Ajali Tabata leo

Chibidu

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
387
49
Kuna taarifa kuwa kuna ajali imetokea Makutano ya Tabata relini. Roli la mizigo limegonga daladala ya Ubungo Tabata watu kadhaa wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa. Dereva wa Roli inasemekana amekimbia. Mwenye taarifa zaidi atupatie tuweze kupata taarifa zaidi za ajali hiyo.

Chanzo: Habari kwa ufupi Radio One (saa nne asubuhi)
 
heeee mungu wangu ndo njia yangu hiyo sema niliwahi mapema kama kuna marehemu rip
na walioumia mungu awaponye haraka
 
JAMANI INASIKITISHA HIZI AJALI JAMANI.ndugu zetu wamepoteza maisha hapo asubuhi hii?
Ninasikitika sana na naomba tupate majina ya hao ndugu zetu marehemu. Polni sana ndugu wa wapendwa waliotutangulia jamani
 
Yaani madereva tusifupishe Maisha ya Watanzania Kwani hali ngumu ya maisha na mfumuko wa bei vinatosha kutupunguza.

RIP marehemu wote.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Poleni wote mliopata hayo matatizo kwa namna moja au nyingine
 
kila kitu madereva mara nyengine ma breki tu yanabuma,matajiri wagumu kufanya service za gari hata wakiambiwa kuwa gari ina tatizo hawaelewi,daladala za mjini huwa zinaendeshwa kimiujiza breki za kuchochea,taa za breki nyuma haziwaki(wakati ndio alama muhimu ya kumshtua anaekuja nyuma kuwa wa mbele kasmama au yupo katika harakati za kusimama)
yote haya yaangaliwe ili kuepusha ajali!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom