Wana JF leo nilikuwa katika mmoja ya Mikutano nchini Canada. Katika kujadili masuala ya husuyo Tanzania na bila kufahamu kama walikuwemo wa-TZ ndani ya Mkutano ule uliokuwa unazungumzia Utalii Afrika, mzungu mmoja kutoka USA akaamka na kusema wazi mbele ya kikao kuwa .. jamani muendapo Tanzania msipande mabasi yatokayo Arusha/Moshi kwenda Dar... mtakufa na mtakuja kusahauliwa na familia zenu. Ametoa ushuhuda alivyosafiri na basi toka Arusha kwenda Dar bila kutaja basi ya Kampuni ipi na kusikitika alivyozomewa na abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo. Abiria walimtaka ashuke kama yeye anaogopa kufa na walimwambia wao wanaharaka na wanataka kufika Dar mapema. Mzungu anasema ilibidi anywe wine/POMBE ili alewe na asijue kinachoendelea hadi alipofika Ubungo na kuashwa na Girlfriend wake.
Alitoa takwimu za ajali Tanzania na inavyo claim maisha ya watu huko TZ.
Nilijaribu kuomba nafasi nikapata na nikatoa blaa blaa ninazozijua ili angalau kutetea nchi yangu.Maswali yalikuja kama nyuki...
USHAURI: Kwanza ni aibu kwa Taifa kushindwa kupunguza ajali zisizo za lazima kama hizi za barabarani.Pili, pato kubwa la Taifa linatokana na utalii, mambo kama haya yatachangia kupunguza mapato ya Serikali..
Sitaki kuzungumza mambo mengi lakini mnaweza changia nini kifanyike, wafukunyungu watazipeleka kwa JK.
Thanks.
Chanzo halisi cha ajali Tanzania ni Mirungi, Bangi, TRAFFIC POLICE, Valeur, Ufinyu wa barabara na usimamizi mbovu wa sekta ya usafiri
Labda ingewekwa time limit ya basi kutoka point A mpaka B.
Pia kuwe na check points barabarani ku check muda.
Mabasi ya railways yalikuwa na system hizo na ajali zilikuwa ndogo.
Mfano upo iringa unataka kwenda mbeya unajua basil litafika saa ngapi kutoka Dar.
Madereva wakiwahi kufika wanapata matatizo.
Chanzo halisi cha ajali Tanzania ni Mirungi, Bangi, TRAFFIC POLICE, Valeur, Ufinyu wa barabara na usimamizi mbovu wa sekta ya usafiri
ili kupunguza kama si kuondoa kabisa janga hili, yatupasa tufanye yafuatayo:
- kupanua barabara kuu
- kujenga barabara mbili mbili, ya kwenda na kurudi.
- kuangalia sheria za barabarani ikiwamo utoaji leseni, bima kwa wafanyabiashara za usafiri wa abiria, adhabu kwa wanaosababisha ajali, adhabu kwa kampuni. Kama inakidhi hali halisi iliyopo.
- kuangalia upya biashara nzima ya usafirishaji, nafikiri kampuni ya usafirishaji yoyote isiwe ya mtu mmoja, bali iwe ni ya watu kadhaa wenye hisa, na yenye bodi ya wakurugenzi ambao wanakuwa na majukumu ya kusimamia uendeshaji wa kampuni, hii itasaidia kuweka uwajibikaji. Hapa tuanahitaji kutunga sheria ambayo itaanisha vigezo hivi vya kamuni ya usafirishaji. Pendekezo hili ni gumu kufanyika, lakini mimi naamini kuwa itasaidia sana katika kudhibiti uzembe, kuboresha maamuzi na uwajibikaji. Kwa mfumu uliopo sasa wa kuwa mtu anaweza kumiliki kampuni yake, naona unashusha uwajibikaji na inaongeza uzembe. Ofcourse, uchumi wetu ni wa kibepari lakini naona linapokuja suala la uhai wetu, tusifungwe na kanuni hizi za kiuchumi.
- abiria wenyewe tutoe ushirikiano katika kudhibiti ukiukwaji wa sheria barabarani, mf. Kama gari limejaa kwanini ulazimishe kupanda? Dereva anaenda mwendo wa kawaida, kwanini umshurutishe awahi, ama anaenda kasi kwanini usitoe onyo?
- tuendeleze njia mbadala za usafiri, njia kubwa ya usafiri ni reli, tutandaze mtandao wa reli nchi nzima, nchi nyingi zilizoendelea, na zinazoendelea mf china, wanatumia reli kama njia kuu ya usafiri, kwa siku kunaweza kuwa na treni 10 zinaenda mji mmoja. Kama tukiboresha njia hizi mbadala, tutawezesha ushindani wa kibiashara, jambo ambalo litahamasisha uboreshaji wa huduma, ikiwapo pamboja na usalama wa abiria.
- mwisho, si kwa umuhimu, jeshi la polisi liwe na uzalendo, askari unaona basi lina tairi kipara, lakini unaliacha liende na safari, au umegundua lina kasoro fulani, unatoza faini halafu unaliacha liendee na safari, mi naona bora abiria wakwame na safari kuliko kuchinjwa. Jeshi la polisi lijirekebishe, ili kurudisha imani ya jamii kwao.
ni mada sensitive sana. lakini inapozungumziwa maisha ya watu Tz, nobody anajali. Sijui why,ila naona uhai hauthaminiwi kabisa bongo as if tuna 2nd chance.Tunajua vifo vingi vinavyosababishwa na mwendo kasi,utajiuliza wapi speed gavanor? mbona hatusikii zikikaguliwa tena? utajiuliza kwanini zisiwekwe camera barabarani,je ni expensive kuliko uhai wetu? police anakamata gari linaenda kasi au bovu au dereva hana leseni,anamuachia kwa rushwa ya 5000tsh,je uhai wetu hauna thamani kiasi hicho? Ujinga wetu pia unasababisha hayo,kama huyo mzugu alivyosema,watanzania wanashangilia mwendo kasi,wanataka kuwahi ikitokea ajali ndio wanamlaumu dereva.Tuchukue hatua,hakuna haja ya kufanya utafiti au kuwasilisha mapendekezo serikalini.sisi tukatae madereva au magari yanayohatarisha uhai wetuTakwimu zinaonesha ajali safari zinaua zaidi ya ukimwi, nyuma ya malaria.
The only people can change the systems is us... We need to act now and not to wait for the un known Government which can't act...
ni mada sensitive sana. lakini inapozungumziwa maisha ya watu Tz, nobody anajali. Sijui why,ila naona uhai hauthaminiwi kabisa bongo as if tuna 2nd chance.Tunajua vifo vingi vinavyosababishwa na mwendo kasi,utajiuliza wapi speed gavanor? mbona hatusikii zikikaguliwa tena? utajiuliza kwanini zisiwekwe camera barabarani,je ni expensive kuliko uhai wetu? police anakamata gari linaenda kasi au bovu au dereva hana leseni,anamuachia kwa rushwa ya 5000tsh,je uhai wetu hauna thamani kiasi hicho? Ujinga wetu pia unasababisha hayo,kama huyo mzugu alivyosema,watanzania wanashangilia mwendo kasi,wanataka kuwahi ikitokea ajali ndio wanamlaumu dereva.Tuchukue hatua,hakuna haja ya kufanya utafiti au kuwasilisha mapendekezo serikalini.sisi tukatae madereva au magari yanayohatarisha uhai wetu