Ajali: Mwenye taarifa ya ajali iliyotokea jana naomba anipe maelezo

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,944
2,458
Nimepata simu niwahi Bugando hospital kutambua mwili wa ndugu yangu.

Kafariki kwa ajali ya bus jana saa 11 jioni maeneo ya Bunda na maiti zinasafirishwa toka Bunda muda huu.

Mtoa taarifa hana details zaidi, naomba kama kuna mwana JF, mwenye taarifa zaidi juu ya ajali hii atujuze, maana sijasikia lolote toka kwenye media zetu pia mpaka muda huu.
 
Atakuwa dereva wa bodaboda alilaliwa na bus wawili walikufa palepale mmoja alifia njiani hakuna abiria aliyepoteza maisha
 
Hata mimi nimesikia asubuhi ya leo kuwa jana kuna ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Kisire ilipata ajali maeneo ya Bunda, sina taarifa iliyo nzuri Mkuu.
 
Nimepata simu niwahi Bugando hospital kutambua mwili wa ndugu yangu.

Kafariki kwa ajali ya bus jana saa 11 jioni maeneo ya Bunda na maiti zinasafirishwa toka Bunda muda huu.

Mtoa taarifa hana details zaidi, naomba kama kuna mwana JF, mwenye taarifa zaidi juu ya ajali hii atujuze, maana sijasikia lolote toka kwenye media zetu pia mpaka muda huu.
Sehemu hiyo ni kona ya Balili ambapo hiyo basi ilikuwa ikipanda mpando wa balili na ilipofikia kwenye kona hiyo dereva akashindwa kulimudu na kunyooka moja kwa moja na hatimaye dereva kuruka na kuliacha basi likiwa na abiria tu na matokeo yake kupinduka na kumlalia mtu mmoja na pikipiki tano ambapo huyo mtu alifariki baadae.
 
Back
Top Bottom