionekana na mume huyo bila ya yeye kujua na kuacha mwanaume aliyekaa nae kutogundua chochote kama hali ya hewa ilishabadilika.

  Dakika zilisogea mwanamke huyo alikuwa harudi kutoka maliwatoni, mume wa dada huyo alimuona mke wake huyo na kwenda kuketi karibu na viti vya milango ya maliwato hayo.

  MTandao huu ulibaini kuwa mwanamke huyo aliingia maliwatoni humo baada ya kumuona mume wake kwa kuwa alikuwa amejichimbia humo kwa muda mrefu.

  Baada ya kutaka uhakiki wa kina, mtandao huu ulikwenda maliwatoni na kumkuta mwanamke huyo akiwa anatetemeka na kuwa na wasiwasi na hali iliyomfika kwa kuwa anaweza akahatarisha ndoa yake.

  “ jamani naomba mnisaidie mmoja akanipe handbag yangu iko pale mezani, halafu aniletee kule mbele, mimi sitarudi tena pale mezani mana nimemuona mume wangu ameingia katika mbaa hii” alimwambia mmoja wa mwanamke walioingia ****** humo huku nifahamishe ikisikia maombi hayo.

  “ nisaidieni jamani, kanipeni handbag yangu mniletee huku ****** niondoke nipitie kwa nyuma ili mume wangu asinione

  MWanamke mmoja aliweza kumsaidia kumletea handbag yake lakini kwa bahati mbaya wakati anatoka ****** humo mume wake kwa kuwa alikuwa anamvizia alikaa karibu na ****** hapo alimuona wakati anatoka ****** humo.

  Mume wake huyo alimuita jina na kujifanya kama hakusikia na mume wake huyo alimuita kwa mara ya pili kwa sauti na kugeuka alimuona mume wake na kubaki hana la kufanya kwa wakati huo.

  HAta hivyo mume huyo baada ya kuhakiki kuwa ni mkewe aliendelea na kuagiza kinywaji na mwanamke huyo kuondoka mahali hapo na hatukujua kilichoendelea baadae baada ya kukutana nyumbani.


  NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mambo ya ndoa bwana!
   
Loading...