Ajali ya treni dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali ya treni dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Charles Mkubya, Jan 12, 2010.

 1. Charles Mkubya

  Charles Mkubya Verified User

  #1
  Jan 12, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Kuna ajali imetokea usiku karibu na mataa ya Chang'ombe ukitokea Karume ikihusisha Treni na Magari mawili ya abiria, moja ikiwa ni ya Mbagala na nyingine ya Tandika. Majeruhi ni wengi japo sijashuhudia maiti lakini uwezekano wa kuwapo watu waliopoteza maisha upo. Atakaekuwa na taarifa zaidi asisite kutupasha ila nawapa pole wote walipatwa na tatizo hili kwa namna moja au nyingine
   
 2. American lady

  American lady Member

  #2
  Jan 12, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  oh my god hizi ajali zitaish lini zinawapa mojonzi walimwengu namna hii?poleni sn walengwa.
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Gosh kila siku nipitayo lazima tusikia ajali eeh mungu mwenye habari zaidi atupe update
   
 4. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  kwanini mamlaka ya reli isiweke mageti pale reli inapopishana na barabara? Pia kwanini isiweke mlinzi hapo wa kuwa anawasiliana na matreni hayo wakati treni linakuja basi anafunga geti mpaka treni lipite? Pole kwa waliopatwa na ajali!
   
 5. O

  Omumura JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mwekezaji mhindi ametema walinzi wote wa magetini, tutegemee ajali nyingi zaidi ya hizo katika maeneo yote ambapo reli inapita.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Pole kwa yaliyotokea,
  Pili Mkubya2 karibu jamvini. Pia naomba be a bit more specific, ukisema tuu ajali ya treni, ni too broad. Sema ni treni ya TRC au Tazara. Ukiachia kwenye treni tuu, watu watajua ni reli ya kati.

  Pia unasema ni treni ya mizigo au abiria, ni treni kweli au kichwa cha treni, au kiberenge, ukiishia kwenye treni tuu, picha inajijenga ni treni ya abiria.

  Pole tena kwa wahanga wa ajali hii.
   
 7. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Pasco, unless wewe ni mgeni wa jiji la Dar, Mkubya amesema karibu ya mataa ya chang'ombe ni wazi ni treni ya TRL (si TRC kama uliweka wewe) au Tazara kwani Treni ya Tazara haipiti maeneo hayo.
  Suala kuwa aseme ni treni ya mizigo, abiria, kichwa au kiberenge haina umuhimu, issue ni kuwa ajali imetokea, . Suppose kilikuwa ni kichwa au hiyo siyo treni?? au unadhani treni ni mabehewa??.
   
Loading...