Waziri Mhagama na uongozi wa Wizara ya Afya, anzisheni haraka Health Information Call Center kuokoa wananchi maskini

PMWAKA

Senior Member
Aug 29, 2019
194
207
Kwa niaba ya watanzania, Mhe. Mhagama naomba pitia huu ushauri kuhusu wizara ya Afya na msaada kwa wananchi.

Serikali chini ya Rais wetu mama Samia naomba muanzishe HEALTH INFORMATION CALL CENTER.

Kuna wananchi hua wanahangaika sana wakati wamepatwa either na magonjwa au ajali wameumia nk.

Ila unakuta wanahangaika na kupoteza gharama nyingi kuzunguka hospital kadhaa za serikali bila solution na washamaliza ka akiba kote kwa gharama za nauli, za hospita nk cas hawana bima itakayowawezesha kumuona bure dr.

na kumbe wanakuja kupewa taarifa kua hospital flani, tena ya selikari ina hiyo huduma, na gharama yake ni kiasi flani, kiasi ambacho walikua nacho tangu mwanzo, lakini sasa wameishiwa hawawezi afford tena sababu ndugu wa mgonjwa hawakupata taarifa kama hiyo haraka, ili wasiharibu gharama kwenda sehemu zingine, hivyo mgonjwa anaweza kua mlemavu sababu alikosa taarifa kwa wakati, za mahali gani aende kuna Dkt. bigwa.

Mhe. Waziri Mhagama, nakuomba kama mkuu wa wizara hii, anzisheni online phone call ya kupata taarifa sahihi kwa wagonjwa wa magonjwa makubwa tu, (sio whatsapp), kama ile 112 ya polisi, au ingine special, ambayo mwananchi akipata changamoto ameenda hospital hajapewa solution ya kuaminika, basi wasiliane na madaktari kwa hiyo number, aeleze ana tatizo gani, kisha wao sasa ndio wamdirect, kua kwa tatizo lako basi inakubidi ufuate utaratibu huu na uende hospital flani iko mahala flani ili ukaonane na madr wabobezi wa hilo suala. utaratibu ni mfano kama hiyo hospital anayodirectiwa aende ni lazima apate rufaa kwanza au ni vipi ili kuwapunguzia gharama wananchi maskini na kupoteza fedha nyingi kuzunguka huku na huko.

Nimeshauri haya leo sababu nimeona mala 4 hii issue, na ya sasa ni ya 5, jamaa flani alipata ajari ya gari, amehangaika mala bugando wanamwambia hivi, mala hospital ya wilaya wanamwambia hivi na kumpa dawa hata hazioneshe kusaidia, hadi bima imeisha juzi, then ndio ndugu wanakuja kuambiwa na jamaa flani ambae pia ni dr tena dr bigwa wa magonjwa ya kina mama, na drs wengije wawili kua kwa walivoona info zote kwenye file la mgonjwa, alizokua anapewa hospital wakashangaa na kusema, ila mbona hawakumwambia jambo fulani tena dogo tu? au ni mdr fresh graduate?

Mlikosea sana kumpekeka sijui bugando sjui wapi akati mngempeleka MOI au hata KCMC au hospital flani (wakazitaja) angeshakaa sawa mda mrefu hizo neuro system zake, nyie mkampeleka bugando.

Ndio ni kweli bugando wako vizuri sana kwenye issue zingine, but issue ya neuro system bado wako chini sana, yani bado wanajifunza, nahizo za mkoa sjui wiraya ndo kabisa hawawezi kukupa jibu la uhakika, mmepoteza gharama bure na anaweza kulemaa kabisa msipofanya haraka.

Sasa hizo hospital zenye mabigwa wa magonjwa flani tu, watu wanazijuaje? zingine hata hao mdr wadogo wadogo hawazijui, huyu mwananchi anajuaje?

Wapeni wananchi taarifa if kunachangamoto wanapitia ya shida ya kihospita muwadirect waanzie wapi, sio kila hospital ina mdr bigwa wa kila kitu, nimejiskia vibaya sana, mtu anafell jambo kwa kukosa information tu kwa wakati kweli?

Anzisheni call center itayokuainawapa taarifa muhimu watu wenye magonjwa makubwa au shida kubwa tu ili iwe rahisi kwao kuwahi kabla mambo hayajaharibiwa zaidi.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom