AJALI: Watu kadhaa wafariki wakitokea Rombo kwenye Miaka 40 ya CCM

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,874
Kuna ajali imetokea Rombo jioninya tarehe 05/02/2017.

Viongoz wa CCM waliokuja kushiriki miaka 40 ya ccm Kimkoa iliofanyika wilayani Rombo akiwapo MNEC wa Same wamepata ajali maeneo ya Mwika wakirejea makwao toka Rombo.

Kwa taalifa za awali watu watano wamefariki ktk ajali hiyo.

Gari hiyo ilikuwa ni ya MNEC wa SAME na alikuwa amebeba Wanavyuo pia

========

UPDATE:

Timu ya waandishi waliotoka Moshi kwenye sherehe za miaka 40 ya CCM Moshi yapata ajali.

Inasemekana watu kadhaa wamefariki papo hapo.

Ajali imehusisha fuso, bodaboda na gari nyingine waliokuwemo waandishi pia.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari wa Majira, Flora Temba kwenye gari walikuwemo watu watano na wanne wamefariki amepona Kimambo Jackson aliyekuwa anaendesha gari.

Chanzo cha ajali kinadaiwa kuwa ni Fuso lililokuwa nyuma kufeli breki kisha kuwagonga na kuwasukuma kwenda mtaroni kisha kugonga pia Bodaboda na Fuso kwenda kupinduka.

Waliofariki inadaiwa ni zaidi ya wanne kwakuwa kuna waliokuwa kwenye Fuso pamoja na mwendesha bodaboda.

Taarifa za awali zinaonyesha waliofariki ni mwandishi Arnold Swai kafariki. Mwandishi mwingine wa gazeti la Habari leo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Hai.

Taarifa zaidi zinasema walikuwa kwenye shughuli za chama (CCM) wilayani Rombo.

IMG_2972.JPG

IMG_2970.JPG

IMG_2971.JPG


Hawa hapa viongozi wa UVCCM na CCM waliofariki kwenye ajali ya gari jana Rombo:


Anold Swai (M/kiti UVCCM Hai)

Ally Mmbaga(MNEC Same)

Edwin Msele (K/Hamasa Shrk Kilimanjaro)

Anna Malamsha.

Ajali imetokea maeneo ya Mwika Mawanjeni maarufu kama Bar Mpya Moshi mkoani Kilimanjaro. Inaelezwa kuwa ndani ya gari walikuwemo watu sita wakiwemo viongozi wa CCM wakitoka kushiriki sherehe za miaka 40 ya CCM kimkoa yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi Shauri Tanga wilayani Rombo. Chanzo cha ajali inaelezwa kuwa ni fuso kufeli breki na kuligonga gari dogo.

“Waliofariki ni mwenyekiti wa Uvccm wilayani hai na mwandishi wa habari Leo Arnold Swai, mjumbe wa NEC ya CCM na Katibu wa CWT mkoa wa Kilimanjaro ally Mmbaga na wanafunzi makada wa CCM kutoka vyuo vikuu vya ushirika na KCM. Majeruhi wa ajali hiyo ni Jackson Kimambo amekimbizwa Hospitali na wote walikuwa wakitoka kwenye maadhimisho ya kilele cha miaka 40 ya kuzaliwa CCM wilayani Rombo” -Ujumbe wa mwandishi wa habari Lucy Ulomi ambaye sasa yupo hospitali ya KCMC akifuatilia habari hiyo.
 
Kuna ajali imetokea Rombo jioninya tarehe 05/02/2017
Viongoz wa CCM waliokuja kushiriki miaka 40 ya ccm Kimkoa iliofanyika wilayani Rombo akiwapo MNEC wa Same wamepata ajali maeneo ya Mwika wakirejea makwao toka Rombo.

Kwa taalifa za awali watu watano wamefariki ktk ajali hiyo.
Gari hiyo ilikuwa ni ya MNEC wa SAME na alikuwa amebeba Wanavyuo pia,ajali imetokana na kugongana na fuso
View attachment 467549
Hawa walikua na mwendo mkubwa sana,
 
Siasa zimetufikisha mbali,kutofautiana kiitikadi kusitufanye kuyafurahia mauti ya "wasiokuwa sisi"

Mauti ni mlango,kila mmoja ataupita bila kujali itikadi yake ya kichama,kidini au utaifa.

Wapumzike kwa amani waliotangulia.




Iulize serikali iliyowahi kuutesa mwili wa Kamanda Arphonce Mawazo(R.I.P),mbali na kuuwawa kinyama,walijaribu kuzuia hadi mazishi yake,sijuwi walitaka wamle nyama?Ilitubidi hadi tuiombe mahakama ili itupe haki ya kumzika kamanda wetu,Tukio la kuuwawa kwa Mawazo na kisha kuzuiwa asizikwe kwa heshima aliyostahiri kulinifanya niichukie policcm zaidi ya ninavyomchukia ibilisi.

Mkifa ninyi ndiyo mnakumbuka kuwa kifo ni mlango ambao kila mtu ataupitia,tukifa sisi hamuoni hata haja ya kuchunguza chanzo cha kifo chetu,mnakuja na majibu mepesi tu kwamba ni wahamiaji haramu,mpinzani nchi hii ana thamani ndogo sana,anazidiwa hadi na Faru John ambaye mwenyezi Mungu alimuumba ili awe kitoweo,lakini kifo chake kilipewa umuhimu mkubwa zaidi ya mwanadamu.
 
Back
Top Bottom