Ajenda ya wapinzani hasa CHADEMA ni nini?

Ajenda ya wapinzani hasa CHADEMA ni nini?

Kelele zooote ni kwa sababu Magufuli amewabana kwelikweli. Zile blaablaa za oh,
rushwa imekidhiri, watumishi wa Umma wanajiona miungu watu, Serikali inaibiwa kwenye mikodini kutokana na kusafirisha mchanga, TRA hawakusanyi kodi, Bandarini kuna ubadhilifu na porojo kibao hazipo tena.

Huku mitaani heshima debe, tofauti ya wenye nacho na wasio nacho imekuwa ndogo sana, hakuna cha wa viti virefu wala vifupi.

Nawaza tu uchaguzi ukifanyika leo, hoja za Wapinzani ili wapewe kura zitakuwa Magufuli ni dikteta? Bashite? na upuuzi mwingine mwingi? Ubashite wa mtu Unatusaidia nini sisi watanzania? Hata kama angekuwa Dikteta kweli, kwa haya anayoyafanya Magufuli basi tulipaswa tuufurahie huo udikteta wake kama ungalikuwepo maana nchi imeanza kurudi kwenye misingi.

Au agenda yao itakuwa ni kulaani ukweli wa rais kuwaondoa watu kwenye mazoea ya kutofanyakazi? Nani hajui hivi sasa watanzania wameanza kubadilika na kuchapakazi badala ya kusubiri pesa za wala rushwa, mafisadi, za wauza unga. Pesa za hovyohovyo.

Au agenda yao itakuwa kulaani wauza unga kutangazwa hadharani? Katika hili wasipoangalia watanzania watawapopoa mawe maana adhari ya biashara hii haramu ilikuwa imefikia pabaya na tayari madhara haya yalishaanza kuonekana kwa serikali, familia na hata kwa mtu mmoja mmoja.

Au agenda yao ingekuwa kulaani Serikali kununua ndege, kujenga reli kwa kiwango cha standard gauge, kujenga barabara za juu, bomba la mafuta kutoka uganda hadi Tanzania n.k kwa propaganda kwamba mambo hayo hayana faida kwa mtu wa kawaida?

Ni mtanzania gani hajui ndege, reli , bomba la mafuta n,k vitakuza uchumi wetu na hivyo kusaidia upatikanaji wa huduma za jamii kama vile madawa, shule, maji, umeme n.k, huduma ambazo zinamgusa mwananchi wa kawaida moja kwa moja.
Au agenda yao ingekuwa kuwaambia wanancni jinsi gani Lissu, Gwajima na mavuvuzela mengjne yanavyojitanua kuinanga serikali?

Onyo: Kwa porojo,propaganda, udaku na hoja nyepesi nyepesi dhidi ya serikali ya Magufuli manpaswa kujitathmini sana.
 
Tukiangalia huko nyuma tunaona hhaya yalisemwa au kufanywa na viongozi Wa chadema!

1 .2008 -July 2015 walisema kuwa Lowassa ni fisadi na wanashangaa kuwa vibaka wanachomwa moto mitani wakimwacha MTU fisadi kama lowasa akitanua mitaani(video clip ipo mpaka Sasa YouTube) ,wengine wakasema anayemshabikia Lowasa akapimwe akili,wengine wakasema wana ushahidi Wa kutosha kuwa Lowassa ni fisadi, wengine eti ni heshima kwa Mungu kumzomea fisadi kama Lowassa!! Mwishoe tuliona kilichotokea !!kiliwashangaza wengi!!!
Chadema ni ndumilakuwili,wepesi wakupoteza kumbukumbu!ukiwapa nchi waweza kusahau mipaka ya nchi!!

2.walimtukana Lazaro nyarandu kuwa ni waziri ambaye kazi yake nikupiga picha na ......,wakamshutumu kupandisha twiga kwenye ndege,Leo amekuwa shujaa wao kwa kuhamia chadema!!kule kukataa ufisadi kuko wapi?chadema ni ndumilakuwili, ukiwapa uongozi mkubwa waweza kusahau kuwa nchi ni huru!

3.walimsema kuwa Sumaye ni Mr zero!!!Leo kwao ni kimbilio!!chadema ni ndumilakuwili,

4.walisema tusikae na mabosi Wa accasia,tutashitakiwa,Leo hatujashitakiwa!!wamekuja na gia nyengine kuwa accasia hawajapoteza kitu ndo maana hawaJatushitaki!!!

5.waliona kuwa ni bora Lowassa(waliyomwita fisadi) kuliko Dr slaa aliyevunjwa mkono akipinga ufisadi! Chadema wanapoteza kumbukumbu haraka!! Jameni utampaje uongozi MTU Wa namna hii?

6.ni watu Wa fitina!!haiwezekani Leo umsemee MTU uongo kwa wananchi ili wamchukie halafu kesho unasema kuwa sikuwa na maanisha hivyo!!!
Yako mengi sana!!


Kwa hiyo napendekeza chadema wasipewe uongozi wowote labda baada ya miaka 50 watakapokuwa wamejirekebisha
 
Haya ushapost Nenda kachukue buku 7 yako sasa ukanywiee chai na mihogo

Ova
 
Back
Top Bottom