Ajali ya bodaboda yaua

Ajali ya bodaboda yaua

Inauma sana. Asubuhi hii hapa Suka, Kimara ajali ya bodaboda na daladala imeua. Usafiri huu umekuwa balaa kubwa. Fikiria, mtu kaacha familia. Anakwenda kusaka riziki halafu maisha yake yanakatizwa namna hii. Inauma sana.

Madereva wa bodaboda jamani kwa kweli hawafuati sheria na wako rafu sana kwenye uendeshaji. R.I.P
 
Kimaadili picha hizi si nzuri. Polisi walifika na WP anashirikiana na wananchi kuweka mchanga kwenye lami ili kufuta damu. Inasikitisha sana.
 
Nyingine imeua jana usiku maeneo ya kibamba darajani.
 
bodaboda zinamaliza vijana tunaotegemea walete mabadiliko katika nchii hii huku serikali ya ccm ikipuuzia uteketeaji huu wa nguvu kazi ya Taifa pasipo kuchukua hatua za makusudi.
 
Inauma sana. Asubuhi hii hapa Suka, Kimara ajali ya bodaboda na daladala imeua. Usafiri huu umekuwa balaa kubwa. Fikiria, mtu kaacha familia. Anakwenda kusaka riziki halafu maisha yake yanakatizwa namna hii. Inauma sana.

Pole kwa wafiwa!
mkuu Manyerere Jackton so sad, niliona hiyo ajali nikiwa katika dala dala natokea Mbezi kwenda kibaruani, ktk siti nilikaa na bidada mmoja, km dk 10 baada ya kuishuhudia ajali hiyo, bidada kapokea simu kuwa baba yake kapata ajali ya bodaboda wakati anaenda kazini kwake! Mimi pia Jumapili mbili zilizopita tulikuwa Tanga tunamzika shemeji yangu waligongwa na gari wakiwa ktk bodaboda, shemeji alikaa icu 3 days, Sewahaji akakaa 3 days, his life came over! Boda boda hizi!
 
Last edited by a moderator:
hawa vijana nafkiri wangepewa elimu ya kutosha kuhusu usalama barabarani maana wanajiendea tu kutakashindana na magari Mungu ampumzishe kwa amani marehemu
 
Wafe tu wanakunywa viroba kila saa
Sio busara kuwa na roho nyeusi kiasi iko!!kama hujawahi kupoteza ndugu,rafiki,mzazi au mpenzi kwa ajali ya bodaboda nakuelewa,lakini sio busara bado bora ungejisemea kimoyomoyo!!
 
Inauma sana. Asubuhi hii hapa Suka, Kimara ajali ya bodaboda na daladala imeua. Usafiri huu umekuwa balaa kubwa. Fikiria, mtu kaacha familia. Anakwenda kusaka riziki halafu maisha yake yanakatizwa namna hii. Inauma sana.
Mzee Lowasa anasema hizi ni ajira kwa vijana. January Makamba anasema ni ajira kwa vijana.......hapa wakimaanisha vijana ni wavulana tu, wasichana wao wakaolewe, hawahitaji ajira.

Huyo ndo rais anaeaza ajira kwenye level ya bodaboda.
 
Tunahitaji mjadala wa kitaifa kujadili hatima ya bodaboda na vijana wa taifa hili. Maafa ni makubwa mno.
 
Back
Top Bottom