Baada ya Tukio la MV Bukoba katika ziwa VICTORIA na kama idadi ya watu wanaohofiwa kupoteza maisha ikawa hiyo inayodhaniwa kati ya 1500 - 2000 itakuwa ni ajali ya majini kubwa kuliko zote katika historia ya Taifa hili. Huu ni msiba usioelezeka (endapo idadi itakuwa hiyo ama kuvuka)
Kwa mintarafu hiyo Uncle Lundenga na Ndugu yangu George Rwehumbiza hamna sababu yoyote ya kuwaweka Watanzania pale Mlimani City wakimkufuru Mungu huku wengine wanaomboleza. Najua mnaweza kutia pamba masikio na mkaamua kuobserve silence kwa dakika 1, lakini dhambi hii haitawatoka kamwe kama mtapuuza maono haya.
Kama kawaida yetu tutasema unajua tumekodi na kulipa gharama kubwa kwa wataalam kutoka maeneo mbalimbali ndani na Nje ya Tanzania kwa hiyo hatuwezi kupoteza fedha hizi na hakuna wa kuzilipa tena kuandaa Tamasha, Aaah nyie watu hizi fedha za nani kama si wauza vitumbua na karanga wa msata hadi mahenge ambao hawalali wakikesha kutuma meseji na kushiriki bahati nasibu wasiyoshinda hata siku moja huku shilingi zao zikiteketea kama fupa katika domo la fisi.
Ndugu zetu wapendwa wa VODACOM na LINO AGENCY INTERNATIONAL kaeni meza moja na mtafakari hili msiba huu leo ni mkubwa kwa Taifa, hatuna haja ya kusherekea kupitia matangazo ya LIVE katika Luninga kwa mabinti zetu kupita wakiwa Nusu Uchi huku mamia ya ndugu zao bado wapo majini miili yao ikiwa inasakwa na huzuni kubwa imeligubika Taifa.
Kila jambo ni mapenzi ya Mungu na kwa moyo wa Unyenyekevu kabisa natoa pole kwa familia zilizoguswa na msiba huu kwa niaba ya wana JF wenzangu.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa...Jina lake lihimidiwe
Ina lilah waina ilaih rajuun
ADIOS
Nilikuwa nasoma habari ya ajali ya kuzama meli huko Unguja na Pemba, BBC kama tulivyo watanzania wengi nao wameshindwa kuelezea ajali ilipotokea.
Habari yao inachanganya na kuibua maswali Tanzania ni nchi gani? Je Zanzibar ni Nchi au Kisiwa? Je Pemba ni sehemu ya Zanzibar? Unguja ni wapi kwenye ramani ya dunia?
Angalia hii habari na ramani iliyowekwa na BBC BBC News - Zanzibar ferry disaster: Scores die, many more missing.
nadhani tunahitaji kuweka mambo clear kutambua nchi zinazotengegeza muungano wa Tanzania.
Ukiuona mambo uliyoyaita "ya kisiasa" kuhusu Muungano yanaibuka hata msibani ujue huo Muungano uko kwenye crisis, una saratani.katika janga kama hili la msiba mkubwa wa kitaifa tuache malumbano ya kisiasa.poleni ndugu zetu wote mliofiwa na mlio majeruhi...
Walahaiwezi kuleta madhara bana japo wanapenda sana kulalamika................ unajua Muungano nikama kiinimaacho si unaona jamaa wahuko wanavyofaidihuku bara lakini waowanachomabaa za wabaraHii kitu ukiitazama kwa juu ni kama iko pouwa tu..ila ukiitazama kwa undani ni kama unaweza kushangaa
Usiku wa jana ...huko Zanzibar au Tanzania Visiwani..wamepatwa na msiba mkubwa sana..wakupoteza watu wengi kwa ajari ya meli
Leo jumamosi..Tanzania Bara tunafanya shindano kubwa la urembo ..Vodacom Miss Tanzania..kumbuka Miss Tanzania haina mshiriki toka Zanznibar(Tanzania Visiwani)...
Je hii haiwezi kuzua mjadala...kwa wazanzibari
Ni wangu mtazamo
<br />
<br />
Mkuu naungana na wewe kushangaa. Vyombo vingi vya habari vime cover hii habari,tena vingine live. Inasemekana zaidi ya watu 100 wamekufa na maiti wamezionyesha.Maskini ya mungu sisi radio na tv toka asubuhi vinapiga mziki na kuonyesha katuni! Hata wenzetu wa nje wanatushangaa kwa kweli.
Basically,hili shindano lenyewe ni laana tu,uwa nashangaa watu wana sababu nyingi tena za msingi kutetea uchafu huu, wengine watakwambia kuwa tunatangaza utamaduni? Je,utamaduni wetu ni kuvaa machupi na kuacha matiti wazi? W engine watakwambia ni ajira kwa vijana,Je,hao wasichana wakitoka hapo uwa wanafanya nini?
Kama sio upuuzi wa akina Wema Sepetu na umalaya wake....Hili shindano ni la kuzalilisha dada zetu na mama zetu....na kwa hakika dhambi hii itamla huyu Hashim Lundenga...kazi yake ya kuwaanika dada zetu kwa mabedeshee ili wanunulike si haki na wala halipaswi kuvumilika kabisa na kila mtu anayemuheshimu Allah(Mungu).....
Huyu jamaa anakusanya mabilioni kupitia kuwaweka uchi dada zetu....MIMI NAUNGA MKONO HOJA KUWA HILI SHINDANO LIFUTWE KABISA NA SIO KUAiRISHA KWA SABABU YA VIFO VYA WENZETU KULE ZENJI.....
Mungu awatie nguvu wafiwa,maana kifo ni jambo lisilozoeleka...
we unaishi dunia gani? Hata china kwenye sheria kali hawana mawazo kama yako. Ni tatizo la watu wanaofanya kazi serikalini wanaoweza kuwaza kama wewe