Ajali ya ndege, somo la utu na ubinadamu

Joshua justine

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
792
1,007
Kila siku huwa nasisitiza jambo hili, mtu asimdharau binadamu mwenzie kwenye dunia ya leo (isipokuwa tu kuchukua tahadhali ya kiusalama).

Ukiwa na pesa, una gari nzuri, mijengo ya maana n.k jitahidi kutokuonuesha dharau ya makusudi kwa wale watu ambao wanaonekana wa hali dhariri sana kwako.

Ni mara ngapi kwenye majanga wale tunaodhani ni wa hadhi yetu huwa hawapo karibu kutupa msaada wadharura tunaouhitaji?

Mbali na hayo pia, hata katika mifumo ya uzalishaji wa aina yoyote ile wa huduma ama uzalishaji wa bidhaa za kawaida popote pale, mchakato wa uzalishaji huanza juu mpaka chini ndipo ukamilike kabisa, hata yule aliweka na kupack bodhaa kwenye box nae pia ni wa muhimu kama wale walioitengeneza kwani akiaamua kufanya hila kwa siri basi brand nzima itachafuka bila kujali elimu za wahusika.

Mvuvi ama wavuvi hao wamekuwa wakitajwa kama watu wa kawaida ila wameokoa uhai wa watu wanaojidhani ni matawi ya juu wakiwa angani, hili liwe somo kwa watanzania.

NASISITIZA : USIMDHARAU MTU ILA USIMUAMINI KILA MTU, JILINDE BILA KUDHARAU BINADAMU WENZAKO.
 
Viongozi kama Nape, Makamba,Mabula na Mwingulu ipo siku mtapata taabu sana na hamna atakayewasaidia mtajisaidia hapo hapo hamtaweza kwenda chooni.
 
Viongozi kama Nape, Makamba,Mabula na Mwingulu ipo siku mtapata taabu sana na hamna atakayewasaidia mtajisaidia hapo hapo hamtaweza kwenda chooni.
Kwa Nape, Makamba hata Membe na Mkwere unawaonea tu. Wangeamua kulipiza kisasi unadhani maadui zao wangepona. Wameshika sasa hivi madaraka wameshika mpinni Ndo kwanza wamewasamehe na kuwapotezea maadui zao.

Kumbuka utawala wa shetani walivyokuwa wakiua na kudhuru hovyo hovyo kwa kusemwa tu.

Achana kabisa na kina nape wana utu. Mimi waliniumiza tu walipompiga vita rais wetu lowasa lakini nimewasamehe.
 
Back
Top Bottom