Ajali tena-wanakwaya 11 rai wa kenya wafa katika ajali ya basi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali tena-wanakwaya 11 rai wa kenya wafa katika ajali ya basi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bemg, Aug 11, 2012.

 1. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  WATU 11 wanaoaminika kuwa raia wa Kenya wamefariki dunia papo hapo, huku wengine saba wakiwa mahututi baada ya mabasi waliyokuwa wakisafiria kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam kupata ajali katika Mto Wami mkoani Pwani.Mbali na vifo hivyo, ajali hiyo pia ilisababisha majeruhi 25 na saba kati yao waliripotiwa kuwa mahututi na walipelekwa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha kwa matibabu.Ajali hiyo ilitokea katika Kijiji cha Makole, wilayani Bagamoyo wakati abiria hao ambao ni wanakwaya walipokuwa wakisafiri kutoka Kenya kwenda Dar es Salaam kushiriki katika tamasha la uimbaji.

  Ajali hiyo ilitokea jana saa 11 alfajiri ikihusisha magari manne, mawili kati yake yakiwa ni mabasi hayo yakitokea Kenya na malori mawili ya hapa nchini.Tukio hilo pia lilifunga Barabara Kuu ya Chalinze - Segera kwa zaidi ya saa nane hivyo abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea na kutoka mikoa ya Kaskazini ikiwamo nchi ya Kenya kwenda na kutoka Dar es Salaam kukwama.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu alisema raia hao wa Kenya ni waumini wa Kikristo na walikuwa wakielekea Dar es Salaam kwenye tamasha la kwaya.

  Source Mwananchi

  Wakti huo huo nipashe linahabari za basi la kampuni ya Allys Sport Bus linalosafirisha abiria kutoka Dar es Salaam na Mwanza liliacha njia na kupinduka baada ya kutokea ajali inayodaiwa kusababishwa na basi la Shabiby lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kwenda Dar es Salaam na kusababisha mabasi matatu kuacha njia eneo la Mkundi Makunganya barabara kuu Dodoma-Morogoro ambapo katika ajali hizo zaidi ya abiria 40 walijeruhiwa mkoani hapa.
   
 2. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Poleni wafiwa na wale waliopata majeraha Mungu awaponyeshe.
   
 3. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Inshu iko toka jana hii,nilidhani we leo umeambatanisha na picha za tukio
   
Loading...