JAPUONY
JF-Expert Member
- Jul 16, 2010
- 383
- 186
Wana JF leo nilikuwa katika mmoja ya Mikutano nchini Canada. Katika kujadili masuala ya husuyo Tanzania na bila kufahamu kama walikuwemo wa-TZ ndani ya Mkutano ule uliokuwa unazungumzia Utalii Afrika, mzungu mmoja kutoka USA akaamka na kusema wazi mbele ya kikao kuwa .. jamani muendapo Tanzania msipande mabasi yatokayo Arusha/Moshi kwenda Dar... mtakufa na mtakuja kusahauliwa na familia zenu. Ametoa ushuhuda alivyosafiri na basi toka Arusha kwenda Dar bila kutaja basi ya Kampuni ipi na kusikitika alivyozomewa na abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo. Abiria walimtaka ashuke kama yeye anaogopa kufa na walimwambia wao wanaharaka na wanataka kufika Dar mapema. Mzungu anasema ilibidi anywe wine/POMBE ili alewe na asijue kinachoendelea hadi alipofika Ubungo na kuashwa na Girlfriend wake.
Alitoa takwimu za ajali Tanzania na inavyo claim maisha ya watu huko TZ.
Nilijaribu kuomba nafasi nikapata na nikatoa blaa blaa ninazozijua ili angalau kutetea nchi yangu.Maswali yalikuja kama nyuki...
USHAURI: Kwanza ni aibu kwa Taifa kushindwa kupunguza ajali zisizo za lazima kama hizi za barabarani.Pili, pato kubwa la Taifa linatokana na utalii, mambo kama haya yatachangia kupunguza mapato ya Serikali..
Sitaki kuzungumza mambo mengi lakini mnaweza changia nini kifanyike, wafukunyungu watazipeleka kwa JK.
Thanks.