Ni kweli ajali haina kinga hasa inapokuwa si kosa lako, lakini pia hakuna ajali isiyo na sababu.
Tunajua ikitokea ajali ya gari polisi huja na kamba kamba zao kupima. Kwenye ajali kubwa kama hii wanatakiwa kutoa ripoti ya ajali.
Vya kuchinguzwa ni vingi. Je gari lilikuwa na ubora wa kuingia barabarani au lilikuwa na hitilafu zilizopuuzwa? Dereva alikuwa na hali gani? Alichoka au alikuwa anasinzia au kalewa? Simu yake ichunguzwe kama alikuwa anatext au anaongea wakati wa tukio. Je ajali ilisababishwa na mwendo mkali?
Mazingira ya barabara yalikuwaje? Kulikuwa na mvua. Kulikuwa na ukungu? Barabara ilikuwa mbovu? Gari lilikuwa limejaa kupita kiasi? Kulikuwa na gari jingine lilisababisha ajali hiyo? Ni muda gani ulipita kabla ya huduma ya kwanza kufika. Waliofariki walikufa kwa ajali au kuchelewa kupata matibabu?
Maswali ni mengi yakipatiwa majibu sababu ya ajali itajulikana. Ikijulikana sababu hatua za kuzuia ajali ya namna hiyo zitaweza kuchukuliwa.
Kujua chanzo cha ajali ni muhimu sana hasa kwa wafiwa. Pole haitoshi, hapo ni malipo kwenda mbele. Kama mwenye gari alitembeza gari bovu ashtakiwe. Bima yake itumike kufidia wafiwa. Kama barabara ilikuwa mbovu damn it! hapo halmashauri au jiji laweza kushtakiwa na kudaiwa mamilioni ya fidia.
Tusiwe watu wa kukubali matokeo kirahisi rahisi. Sababu ya ajali ipatikane. Kama kuna
aliyesababisha ajali atumbuliwe. Hata kama amefariki kuna namna za kumuwajibisha. Kama kuna kilichosababisha ajali kijulikane ili kidhibitiwe kisije kusababisha ajali nyingine siku zijazo.