Ajali ya ndege CCM wapongezana.

Ajali ya ndege CCM wapongezana.

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
24,607
Reaction score
30,222
Kama kawaida ya CCM leo wakati wakuaga miili ya waliopoteza maisha kwenye ajali ya ndege, CCM wametumia muda mwingi kupongezana. Pongezi za kujirudiarudia vimepelekwa kwa viongozi wa CCM mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita na Mwanza kwa kushiriki kwenye uokoaji akizitoa Shaka! Na waziri Mkuu akisema Mwenyekiti wa CCM ameacha shughuri zote ili afuatilie na kutoa maelekezo ya uokoaji kutoka uarabuni!
Katika hali ya uchoyo na kutojiamini Waziri Mkuu alitoa salamu kwa viongozi wote akashindwa kuwatambua viongozi wa upinzani, chuki mpaka kwenye misiba, yaleyale ya Arusha kwenye msiba wa wanafunzi yanajirudia sijui kama na huu msiba watazipiga hela za rambirambi, Kagera walizipiga hela za tetemeko na Arusha walipobanwa wakajibaraguza na mwisho zikaliwa, waswahili husema "nyama nono usimpe masikini aigawe, itamuozea mikononi".
 
Kama kawaida ya CCM leo wakati wakuaga miili ya waliopotezaaisha kwenye ajali ya ndege, CCM wametumia muda mwingi kupongezana. Pongezi za kujirudiarudia vimepelekwa kwa viongozi wa CCM mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita na Mwanza kwa kushiriki kwenye uokoaji akizitoa Shaka! Na waziri Mkuu akisema Mwenyekiti wa CCM ameacha shughuri zote ili afuatilie na kutoa maelekezo ya uokoaji kutoka uarabuni!
Katika hali ya uchoyo na kutojiamini Waziri Mkuu alitoa salamu kwa viongozi wote akashindwa kuwatambua viongozi wa upinzani, chuki mpaka kwenye misiba, yaleyale ya Arusha kwenye msiba wa wanafunzi yanajirudia sijui kama na huu msiba watazipiga hela za rambirambi, Kagera walizipiga hela za tetemeko na Arusha walipobanwa wakajibaraguza na mwisho zikaliwa, waswahili husema "nyama nono usimpe masikini aigawe, itamuozea mikononi".
Kumbe huyo mama yuko Uarabuni, nilikuwa sijui nashukuru kwa taarifa
 
Tatizo hatuna viongozi, kuna walaghai wanaojiita viongozi
 
Viongozi wa CCM ni tatizo, wafiwa wamekaa wanahamu wachukue miili ya ndugu zao wao hawaoni umuhimu zaidi ya wao kupongezana kwa kurudiarudia! Ni CCM haohao waliokula michango ya wanakagera wakati wa tetemeko kwa madai serikali haikuleta tetemeko! Wahanga wengine mpaka leo wameshindwa kuzijenga nyumba zao, ni kweli nyama iliyonona usimpe masikini aigawe, itamuozea mikononi.
 
Back
Top Bottom