Ajali ya moto Msamvu, Morogoro: Waziri Mkuu aunda Tume ya kubaini kama mamlaka zilishindwa kutimiza wajibu

Hatimaye Waziri Mkuu naye kajiuliza swali ambalo wengi wetu tumejiuliza tangu jana ila tukawa tunapingwa kwamba askari wasilaumiwe.

Pale msamvu ndani ya stendi kuna askari muda wote wakuruhusa magari, nje ya stendi kuna kituo cha askari, kutoka fire hadi msamvu si zaidi ya dk 5 (hawa wanaweza kuchelewa kidogo kwasababu mpaka wawashe gari, wajaze maji, watafutane, watafute vifaa)

ila polisi wa kuzuia watu wasiibe mafuta na kuwasaidia dereva na tingo wake baada ya ajali wasingeweza kukosekana kwa eneo lile!

Hivyo lawama hawazikwepi kwani kwa umbali wa walipokuwa na eneo la ajali kufika ni chini ya dk 1 labda tuambiwe ajali inapotokea lazima asubiriwe askari mwingine toka central wale wa pale msamvu hawaruhusiwi kujishughulisha na kitu kingine zaidi ya kuongoza magari!?View attachment 1178222
ni muda gani ulipita kutoka ajali mpaka mlipuko?
 
Jamii forum mnanongwa yaani nyuzi kibao ilimradi moto uwende na watu!
kumbukeni hawa nao wanawatoto na wazazi pia.
Haaa haaaa kama ulifanya uzembe Mkuu kubali kuwajibika,wale waliofariki nao wameacha watoto bora wewe ukitumbuliwa watoto wako watakuona na unaweza ukawa mkulima mzuri tu kule Ifakara,kilosa au popote pale hapa Tanzania.
 
hapana
  • kwani hii ni ajali ya kwanza kutokea ya namna hii?
  • au je tulishatoa huko nyuma maelekezo ni kwa jinsi gani gari la mafuta likianguka linastahili kulindwa au taathari gani zichukuliwe?
  • je tumeweza kufikiria kuwa hawa jamaa walikuwa ni wezi au huruma tu sinatujaa kwasababu wamekufa?
wanasiasa sio wazuri watawafukuza watu bila sababu za maana wakati tunatakiwa kuweka misimamo ya siku zijazo.
  • mfano mzuri katika stendi zote za mkoa hakuna zima moto hata moja hii hatuioni hatari? na hili ni la kufanya lakini pia katika barabara kubwa kunatakiwa kuwe na zima moto hata moja kwa kuanzia kwa wastani tungekuwa tunajiweza kila baada ya km200 kuwe na zima moto lakini gari moja linauzwa zaidi ya 400m je tunazo?
Mkuu umeongea point sana,hatuko serious na majanga kama watu wameweza kununua magari 35 kwa bilioni 14 wanashindwaje kunua magari ya zima moto?

Angalia wilaya nyingi hazina hata gari moja ya zima moto,nchi inashindwaje kuwepo angalau gari za zimamoto tatu kila wilaya?mbona kila wilaya kuna cruser kibao,DAS,DED,DMO,wote hao wanatumia cruser,Serikali wao Magari ya kuzimia moto siyo kipaumbele.
 
nafikiri polisi(kituo cha msamvu)walikua wanasubiri amri kutoka juu,maana hawa sasa sioni kama wanafahamu wajibu wao
 
Waziri Mkuu Aunda Tume Kuchunguza Ajali Ya Morogoro

MPEKUZI / 7 hours ago

[https://1]

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameunda tume maalumu kwa ajili ya kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali ya moto iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 69 hadi mchana huu na wengine 70 kujeruhiwa wakati wakichota mafuta yaliyokuwa yakimwagika baada ya lori la mafuta kupinduka, mjini Morogoro.


“Hii tume inaanza kazi leo (Jumapili, Agosti 11, 2019), Hadi ijumaa inipe taarifa yake na hata kama mimi sijawajibika initaje. Ajali ya namna hii si mara ya kwanza ilitokea Mbeya eneo la Mbalizi. Naomba niwasihi Watanzani pale gari linapoanguka tusitume kama fursa twende tukaokoe binadamu waliopo pale”.


Waziri Mkuu ameunda tume hiyo leo (Jumapili, Agosti 11, 2019), wakati akizungumza na waombolezaji waliofika katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kutambua miili ya ndugu zao. Niko mbele yenu nikimwakilisha Rais Dkt. John Magufuli aliyenituma kuja kuungana nanyi kwenye siku hii ya huzuni”.


Waziri Mkuu amesema lazima wajiridhishe kama Serikali ilitekeleza vizuri jukumu lake kwa sababu ajali imetokea saa mbili asubuhi katikati ya mji, hivyo tunataka kujua ajalj ilipotokea kila mmoja alitumiza jukumu lake.


Amesema ajali imetokea karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi na kuna polisi sasa je hawa wananchi waliopata ajali walienda na madumu ya kuchotea mafuta inamaana waliamka asubuhi wakijua ajali itatokea. “Najua pale ajali inapotokea trafiki wana wahi haraka hata kama kwa gari la kukodi. Watu walikuja na madumu, wengine kuchomoa betri nani aliwazuia.Je lilipoanza kuungua gari la zima moto lilikuja kwa wakati gani”.


Waziri Mkuu amesema lazima wajiridhishe ndani ya Serikali kama wamewajibika. “Kuna vitu vingi lazima tuviangalie tujue nani hakutimiza majukumu yake. Nadhani ujumbe mnaupata si vyema tutakimbilia vitu badala ya watu. Tunasikitika sana kwa yaliyotukuta hata upande wa Serikali tunasikitika kuwapoteza Watanzania”.


Pia, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu jitihada za kuokoa waliopata majeraha kwamba zinaendelea vizuri na jukumu lao kubwa kuwaombea marehemu wapumzike kwa amani na pia wawaombee wajeruhi waweze kupona.


Waziri Mkuu ameongeza kuwa, Rais Dkt. Magufuli tayari ameshatoa kibali cha kutolewa fedha kwa ajili ya kununuliwa vifaa tiba na dawa zinazohitajika.


Akizungumzia kuhusu idadi ya vifo na majeruhi waliotokana na ajali hiyo ambayo inatangazwa kupitia vyombo mvalimvali vya habari, Waziri Mkuu amesema ni vema takwimu hizo wakaacha zikatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Stephen Kebwe.


“Kwenye vyombo vya habari tuelewane kwenye takwimu za vifo na majeruhi. Msiseme suala la takwimu anayetoa ni Mkuu wa Mkoa na matukio haya yapo chini yake. Nimeamua kusema hivi hizi takwimu zikitajwa nyinginyingi mnajenga hofu na taharuki kwa wananchi. Hili halikubaliki mkitaka taarifa mtafuteni mkuu wa mkoa”.


Wakati Huo huo, amesema Rais Dkt. Magufuli alipokea taarifa mapema ya ajali ya lori la mafuta na kusababisha vifo vya Watanzania 69, ambapo alimtaka aende mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwasilisha salamu za pole kwa wananchi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla kufuati tukio hilo la kuhuzunisha.


Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli anawaombea marehemu na majeruhi lakini pia amawataka wafiwa na wananchi wote wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na wapendwa wao.



“Mheshimiwa Rais amehuzunishwa sana na msiba huu ndio maana amenituma nilete ujumbe huu kwenu.Lakini pia nimekuja na salamu za pole kutoka kwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan. Jambo hili si dogo ni kubwa kwani tumepoteza ndugu zetu wengi. Kwa idadi hii kubwa ya ndugu zetu waliotangulia mbele za haki na wale waliopo kwenye maumivu si jambo la faraja”.


Waziri Mkuu amesema wananchi wasipeleke miili kwanza makaburini ili waweze kupitia na kutambua ndugu na rafiki kwa ajili ya kuwa na kumbukumbu ya kudumu. “Hali si nzuri ndugu zetu wameungua sana wapo wengine mnaweza msiwatambue lakini mnaweza kutambua kwa alama. Wapo wengine walivaa bangili, heleni, mkanda havijaungua”.


Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kama hawajawatambua Serikali imeweka utaratibu wa vipomo vya vinasaba, ambapo kumbukumbu hizo zimechukuliwa na wataalamu wetu wa afya. “Kama ukipita ukishindwa kumuona bado tunakuruhusu kukupima vinasaba na kulinganisha na vyakwako. Bado haki ya kumpata ndugu yako iko pale pale madaktari wapo, mitambo ipo tutachukua vinasaba na kuainisha tutatoa nafasi leo hadi saa 10 kufanya utambuzi”.


Amesema Serikali inaratibu vizuri jambo hilo lakini kuanzia saa 10 itaruhusu wale waliotambuliwa kuchukua mwili lakini kama hawajajipanga vizuri itauzika na kama kuna jina litaliandika na kama hakuna jina wataandika namba ya vinasaba ili kutoa fursa kwa ndugu siku nyingine waende wakapimwe na kuoneshwa kaburi la ndugu yao.


(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAPILI, AGOSTI 11, 2019.

Visit website
 
Majaliwa tume ya nini fukuza R .P.C,fukuza traffic,fukuza hao fire,yaani tunafedha za kuchezea hivyo
 
Pamoja na tume kwenda kubaini chanzo na makosa yake. Nadhani issue ya msingi inaonekana hakuna framework approach ya ku deal na hazardous situation. Maana ata hao polisi waliofika awali awakuwa na vipaza sauti wala seal tapes sasa sijui walitakiwa kufanya nini.

Sasa badala ya kutafuta mbuzi wa kafara wakati clearly hakuna policy approach ya ku deal na mambo kama hayo from the evidence, hiyo ripoti ikishabaini kilichojiri mwanzo mwisho; polisi, traffic, zima moto na wadau wote nchi nzima wajipange na kuja na utaratibu sahihi kutokona na mapungufu yaliyojitokeza ili kuzuia unnecessary loss of life in the future.

Lakini si kutaka kutafuta mchawi wakati ata kwenye sinema tu na international news channels tunaona polisi wa wenzetu wanavyofanya kitu cha kwanza when there is a larking hazard, na wahusika waliofika mwanzo kwa kweli hawakua equipped kuweza kuzuia watu bila kuhatarisha maisha yao.

Fire response yetu pia sio desirable huwa wanachukua muda wao sana. Kwenye ajali kwa wenzetu wanatakiwa kufika wa kwanza kama traffic kwa sababu kuna risk za moto ata kwenye gari ndogo tu isitoshe fire pia wanatakiwa kuwa trained kukata body za magari na kadhalika watu watoke kirahisi ndani ya ajali ndio watu wanavyofanya mambo.

A lot went wrong and there is so much blame to be shared around busara ni kulitumia tukio kufanya mageuzi ya utamaduni wa kudeal na ajali zenye elements za hazard.

Wewe ndio umelichambua vizuri, kungekua na Muongozo ikitokea ajali kama hio tena kufanyike nini,hivi hivi tutaendelea kuona maafa mengine yakitokea...
 
Mheshimiwa waziri mkuu nimesikia hotuba yako.
Hivi hao polisi wangejuaje kuna gari limeanguka bila kupewa taarifa.
Mheshimiwa waziri mkuu sasa ni wakati wa kuwaeleimisha wananchi kuwa mlinzi wa kwanza wa maisha ni mwananchi mwenyewe.
Gari limeanguka badala ya kupiga simu polisi wote walikimbilia kufungua tank.
Kwanza inasikitisha sana badala ya kumwokoa dereva na abiria wote wanakimbilia kwenye mafuta.
Hao wananchi hawakupiga simu polisi maana walijua polisi wangefika mapema wangetibua deal la kuiba mafuta.
Wito wangu ni hivi kama mnavyohimiza watu wazaliane himizeni pia utoaji wa elimu ili kuondoa ujinga na umaskini.
Matokeo yake ndo hayo watu wengi walio maskini na wajinga wakiona ajali wao wanaona fursa.
Tamaa zinawafanya hadi wasifikirie kuokoa hao waliopata ajali.
Moja wapo ya kazi ya polisi Ni kulinda raia pamoja na mali zao.
Polisi ili kutekeleza kazi hizo WANALIPWA mishahara ,marupurupu na pia wanapelekwa kwenye mafunzo kwa kutumia Kodi tunazotoa sisi wananchi.
Sasa kama wameshindwa kufanya kazi waliyostahili kufanya ya kuokoa maisha kwa kuchelewa kufika eneo la tukio mapema .
Ukichukulia tukio limetokea mjini kabisa jirani na stendi ya msamvu ambapo Kuna Polisi masaa 24 .
Kwenye hili suala Polisi wamezembea sana
 
Hao polisi msipopiga 112 watajuaje ? Hao wananchi waulize hata kama wanaijua 112.Ndo maana nasema tunapohimiza kuzaliana kuende sambamba na utoaji wa elimu ili kulinda ustawi wa jamii.
Acha kutetea ujinga hivi Polisi wanavyosemaga Intelligencia imetushtua kwamba kutakua na hatari unajua wanatumia kitu gani?
Hivi unajua kwamba Polisi wanakitu kinaitwa Patrol unajua maana na kazi ya patrols.
Na kwa taarifa yako hapo msamvu Kuna Polisi wanafanya kazi masaa 24 na pia Kuna gari yao ya anti robbery inapaki hapo barabarani kama point yao kubwa.
 
Hawa jamaa huwa ni wahusika pia katika uporaji mara tu ajali zinapotokea karibu na maeneo yao ya kazi.

Nilishashuhudia wakipora cement na mafuta ya diesel ajali zilipotokea pale Mlima Sekenke, Singida.

Hivyo si ajabu hata hawakuwajibika kwa wakati ili vikundi vyao vya uhalifu waibe mafuta kwanza.

Kuna mkuu mmoja wa Kituo cha Polisi Misigiri alikuwa muumini wa matukio ya uporaji kwenye ajali hizi. Pia alikuwa na vijana wake wa chini alikuwa akiwatuma.

Tuanzie hapa kama tunataka kupata ukweli.
Hivi bro mm natoka nje ya mada, hiyo ID yako Daraja Makofia ilikuwaje ukajipa ilo jina?
 
Just imagine. Walikuwa hai sema walishindwa kutoka. Watu 200+ hakuna aliowafikiria kuwatoa kwenye kichwa cha lori.Matokeo yake na wao wameteketea kwa moto kwa sababu tu ya tamaa na upumbavu wa hawa watu waliokosa ubinadamu na kuwaza mafuta tu. Hiyo adhabu walioipata inawafaa kabisa.
Kabisa, mtu kabanwa na cabin amekatika miguu watu wanashindwa kumuokoa wanawaza mafuta ya gari ambayo wakienda kuuza hawapati hata elf 50
 
Kufuatia tukio baya la ajali ya moto mkoani Morogoro Waziri Mkuu ameongea ukweli kwamba kuna viashiria vya uzembe upande wa Serikali kulikosababisha watu wengi wafe, hususani kwenye suala la uharaka wa vyombo vya Serikali Mkoa .
Hii Ni kwa kuwa kwa muda ambapo roli lilianguka na hadi kuja kulipuka kulikuwa na uwezekano mkubwa Sana kwa vyombo vinavyohusika kama vingeharakisha kufanya kazi vifo vya watu wengi namna ile visingetokea.
Kwa ushauri wangu Mamlaka zifuatazo za Serikali Mkoa wa Morogoro wakae pembeni kwani wanaweza kiathiri uchunguzi wa tuhuma alizosema waziri mkuu za uzembe.
Viongozi hao Ni;-
1. Mkuu wa Mkoa
2. RPC
3. Mkuu wa Zima Moto Mkoa.

Hawa watu wakae pembeni kwani Kuna uwezekano mkubwa Sana wa wao kuharibu au kupotosha taarifa.

Watu hawa wanatumia Kodi za Serikali kuhakikisha kwamba usalama wa raia pamoja na mali zao upo muda wote.

Kwa jinsi tukio lilivyotokea mjini tena kwenye makazi yao na siku ya tukio hawakuwa nje ya Mkoa.( Morogoro mjini)

Hawa watu wanapewa mishahara mizuri na Serikali, nyumba nzuri ,usafiri mzuri ili waweze kufanya kazi za Serikali ikiwemo ya kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao .
kwa kilichotokea Morogoro watu hao wanahusika moja kwa moja na uzembe huo anaoushuku Waziri Mkuu.
Ni vyema basi Waziri mkuu ili tume yako ifanye kazi vizuri, viongozi hao wakae pembeni
 
Hii ngoja itamwegemea mtu.
However this is Africa bhana though time will tell!!
 
Back
Top Bottom