Nipo safarini kwenda mlandizi,ila maeneo ya MADAFU basi la Tahmeed limepata ajali baada ya kugongana na toyota pickup,na semitrailer,
trafiki ndo anachukua maelezo na kupimapima,hakuna mtu aliyekufa
dah! Basi zangu enzi hizoo niko horohoro, chases na engine ni fuso, ua nissan ud,bodi imechongwa master hapo kenya mwendo wake usipime,mwarabu kashakula tambuu,pariki na kuberi plus mirungi imejaa mdomoni. Namshukuru Mungu kama wamesalimika watu.
Mwendo kasi umekuwa tatizo kwa mabsi mengi, na cha ajabu mara nyingi watu wakiwa ndani ya basi na likawa linakimbizwa vibaya sana huwa wanakaa kimya likipata ajali wakisalimika ndio wanaanza lawama dereva alikuwa anakimbiza sana mlimwambia hapa, ama oh tulimwambia ila hakutusikia kitu ambacho si sahihi hata kidogo abiria mna nguvu zaidi ya dereva kitendo cha yeye kuendesha gari hakimaanishi basi anaweza kufanya lolote atakalo.
Nwatakia kheri hao waliopata ajali.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.