Ajali ya Wazari wa Michezo

inols

JF-Expert Member
Sep 22, 2010
283
95
Jamani mwenye taarifa kamili juu ya ajali ya waziri wa michezo tunaomba atupatie
 
Labda Mungu ameanza kulipiza kisasi kwa Dr. Ulimboka. Kwani Mwenyezi Mungu huwapigania wanyonge na walionewa.
 
NEWS ALERT: Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo apata ajali mbaya maeneo ya Nzega Mkoani Tabora mchana huu


Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh.Dkt. Fenella Mukangara (pichani) amepata ajali mbaya mchana huu maeneo ya Nzega Mkoani Tabora wakati akiwa njiani kuelekea Jijini Mwanza kwenye Ufungunguzi wa Mashindano ya Taifa ya Mchezo Vishale (Darts) yanazinduliwa leo Jijini humo.


Globu ya Jamii imefanya mawasiliano na Mh. Mukangara na kuthibitisha kupata ajali hiyo ambapo anasema chanzo chake ni kuchomekewa na basi moja la abiria (ambalo hakulitaja jina lake).


"Ni kweli tumepata ajali hapa maeneo ya Nzega Mkoani Tabora wakati tukiwa njiani kuelekea jijini Mwanza ambako leo kunafanyika ufunguzi wa Mashindano ya Taifa ya Mchezo wa Darts,tunashukuru Mungu wote tumetoka salama japo tumepata majeraka katika sehemu mbali mbali za mwili."Alisema Mh. Mukangara.


Tunaendelea kuwasiliana na Mh. Mukangara na tutaendelea kupeana taarifa zaidi.

HU1.JPG
 
waziri wa serikali ipi?mi sijaelewa hivi kuna serikali Tanzania?
 
Back
Top Bottom