Ajali zimekuwa nyingi kwa sasa

jeipm

JF-Expert Member
Sep 28, 2018
500
821
Kwa wenye kumbukumbu wakati wa awamu ya nne ukifungukia taarifa ya habari, taarifa ya Kwanza ilikuwa inahusiana na ajali mara nyingi ilifika wakati ajali ziliibwa redioni kama wimbo wa taifa.

Awamu ya tano vyombo wa usafiri vilidhibitiwa kwa kiasi chake na mabasi ya mikoani yalifungwa Hadi vingora vya kutoa taarifa kipindi wanapozidisha kasi pindi wawapo safarini na madereva walikuwa wakibadilishana njiani ili kupata muda wa kupumzika

Cha ajabu sijui nini kimetokea sasa, ajali zimekuwa nyingi kila ukifungukia taarifa ya habari utausikia kuhusu ajali.

Jana nilipanda basi toka Igunga Tabora Hadi Morogoro, hysee lile basi lilikuwa linaendeshwa kwa kasi ya ajabu na haikupigwa mkono na askari wa njiani hadi tunafika morogoro.

Kweli kwa namna hii tutafika kweli au ndio wakati wa fungulia mbwa....
 
Hilo linaitwaje?
 
Kuna clip moja lori linakimbia kama lipo kwenye rally, sijui kama ni Tanzania asee πŸ€”πŸ˜€πŸ˜€
 
Sasa kwa nn hukupaza sauti kwa dereva kua anenda speed kubwa ,kwan ajali ikitokea waathirika wakubwa ni ninyi mliopo kwenye basi , sio kila kitu mpaka usubiri serekali mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…