ajali ya zanibar bussinesswise....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,218
91,811
ajali ya zanzibar ya meli imeua watu 200 au zaidi
wameokolewa zaidi ya 500 inasemekana walikuwa zaidi ya 3000

sasa hapa napata maswali ya kibiashara,atakaeweza kunisaidia nitashukuru...

1.nauli walilipa kiasi gani?
2kwa kawaida nauli ni kiasi gani kati ya unguja na pemba
kwa meli na boti?

3.meli au boti zipo ngapi zinazofanya biashara njia hiyo ya unguja na pemba?
4.wastani ni watu wangapi wanakwenda au kutoka unguja na kwenda au kutoka pemba?

5.ni masaa mangapi kwa meli au boti,wastani
6.mizigo ya aina ipi hasa inasafirishwa kati ya unguja na pemba?
7.na mengineyo.....
 

Mani H

Senior Member
Mar 25, 2011
180
45
kabla sijakujibu maswali yako naomba nikupe taarifa iliyotolewa na serikali ya zanzibar hadi sasa , idadi ya abiria inayotambuliwa na serikali kwa uharaka zaidi ni 610 ni ile idadi ya ununuzi wa ticket, ila inakadiliwa ilikuwa na abiria kati ya 900 - 1000, waliokolewa wakiwa hai 601 na waliopatikana wakiwa wamekufa ni 192 mpaka sasa na bado jitihada zinaendelea kufanya la kuokoa na kutoa miili ya marehemu.

majibu ya maswali yako
1.nauli walilipa kiasi gani?
nauli ni sh.11000 per head.

2.kwa kawaida nauli kwa meli nish.11000 per head na boat ni sh.22000per head,(from unguja to pemba).

3.meli za abiria zinazokwenda unguja to pemba zilikuwa tatu ambazo ni serengeti, buraq, na hiyo spice islanders inamaana kwa sasa zitabaki mbili tu kwa kuitoa hiyo ilipata ajari. pia boat zinazoenda uko ni mbili tu ambazo ni sea express na seagul .

4.abiria wanasafiri huwa awana wastani maalamu kwa sababu wasafiri wa sehemu hizo utegemea sana msimu na matukio mbalimbali , nina maana kuwa kuna msimu wa mavuno ya karafuu huwa watu wengi kusafiri kwenda pemba, na pia kipindi cha sikukuu kuja unguja, ila kwa makadilio ya chini kwa wasafiri wa kila siku ni 1000 pemba to unguja na unguja to pemba.

5.wastani wa masaa kwa boat ni masaa 3, na kwa meli ni 6 kwa mchana na 7 kwa wakati wa usiku.

6.pemba to unguja aina ya mizgo inayosafirishwa ni mazao ya chakula, kuku, samaki n.k, unguja to pemba ni bidhaa zote za madukani na pia mzao ya chakula ambayo pemba awalimi ni kma vile viazi (mbatata) ngano,nk.

7. mengineyo. kwa ufupi pemba na unguja wanategemeana aslimia mia kwa mia na hii upelekea kuwa waunguja kuishi pemba na wapemba kuishi unguja katika harakati zao za masiha ya kila siku.

kwa ushauri wangu kuhusu biashara ya usafirishaji kupitia bahari. biashara hii ina risk kumbwa kwa chombo chako na abiria pia, vyombo vyote hudumu kwa muda mfupi sana kwa sababu chumvi ya bahari inaharibu sana machine za vyombo hivyo. kwa sababu hiii wafanya biashara wengi upata hasara kwa kutopata faida na wakati mwingine kujikuta kupoteza na mtaji pia. vilevile ina risk kubwa kwa usalama wako binafsi, maana wakati wowote unafikishwa mahakamani na usipo kuwa makini unaishia kufungwa. ahsante
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,218
91,811
mani h
asante saana
hivi umesema nauli ni elfu moja na mia moja?
au elfu kumi na moja?
 

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
Naomba ufafanuzi tofauti ya boti,meli na ferry

Mzee ferry ni commuter boat, yaani boat inayotumika kufanya biashara ya kusafirisha watu kibiashara. Haina tofauti na hiace za mjini zinazobeba abiria mjini. si kuna zingine ni private ambazo hazibebi abiria kibiashara. Hilo la meli mkuu tia akili mwenyewe!!!!!!!
 

Mani H

Senior Member
Mar 25, 2011
180
45
Naomba ufafanuzi tofauti ya boti,meli na ferry

boti,meli na ferry hivyo vyote nivyombo vya majini na utofautiana au tofauti yake inatoka na size, passenger capacity na cargo. vitu hivyo ndio vinavyotofautisha na kuvipa hivi vyombo majina tofauti.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom