AJALI: Watatu wamefariki na 24 kujeruhiwa baada ya basi la Hamandos kutumbukia mtoni

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Watatu wamekufa na 24 kujeruhiwa baada ya basi la Hamandos kutoka Haydom kwenda Mbulu mjini kutumbukia mtoni.

-------

Watu watatu wamefariki dunia na wengine 24 wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Haydom, kuelekea Mbulu Mjini, kuingia mtoni.

Ajali hiyo imetoka leo asubuhi, ambapo basi hilo limeingia kwenye mto ambao hauna maji uliopo kilomita chache kutoka mji mdogo wa Haydom.

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga alisema ajali hiyo ilihusisha basi la abiria la Kampuni ya Hamandos lililokuwa linatoka mji mdogo wa Haydom likielekea Mbulu Mjini.

Mofuga amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi hilo kukatika usukani (sterling road) na kukosa mwelekeo kisha kuingia mtoni na kugonga kingo za mto huo.

Amewataja waliofariki dunia ni Gidaguy Samo (65) mkazi wa Kijiji cha Basodesh, Josephina Nade (45) mkazi wa Kijiji cha Gdihim na Neema Petro Amma (25) mkazi wa kijiji cha Haydarer wilayani Mbulu.

Mkuu huyo wa wilaya amesema miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Haydom na majeruhi hao 24 wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo.

Amesema watu 27 walipokelewa kwenye hospitali hiyo, watatu walifariki dunia, kati ya 24 walio majeruhi, wawili bado hawajapata fahamu.

“Majeruhi wanaoendelea kupata matibabu ni Sulemani Hussein, Samweli Zacharia, Katarina Daniel, Loth Baha, Captolina Lohay, Daniel Sanja, Felistiani Anthony na Dengu Matle,” amesema

Amewataja majeruhi wengine ni Julieth Lowry, Grace Tumaini, Fanuel Thomas, Sabrina Thomas, Hagai Daniel, Edward Petro, na Olivery Fuumay.

"Majeruhi wengine ni Gersael Akonaay, Sese Gwayadesh, na Daniel Gilengana" amesema Mofuga.

Majeruhi wengine hawakuweza kufahamika mara moja majina yao.


Mwananchi
2.jpg
1.jpg

 
Chachu ombara na breaking news za maajali

Mola warehemu walioiacha dunia na waliojeruhiwa wawe mikononi mwako wakati wakishughulikiwa na madaktari
 
Hatari sana uzembe barabarani
Mkuu subiri walete sababu zaidi kuhusu chanzo. Ukisema uzembe barabarani sina imani...maana huko kuna barabara za vumbi tupu alafu kuna kona kali sana huko....ngoja walete info zaidi
 
Wapumzike mahala pema waliotangulia mbele ya haki na Mungu awajalie unafuu majeruhi..

So sad
 
Wakuuu..
Hilii Basii Lazma litakua nimiongoni mwa yale magari yanayosubiri ifike tarehe 01/07/017..
Hili limeingia mapema barabarani..
 
Inasikitisha kuona bado barabara zetu zinaendelea kugharimu uhai wetu, Mungu awatangulie majeruhi wote wakapate kurudi hali zao za kawaida. Wapumzike kwa Amani waliotutangulia
 
NIMEPANDA SANA HAYA MAGARI..... RUTI HIZO ZA MBULU HAYDOM.

POLENI WAFIWA.
 
Back
Top Bottom